fieldmashal
Member
- Nov 22, 2015
- 78
- 3
Ikiwa ni mwaka wa pili sasa tangu nijiunge na chuo hiki Cha udom, naona maisha yanazidi kuwa magumu kila uchao ni bora ya jana, hali inayonifanya nisononeke sana na kutaka kuacha masomo Kwani kila jitijada ninayofanya najikuta imegonga mwamba,
Nilimaliza form six 2013, nikafauru hivyo nikaaply chuo nikapata ila mkopo nikakosa ikanilazim kuahilisha mwaka, hivyo nikatafuta tempo ya kufundisha huku nikisubiri mwaka mwingine wa masomo ili niweze kuapply tena, Mungu ni mwema mwaka ukafika, uzuri nikawa nimepata vihela kidogo nikatumia kufanya application tcu na bodi ya mikopo.
chuo nikapata udom edn bahati mbaya zaidi mkopo nikakosa tena, hivyo nikapata ushauri kutoka sehemu mbalimbali kuwa ikiwa chuoni kuna muda wa kuappeal pia, hivyo nikatumia hela kidogo ambazo nilipata wakat wa tempo kwenda kuripoti chuo, kweli muda wa kuappeal ukafika nikaappeal kwa kuwa nilikuwa na kila sababu ya kuappeal, mimi ni yatima na nilikuwa nasomeshwa na serikali kutoka secondary ya chini hadi ya juu, nikaappeal nikakosa tena.
hivo maisha yakawa magumu Sana hadi nikawa natamani kujinyonga, nikapata ushauri tena kutoka Kwa wadau mbalimbali nikaona ni vema kuvumilia, mid semister ikaisha brother akajitahidi japo na yeye maisha ni magum akalipa Ada ya semister ya pili, hivo nikajikaza tena nikarudi chuoni maisha yakaendelea, nikiwa sku nikipata chakula nashukuru mungu nikikosa, siku nikikosa chakula naenda tu cafeteria nakula mabaki waliobakiza wanafunzi wenzangu sku inapita.
maisha yaliendelea kuwa magumu Hadi ue (university examination) nikafanya chuo kikafungwa na kwenda field, da maisha yalikuwa magumu zaid, waliposema field haifanyiwi vijijini, bali ni maeneo ya mijini tu na mimi nakoishi ni vijiji Sana,
daa niliumia sana,hivyo nikaenda kuripoti field nilihangaika Sana, hadi nikataka kuacha field, wazo likanijia La kuongea na mkuu Wa shule nikamueleza hali halisi kwa uzuri akanielewa, akanipangia vipind na kusema nimaliza kipindi changu ninaweza kuondoka maeneo ya shule, pengine ikitokea siku sina kipindi niko huru kutofika shuleni.
maisha yakaendelea, nikatafuta kazi moja ngumu sana ambayo kwa msomi wa kawaida hawezi kuifanynya, mimi niliifanya kwa lengo La kupata hela ya kula na kufanya application bodi ya mikopo.
Nikafanikiwa kutuma form na kusubiri majibu tena
Wakati nasubri majibu ya bodi niliendelea kufanya kufanya kazi, mbalimbali kwa bidii zangu zote, hadi nikafanikisha kupata ada ya chuo pamoja na direct cost.
Muda ukafka tena bodi ya mikopo wakatoa majina kwa mara ya kwanza, jina langu halikuwemo tena, kichwa kikachemuka, badae nikauliza watu mbalimbali kuwa vipi majibu ya continuing students, nikapatapa tetesi kuwa majibu ya continuing hatoki online yanatumwa direct kwemye chuo husika, mmm nikajipa moyo kwa kuwa Ada na direct cost nilikuwa nimepata niona kwamba, goja niende chuoni majina yatanikuta huko hivyo nikaanza Safari ya kwenda chuoni hadi nikafika chuoni.
Nilipofika chuoni kweli nikakutana na watu wengine wenye matatizo yanayo fanana ya yangu ila njaa tunatofautiana nikaona njaa yangu ni kubwa sana, hivyo nikaulizia kuhusu majina ya continuing students wadau wakesema soon watatoa kwahiyo tusijari.
Maneno hayo yalinipa moyo nikatoa hela zote nilizokuwanazo ili kufanya usajiri ,baada ya muda nikaona kimya hakuna majina wala rafiki yake na majina hadi sasa niandikapo taarifa hii.
Nimechoka zaidi baada ya kuona bodi ya mikopo wamefungua dirisha la kuappeal ndo nikajwa mimi ndo imetoka hvo tena.
Kwa sasa najiuliza nitaishije hapa chuon, wandaful zaidi kuna brother wangu ambae kidogo alikuwa akinisaidia pindi niwapo chuoni, sasa na yeye ni mgonjwa HIV /AIDs positive na hawezi kufanya kazi yoyote, je mimi kwa sasa nitaishi vipi hapa chuoni ukizingatia na ratiba ya chuo ilivyo ngumu kiasi kwamba huwezi hata siku moja kwenda kufanya kibarua chochote.
Jamani wasomi wenzangu ebu naombeni ushauri wenu pengine mtanisaidia Sana, Mungu awatangulie ili muwezo kunipa mwelekeo wa maisha, kimawazo, fikira ata finential support kwani haya ni maisha, Karibuni Sana .