Mwaka huu Chama chetu kikongwe kinaenda kufanya chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi mpaka taifa. Ni matarajio yangu wanachama wetu kwa ngazi zote watajitokeza kuomba ridhaa ya kuongoza Chama kwenye kipindi hiki chenye kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu". Hivyo ni matumaini yangu wagombea wote watakuwa na mtazamo na muelekeo wetu wa kuiifikia Tanzania mpya ya Viwanda.
Kilichonigusa mpaka kupandika uzi huu ni pamoja na mambo yanayoendelea sasa. Nakumbuka wiki mbili zilizopita pale Dodoma, ulituahakikishia wana CCM kuwa nafasi ziko nyingi tu. Ila ni rai yangu huyu kijana wetu mpendwa Paul Makonda naomba umludishe chamani tafadhali Mwenyekiti.
Kutokana na misuguano ya kimtazamo iliyopo kati ya wadau mbalimbali juu ya mpendwa wetu huyu. Kwasasa sioni kama atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watumishi anaowaongoza pamoja na wadau wa jiji la DSM. Najua Mwenyekiti wewe ndio unamtaka nani ufanyenae kazi na nani umtaki, wewe unajua nani akae wapi na nani asikae. Ila kwa hili mimi natoa kwa ajili tu ya afya kwa jiji letu la DSM.
Mwenyekiti, Paul Makonda amekuzwa ndani ya CCM kimkakati zaidi, rejea jumuiya ya vijana UVCCM. Katika jumuiya hii kijana huyu alikuwa ni kijana wa kupanga mikakati mingi iliyosaidia kuinua hali ya Chama kwa vijana hasa kupitia vyuo vikuu. Kijana huyu alikuwa mstari wa mbele kabisa kupambana kwa wale aliwaita vibaraka wa ufisadi - Mgeja na mwenzake ambao bado kesi yao inaunguruma mahakamani, pia alidiliki kumsema mgombea wa UKAWA wakati akiwa CCM waziwazi. Hivyo kwangu ni mtu ambae anakijua Chama na kama unavyosema mwenyewe kuwa ni mchapa kazi hodari. Pia alisaidia kuzima mijadala mbalimbali ambayo kwa namna moja ikasaidia mapendekezo ya Katiba mpya yabaki na Jamhuri na SMZ.
Hivyo nafikiri kijana huyu ukimludisha chamani bado ataendelea kukufaa zaidi kulivyo alipokuwa sasa kwani nafasi aliyopo imeshaingia shubiri. Huku chamani sisi hatuna shida na Elimu kwani tunachoangalia sisi ni chama kwanza mtu baadae. Mifano huku chamani ipo, rejea Bulembo na Msukuma hawa ni viongozi wetu wa chama lakini wamepewa nafasi bila ya kujali Elimu yao.
Mwenyekiti, kwasababu mpendwa wetu Paul Makonda bado unamuhitaji ni vyema ukamludisha chamani. Nafasi ya Katibu Mwenezi wa Chama chetu ingemfaa sana mpendwa wetu huyu. Kwangu nafasi hii imepwaya sana baada ya kutoka Nape. Paul Makonda kama nilivyosema awali ni kijana wa mikakati ambayo mingine umeshuhudia wewe mwenyewe, kwani Katibu Mwenezi wa sasa bado chamani hakubaliki (mtazamo), kwanza kwa msimamo wake wa Serikali Tatu na pia huyu mtu ni mgeni chamani.
Mwenyekiti nikirejea kwa Komredi Nape, yeye nadhani umeona utendaji wake akimsaidia Katibu Kinana. Yeye amethubutu kuisema Serikali iliyopita na watendaji hadharani kwa kuiona kuwa kuna watu mizigo wakiwemo Mawaziri. Huyu nae amezunguka Tanzania nzima kufufua uhai wa Chama. Amefika kila pembe ya nchi yetu kuona wanachama na kuongea nao, pia walisaidia kutoa maelekezo ya chama kwa viongozi wa Serikali.
Vilevile kumbuka Mwenyekiti, Nape ni mmoja kati ya mtu aliyezuia mafuriko kwa mikono, pia alisema waziwazi kuwa mtu asiyefuata utaratibu wa chama watamkata. Pia sina shaka kama utampatia Ukatibu Mkuu wa Chama atakusaidia sana kwani nae ni mmoja wa watu wanao kijua chama. Mtu huyu pia ni mpambanaji hasa rejea harakati za Uchaguzi 2015.
Mwisho, Mwenyekiti naomba tuanze sasakujenga chama kwa kuanza na sisi mikutano yetu ya ndani kwa wanachama wetu kwani vidonda ni vingi, tukikaa sana bila ya kuviponya vitaoza.
Pia rejea hotuba ya Mwenyekiti aliyepita, kuwa tusijisahau sana kuna mtu upande wa pili anajipanga usiku na mchana, tusijekushtuka kumekucha.
Wasalaam
Methadone.