Kama unasoma ili utambulike kua umesoma chuo fulani then unapoteza muda, maana edx ni sehemu unajisomea mwenyewe tu kama tuition vile, na cheti ukilipia wanakupa ila huwezi kitumia kama cheti cha chuo.
Ila bado nakushauri usome, hiyo ni course moja tu kati ya nyingi, hapo ukiimaliza hujagusa hata 2% ya computer science, CS50 hata mimi niliisoma hiyo course online nilipokua mwaka wa kwanza chuoni na ilinisaidia sana kupass courses nilizokua nasoma chuoni kwa kua nilikua sina knowledge ya programming kabla sijaingia chuoni. Ni course nzuri sana na inajaribu kukuonyesha what's possible kwenye Computer science, japo haiingii deep sana, wanagusia juu juu lakini wanachofundisha ni fundamentals ambazo kila mtu inatakiwa ajue. Na mtu asikudanganye kua haya mambo huwezi jisomea mwenyewe, kwani anayekaa darasani anafundishwa na mwalimu, na anayekaa kwenye internet anaangalia mwalimu akifundisha wana tofauti gani? Kama una swali hata comment section, stackoverflow zipo unauliza watu wanakujibu haraka tu tena mara nyingine vizuri zaidi kuliko mwalimu wako wa darasani. Kitu kigumu kujisomea mwenyewe mi naona ni hardware tu.
Ukisoma CS50 ukaimaliza na ukaelewa vizuri, unaweza ukajisomea na courses nyingine pia, hawa jamaa wanatema madini ambayo hutokutana nayo kwenye vyuo vya Tanzania, course za lazima kuchukua Algorithms and Data Structures, ningeshauri pia uangalie na Introduction to Data mining, hadi kufika hapo utakua unajua mwenyewe direction ipi unataka kwenda, kama ni kwenye games, robotics, web, mobile, au general application software kusolve matatizo mbalimbali kama kilimo kwa kutumia drones e.t.c Unaweza jifunza online yote haya na ukayaelewa, sema usitegemee cheti, kama unasomea cheti then unapoteza muda na utaishia katikati haya mambo yanazidi kua magumu na mengi mno unavyoenda juu.