Ushauri: Namna ya kupangilia mshahara

mikumiyetu

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
1,312
944
Habari ya Jumapili wadau,

Mimi kijana wa miaka 25 ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea kuna kazi naifanya ambayo kwa mwenzi huwa inaniingizia kipato cha laki tatu(300000). Sasa nilikuwa nahitaji mpangilio mzuri wa matumizi wa haka kamshahara kangu ili nipate kubaki na akiba hata wazazi siku wakihitaji msaada wa kifedha nipate kuwasaidia.

Naombeni ushauri wenu mlionitangulia katika maisha ya kujitegemea.
 
fanya kwanza cash multplication yan hyo laki 3 iwekeze alafu fedha zikiongezeka....uje tukushauri cha kufanya........
 
siwezi kuiwekeza yote sababu kuna mahitaji hapo kama pesa ya kula na vitu vingine vidogo vidogo inatoka hapo hapo
 
Habari ya jumapili wadau,mi kijana wa miaka 25 ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea kuna kazi naifanya ambayo kwa mwenzi uwa inaniingizia kipato cha laki tatu(300000) sasa nilikuwa nahitaji mpangilio mzuri wa matumizi wa aka kamshahara kangu ili nipate kubaki na akiba hata wazazi siku wakihitaji msaada wa kifedha nipate kuwasaidia.Naombeni ushauri wenu mlionitangulia katika maisha ya kujitegemea
Japo kuwa ujasema kama umepangisha ama hujapangisha ,
Lakini pia kama huna fenicha za Ndani isiwe ishu
Nakuambia tuu kwa utashi wangu
Anza kununua godoro , mashuka na neti achana kitanda kwanza
Weka stock ya Chakula na gesi ya miez miwili au mitatu
Usiwe na papala tunza pesa ktk hiko kpnd cha miez mitatu .

Mwezi ujao kawakatie bima ya afya wazazi wako na wewe pia .

Baada ya hapo sasa unatakiwa ujali mda, pesa uiheshimu , kama mnywaji na mvutaj acha .

Weka urafiki na majilani . jitahdi kuwa mshauli na msuluishi maana itakujengea nafasi ya kupata msaada utakapo teleza

Weka malengo ya kupanga mda mfupi , ujibane ukajenge utakuwa huru zaid na mfano wa kuigwa

Kuna mengi nimeacha lakini unatakiwa ujibane avoid magrupu lelemama
 
Me nakushauri utafute njia nyingine ya kukuongezea kipato yaani usitegemee kazi moja hapo ndo utaweza kuweka akiba.
 
Japo kuwa ujasema kama umepangisha ama hujapangisha ,
Lakini pia kama huna fenicha za Ndani isiwe ishu
Nakuambia tuu kwa utashi wangu
Anza kununua godoro , mashuka na neti achana kitanda kwanza
Weka stock ya Chakula na gesi ya miez miwili au mitatu
Usiwe na papala tunza pesa ktk hiko kpnd cha miez mitatu .

Mwezi ujao kawakatie bima ya afya wazazi wako na wewe pia .

Baada ya hapo sasa unatakiwa ujali mda, pesa uiheshimu , kama mnywaji na mvutaj acha .

Weka urafiki na majilani . jitahdi kuwa mshauli na msuluishi maana itakujengea nafasi ya kupata msaada utakapo teleza

Weka malengo ya kupanga mda mfupi , ujibane ukajenge utakuwa huru zaid na mfano wa kuigwa

Kuna mengi nimeacha lakini unatakiwa ujibane avoid magrupu lelemama
asante
 
Habari ya Jumapili wadau,

Mimi kijana wa miaka 25 ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea kuna kazi naifanya ambayo kwa mwenzi huwa inaniingizia kipato cha laki tatu(300000). Sasa nilikuwa nahitaji mpangilio mzuri wa matumizi wa haka kamshahara kangu ili nipate kubaki na akiba hata wazazi siku wakihitaji msaada wa kifedha nipate kuwasaidia.

Naombeni ushauri wenu mlionitangulia katika maisha ya kujitegemea.
Ngoja nitoe ushauri kwa mtizamo wangu. Binafsi naamini kuwa kipato chochote kile mtu anaweza kufanya jitihada na kufika pale anapotaka kufika.
Unapokuwa na kipato chochote kile iwe kikubwa au kidogo ni vyema ukikitumia kwa mgawanyo wa asilimia.
Kuna makundi tofauti kwenye matumizi ya pesa baadhi yake ni:-
1. Matumizi ya kawaida, hapa najumuisha chakula, nauli, vocha, kuhonga, umeme, maji na kadhalika. Kwa kipato chako unaweza ukaelekeza 60% ambayo ni 180,000
2. Matumizi ya ununuzi wa mali binafsi kama kiwanja, gari, simu, furniture na kadhalika. Unaweza ukaelekeza 15% ambayo ni 60,000. Unakuwa unakusanya taratibu taratibu unanunua assets taratibu taratibu.
3. Matumizi ya uwekezaji, hapa ni kama unaanzisha biashara, au unanunua hisa za makampun ili kipato chako kizalishe mara dufu na kadhalika. Unaweza pia ukaelekeza 15% unakusanya huku unafikiria biashara ambayo unaweza ukawekeza.
4. Mfuko wa dharula, hii ni kwaajili ya mambo ambayo haukutarajia kama kuibiwa vitu vya muhim kama simu, matatizo mengne mengine na kadhalika. Unaweza ukaelekeza 10% ambayo ni elfu 30, hii hela hakikisha hauigusi iache ikue hivyo hivyo taratibu ni kwaajil ya dharula tu.
Wakati huo unapambana kuhakikisha unaongeza kipato chako, usiridhike na kipato cha 300,000. Jitahidi kuwa mbahiri kadri uwezavyo zaidi ya mchaga, tupo tulioanza kwa kipato cha 150,000 kwa mwezi na tukaweza.
Kipato kikikua unaweza ukaadjust asilimia zako na ukaongeza fungu lingine ambalo ni matumizi ya starehe na kujifurahisha unayoweza kuiwekea hata asilimia 5% ila kwasasa si vyema ukawa ni hicho kipengele.
 
shukran sana
 
Japo kuwa ujasema kama umepangisha ama hujapangisha ,
Lakini pia kama huna fenicha za Ndani isiwe ishu
Nakuambia tuu kwa utashi wangu
Anza kununua godoro , mashuka na neti achana kitanda kwanza
Weka stock ya Chakula na gesi ya miez miwili au mitatu
Usiwe na papala tunza pesa ktk hiko kpnd cha miez mitatu .

Mwezi ujao kawakatie bima ya afya wazazi wako na wewe pia .

Baada ya hapo sasa unatakiwa ujali mda, pesa uiheshimu , kama mnywaji na mvutaj acha .

Weka urafiki na majilani . jitahdi kuwa mshauli na msuluishi maana itakujengea nafasi ya kupata msaada utakapo teleza

Weka malengo ya kupanga mda mfupi , ujibane ukajenge utakuwa huru zaid na mfano wa kuigwa

Kuna mengi nimeacha lakini unatakiwa ujibane avoid magrupu lelemama
Mkuu bima gani anaweza kata na bei gani ebu saidia hapo
 
Dah hongera mkuu kwa kutaka kupata ushauri maana watu wengi kwenye elimu ya financial management hawana, cha kukushauri zaidi acha kupenda mambo ya anasa ishi kwenye budget line uliyojiwekea
 
Back
Top Bottom