Ushauri: Mwanamke tajiri anataka niache chuo tufanye biashara

Msigwa Amos C

Member
Nov 1, 2015
38
22
Habari wana JF,

Mimi ni kijana wa miaka 25 nipo chuo mwaka wa pili, lakini maendeleo ya chuo yameanza kufifia baada ya kukutana na mwanamke tajiri na mwenye umri mdogo miaka 23 huyu dada nilikutana nae kwenye dalala nikamtongoza akanikubali na kunielewa kadili siku zilivozidi kusonga upendo wake kwangu ukaongezeka mara dufu.

Sasa yeye ameishia kidato cha nne hakufanikiwa kuendelea na shule lakini baba yake akamuchia nusu ya utajiri wake, kipindi hicho chote mimi sikujua kama nimepta Bosslady. Jana akawaananiambia ukweli wa haya yote, nami nikamwambia nipo chuo, akaniuliza nasomea nini?

Nikamjibu nasomea education, akaniuliza masomo gani nikamjibu arts subjects, akakata tamaa ghafla na kuniambia mbona nahangaika na masomo yasiyo na ajira na yananichelewesha maisha, nilijikuta navunjika moyo ghafla nikifikilia kweli ajira ni shida.

Kibaya zaidi akanishauri niache chuo tufanye biashara kwa kutumia pesa zake, pia issue ya chuo anaona mimi nitaibiwa na wanawake wengine kwahiyo niachane na chuo tujikite kwenye biashara zaidi nikamwambia ngoja nifikilie nitakujibu.

Naombeni ushauri niache chuo manake hata ada yenyewe naungaunga tu au niendelee kukomaa na chuo?
 
Habari wana JF

Mimi ni kijana wa miaka 25 nipo chuo mwaka wa pili, lakini maendeleo ya chuo yameanza kufifia baada ya kukutana na mwanamke tajiri na mwenye umri Mdogo miaka 23...huyu dada nilikutana nae kwenye dalala nikamtongoza akanikubali na kunielewa kadili siku zilivozid kusonga upendo wake kwangu ukaongezeka mara dufu. Sasa yeye ameishia kidato cha nne hakufanikiwa kuendelea na shule lakin babake akamuchia nusu ya utajir wake, kipindi hicho chote mie sikujua kama nimepta bosslady. Jana akawaananiambia ukweli wa haya yote, nami nikamwambia nipo chuo, akaniuliza nasomea nn? Nakamjibu nasomea education, akaniuliza masomo gani nikamjibu arts subjects, akakata tamaa ghafla na kuniambia mbona nahangaika na masomo yasiyo na ajira na yananichelewesha maisha..,nilijikuta navunjika moyo ghafla nikifikilia kwel ajira ni shida....kibaya zaid akanishauri niache chuo tufanye biashara kwa kutumia Pesa zake, pia issue ya chuo anaona Mimi nitaibiwa na wanawake wengine kwahiyo niachane na chuo tujikite kwenye biashara zaidi....nikamwambia ngoja nifikilie nitakujibu.


Naombeni ushauri niache chuo manake hata ada yenyewe naungaunga tu au niendelee kukomaa na chuo?
Endelea na chuo.
 
Mario kwenye ubora wako.

Mwanamke tajiri unakutana nae kwenye daladala halafu ukiwa muongo uwe unaweka sawa fact zako eti miaka 23 kaachiwa urithi na baba yake na anakushawishi wewe wa chuo uache mkatumbue pesa zake kwa kirungu gani ulichonacho oohoooo kijana be careful
 
We jamaa usitafut kuchizija mapema,,, yani mwanamke unatak akakutunze, ety uache chuo mkafany biashara, mtaji wenyew wa mwanamke tena bdo mdgo miak 23 msichan mwenyew, unaisi anajielewa huyo?? tafakar vizur zen uchukue hatua usije kuua wazazi wako kwa presha…!!

Halafu ukiangalia mwakn unamaliza kwann km anakupenda kwel asisubir umalizie huo mwaka zen nd mkafany hizo biashara??
 
Somaa wee!then ajira utaipata 2019-20!nakushauri usipishane Na helaa!mute chuo kapige hela!wtu wana elimu Na bado bu10 inawaza shida
 
Oya chuo chenyewe kinachosha elimu ipo ilimradi unavyeti vyako we jiongeze mkuu

Kaa kwa uyo demu kimaslah zaid ata akikupiga chini ujue umeondoka na kitu saa wee endekeza papuchi tuu

Alafu hawo wanao kwambia endelea na chuo wao wamegundua nn tangia waanze kusoma mpk sasa acha fikra mgando katafute life mbaba
 
Watu tumesoma miaka kumi na saba yaaan miaka yote iyo unasoma tuu hujui changamoto za maisha alafu ukitoka apo utafute kazi miaka 3

So miaka 20 wee unasoma tuu na kama umeandikiwa kufa na miaka 40 means nusu ya miaka yako umetumia ktk elimu

F@&kn elimu tena namshukuru mungu me mchaga najua kutafuta pesa bila ivyo ningekuwa sina ata kijiko changu mpk sasa
 
Ghafla Tu Baba Na Bado Yupo Hai Anaamua Agawanye Utajiri Wake Nusu Ampatie Binti Yake Aliye Hitimu Kidato Cha Nne Kibongo Bongo Hata Ulaya Hili Linawezekana Kweli Na Kama Ni Inawezekana Huyo Mzee Kwajinsi Anavyo Mjali Mwanae Akisikia Upo Na Binti Yake Atakulipua Nakushauri Endelea Kuota Ndoto Nyingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom