MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Bara Mzee Stephen Wassira amemuonya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif kuacha kubeba wagombea wa nafasi za Ubunge wasiokubalika na wananchi kwani msimamo wa Chama kwa sasa ni kuteua wagombea wanaokubalika kwa wananchi.
Akizungumza leo Februari 10, 2025 mjini Lamadi, Busega Simiyu, Mzee Wasira amesisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kitasimamia kiwe chama cha haki na kwamba chama hakitavumilia dhuluma za aina yoyote kwenye mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama na kusisitiza kuwa chama hicho hakitaki vitisho na kinataka wanachama wake waseme mawazo yao waziwazi.
"tunataka chama chetu kilinde haki za watu, chama chetu hakitavumilia dhuluma kwa sababu tumeandika na kuapa katika Katiba kwamba tutaondoa dhuluma, chama chetu hakitaki vitisho chama chetu kinataka watu waseme Mawazo yao wazi wazi" amesema Wasira
Pia Wassira amemuonya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu kuacha siasa za vitisho kwa wanachama wake kwani mambo hayo yamekataliwa kwenye Katiba ya CCM
"Tunataka ninyi wananchi kupitia vikao mtuambie sifa moja tunayotaka nani anakubalika katika jimbo anakubalika na wananchi na hili namwambia mdogo wangu Mwenyekiti wa MKOA (Shemsha Mohamed Seif) kwamba hakuna kusema huyu ni mwenzetu wote ni wenzetu tena wenzetu ni wale wanaokubalika kwa wananchi hapo ndiye wenzetu mwenzetu ambaye hakubaliki tutabaki naye tunamuombea kwa Mungu siku moja akubalike" ameonya Mzee Wasira huku akishangiliwa na mamia ya wanachama wa CCM waliofika kumlaki eneo la Busega.
Mzee Wasira akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif