Ushauri: Nahitaji kuanza ujenzi

Ushauri: Nahitaji kuanza ujenzi

linkedIn

Senior Member
Joined
Dec 20, 2014
Posts
151
Reaction score
55
Habari wanajamvi,

Nina imani humu kuna watu wenye fani mbalimbali na wenye uzoefu wa mambo tofautitofauti. Naomba mawazo yenu wakuu.

Ninahitaji kuanza kaujenzi ifikapo mwakani, niandae kiasi gani cha fedha kukamilisha boma peke yake lenye jumla la vyumba vinne, sebule, jiko na dining.

Karibuni!
 
Nakuja si muda , halaf nkija nataka pia kujua uko mkoa gani na site yako ikoje!! Tambarare au panda shuka
 
Hongera sana! Ili uweze kujenga nyumba bora Ni lazima uwe na mchoro ambao utakusaidia kufanya mipango katika ujenzi wako,ukishakuwa na mchoro Ni rahisi kukadiria kiasi cha material na gharama za ujenzi katika hatua mbali mbali kama msingi,kuta,kupaua na kuezeka pa1 na finishes,kwa maelezo zaidi niPM
 
Inategemeana na mkoa mkuu coz material, mafundi vinatofautiana
 
1.Msingi=3m
2.matofari (block)2000=2m
3.cement=1m
4.posho vibarua&fundi=3m
5.maji=5l
6.others=1m.
Jumla=10.5m
huo niujenzi wa boma tu bila paa,
ni makadirio na ujenzi usiwe na mbwembwe nyingi
 
*Unajenga wapi/mkoa gani?

*Una kiwanja, kipo katika hali gani? Kipo kwenye mwinuko au flat? Ardhi ya eneo hilo ikoje? Ni udongo wa aina gani?

*Je, vifaa vya ujenzi katika eneo hilo vinauzwa bei gani? ie. Mchanga, tofali, kokoto, maji, cement, vifusi, mbao.

*Ufundi katika eneo hilo unagharimu kiasi gani? Umekutana na mafundi wangapi kusikiliza bei zao, umehakiki baadhi ya kazi zao?

*Una mchoro, umechorewa na wataalamu, wamefika kuangalia jinsi eneo lilivyo? Au umenunua mchoro blindly?

Maoni: Kama una mchoro, tafuta fundi, elewana nae bei ya ufundi, then yeye ndio atakupa makadirio ya tofali, mchanga, mbao, maji, nk kutokana na ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga.
 
Makadirio ya gharama ya paa yakoje?Bati za aluminium

Je msingi wa boma kama hilo unahitaji nondo?
 
*Unajenga wapi/mkoa gani?

*Una kiwanja, kipo katika hali gani? Kipo kwenye mwinuko au flat? Ardhi ya eneo hilo ikoje? Ni udongo wa aina gani?

*Je, vifaa vya ujenzi katika eneo hilo vinauzwa bei gani? ie. Mchanga, tofali, kokoto, maji, cement, vifusi, mbao.

*Ufundi katika eneo hilo unagharimu kiasi gani? Umekutana na mafundi wangapi kusikiliza bei zao, umehakiki baadhi ya kazi zao?

*Una mchoro, umechorewa na wataalamu, wamefika kuangalia jinsi eneo lilivyo? Au umenunua mchoro blindly?

Maoni: Kama una mchoro, tafuta fundi, elewana nae bei ya ufundi, then yeye ndio atakupa makadirio ya tofali, mchanga, mbao, maji, nk kutokana na ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga.
ww umeongea vzur sanaa
 
Back
Top Bottom