GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 3,593
- 4,652
Kama nimekuelewa vizuri biashara yako inahusu fani yako.Hiyo ni faida kubwa kwako maradufu.Kwa kuwa bado ni mwajiriwa miezi sita ya kwanza jipange vizuri na wewe na mkeo mjiandae kisaikolojia,pesa ya mshahara unayoipata ifanyie utaratibu wa akiba kwa miezi kama sita hivi.Baada ya huo muda omba likizo ukasimamie mwenyewe biashara yako na ufanye udhibiti mzuri wa mapato na matumizi yako katika kipindi chote cha likizo yako nzima.Iwapo utaifanya biashara yako ambayo kama ulivyosema ndiyo fani yako kwa ufanisi katika kipindi cha likizo yako, utakuwa tayari umejifunza mazingira ya ofisi yako mpya.Baada ya likizo nenda kaage kazini kuwa maisha yako sasa yako katika mikono na akili yako badala ya kutumiwa na tume taa kwa ujira mdogo hivyo.Niamini baada ya miaka mitano utagundua na kujutia muda uliopoteza kwa kuajiriwa.Karibu katika maisha ya kweli.