Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Habari zenu wanajukwaa,

Msaada nina mtaji wa laki tano naomba ushauri ninaweza kufunguaa duka La rejareja. Kama uuzaji wa unga, sukari, maharage, na bidhaa zingine? na vipi kuhusu faida huwa ikoje? Msaada tafadhali.

Mbarikiwe.
 
Habari wandugu.

Naomba uzoefu wa kuendesha duka la kawaida. Linalouza bidhaa za majumbani kama chakula na vinywaji.
 
Mtaji kwanza, eneo gani (mjini ama kijijini au kwenye mji ulio na watu wengi). Chumba cha duka unalipia ama umejenga?
 
Inategemea unauza nini. All in all mil 2 inatosha lakini faida yake haiwezi kuzidi 20% kwa mwezi kwa kuwa faida kwa bidhaa sio kubwa kama unavyodhani. Kuna jamaa anamtaji wa milioni 5 anaweza kwa mwezi kukunja faida ya mil 1 na ni mbinde hasa ujue.
 
Nimefungua biashara ya duka lakini baada ya muda nimejikuta niko katikati ya maduka mengi.

Naombeni ushauri namna ya kutokata tamaa na kusonga mbele. Pia namna ya kuiboresha.
 
Mteja awe mfalme, usikubali kupoteza mteja, huduma ziwe first class ili mteja arudi kwako na asiende kwingine.
 
Karibisha wateja, usitake faida kubwa sana (nyongeza) au kupunguza bei iwapo mteja akikuomba sana. Kama ni mtaani hakikisha vitoto vikija kununua au housegirl/boy hakikisha unaanda vipipi n.k.
 
1. Bidhaa zenye ubora
2. Lugha nzuri
3. Ofa kwa wateja
4. Kufungua biashara mapema Na kuchelewa kufunga
5. Mtangulize MUNGU
6. Hakikisha mteja hakosi bidhaa mfano Sina chenchi, sina bidhaa Fulani hupoteza wateja. Badala yake komaa kutafuta chenchi pia kama bidhaa fulani huna mwambie imeisha ila inakuja muda c mrefu itakuwepo.
 
1.Bidhaa zenye ubora
2.Lugha nzuri
3.Ofa kwa wateja
4.Kufungua biashara mapema Na kuchelewa kufunga
5.Mtangulize MUNGU
6. Hakikisha mteja hakosi bidhaa mfano Sina chenchi, sina bidhaa Fulani hupoteza wateja. Badala yake komaa kutafuta chenchi pia kama bidhaa Fulani huna mwambie imeisha ila inakuja muda c mrefu itakuwepo
Mzee wa fitin nakushukuru sana kwa ushauri nitaufanyia kazi haraka!!!!!!!!!
 
Habari wakuu:

Naomba ushauri kwa watu wazoefu au wenye uelewa kuusubiashara ya duka la rejareja la vyakula na vitu vya nyumbani kawaida.

Kwa mtaji wa mil 2. Ningependa kusaidiwa katika mambo yafuatayo;

1. Ni vitu gani vya kuzingatia sana wakati wa kutafuta mahali (location)
2. Tofauti na location kuna vitu gani vingine vya kuzingatia?
3. Je, kuna changanoto zozote katika upande wa usalama (wiz)
4. Ni vitu gani vinaweza kupelekea hasara kwenye biashara hii
5. kwa Dar es salaam naweza kufanyia biashara hii wapi labda?
6 Biashara gani nyingine mbadala naweza kuifanya kwa pesa izo?

Thanks in advance
 
Duka hilo unaweka mfanyakazi au unauza mwenyewe?
Umewah kufanya hiyo biashara au ndo unaanza?
Changamoto yake kubwa ni kuwa faida ya hiyo biashara imebase kwenye hela ndogondogo unaweza kuta faida kwa kitu ni sh 50,100,200 hivo usipokuwa makini badala ya kuendelea unaweza pata hasara
 
  • Hakikisha unanunua bidhaa kidogokidogo kwa kwa kila item.
  • Weka bidhaa ambazo hazitakusumbua sana kuuza kwa eneo lako, mfano. Juice, Maji, Unga, mafuta Kula, sabuni etc, bidhaa ambazo ni mahitaji ya lazima.
  • Weka vocha kwa huvutia wateja. Biashara hii inalipa sana kama utajituma na kuwa na nidhamu ya matumizi.
  • Bidhaa inayo uliziwa Sana na dukani haipo hakikisha unaandika Kisha uininue.
  • Survey maduka ya jirani Kujua bei na baadhi ya bidhaa ambazo hawana we uziweke japo kidogo.
 
Pia ukumbuke kuangalia expire date mana kuna bidhaa hazikai muda mrefu bila kuharibika hivo unatakiwa ujue zinatokaje kama zinatoka taratibu unaweza kununua kiasi tu.Mfano badala ya kununua box zima unanunua nusu au robo yake na uzuri ni kuwa kuna maduka yanaweza kukuuzia kwa stail hiyo.
 
Back
Top Bottom