Ushauri: Mpenzi wangu yuko hati hati kuachishwa kazi

Feb 7, 2017
11
26
Habari zenu,

Mpenzi wangu yuko hati hati kupunguzwa kazi kwenye hotel kubwa jina kapuni, toka jana sina raha aliponiambia na tuko kwenye maandalizi ya kufunga ndoa hapa tulipo tumeshauriana hiyo hela atakayopewa aende akosomee udereva ili aweze kubadilisha kazi. Yani sina raha kabisa nawaza na je naweza kuhusu vikao vya harusi mana mpaka sasa tushakwama

Nimeleta hii mada ili muweze kunifariji na kunipa ushauri.
 
je unampenda yeye mwenyewe au unapenda kazi yake?. Najua wadada wengi wanapenda security kwenye maisha ya ndoa na maisha yenye uhakika. Huo ni mtihani ukabili mweke Mungu mbele na usirudi nyuma. Vipi kama angepunguzwa kazi mwezi mmoja baada ya ndoa ungefanyaje?
 
Pole. Kwa kipindi hiki hata mkifunga harusi ya elfu hamsini kila mtu atawasifu maana uchumi umeyumba kwa kila mtu... So kifo cha wengi ni harusi... Wala usipate presha kuhusu arusi.
Ukikwama kabisa njoo na namba ya mpesa, wana JF ni wat wazuri, wakikuchangia hata elfu tano au kumi harusi itasonga. Kila la kheri mwana JF mwenzetu...
 
Kwa hakika kwa sasa wewe ndiyo ulitakiwa uonekane ni sapoti ya mpenzi wako katika hii hali. Kama sapoti yake sasa hivi upo humu ukisema hauna raha unataka kusema utakua unalia mbele yake kila mkiwa wote?

Unadhani utakua unamsaidia?

Huu uzi ilibidi aje nao mhusika akionesha anavyohofia jinsi gani ataweza kuleta mkate mezani, lakini umekuja nao wewe nathubutu kusema mhusika atakua na kazi kubwa ya kukufariji wewe kushinda wewe kumfariji yeye.

Pia haujasema kama na wewe hauna shughuli ya kukuingizia kipato ili umpe msaada jamaa kwa kipindi hiki...
 
Pole sana mkuu! Hayo ni mapito tu, kama yeye ndo mwenye kazi pekee kwenye huo uhusiano nakushauri msitishe mipango ya ndoa ili akasome hiyo kozi, na wewe anza kujishughulisha. Akimaliza kozi yake na kupata kazi endeleeni na mipango yenu.
Kaa nae karibu umfariji, mwambie mambo yatakua sawa.
 
Kwa hakika kwa sasa wewe ndiyo ulitakiwa uonekane ni sapoti ya mpenzi wako katika hii hali. Kama sapoti yake sasa hivi upo humu ukisema hauna raha unataka kusema utakua unalia mbele yake kila mkiwa wote?

Unadhani utakua unamsaidia?

Huu uzi ilibidi aje nao mhusika akionesha anavyohofia jinsi gani ataweza kuleta mkate mezani, lakini umekuja nao wewe nathubutu kusema mhusika atakua na kazi kubwa ya kukufariji wewe kushinda wewe kumfariji yeye.

Pia haujasema kama na wewe hauna shughuli ya kukuingizia kipato ili umpe msaada jamaa kwa kipindi hiki...
anachokitaka mi nakijua ila lazima asonge mbele na ndoa yake
 
hapo ndiyo mapenzi uyaongeze , kama anaakili ni mume mzuri tu kama unakazi wewe jiandae kisaikolojia kumuhudumia .... sasa ndiyo maana ya ndoa inaanza .. kamamtaweza kupunguza bajeti ya harusi mkaziweka saving itakuwa heri
jamaa alikuwa na kazi kweli? tuanzie hapo maana mjini hapa ni shida tupu
 
hizo ni changamoto za maisha kama unampenda kiukweli huu ndio mtihani wako wa kwanza na uta stick nae together
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Usije tu ukamwacha mwenzio kisa kua kuachishwa kazi...

Hapa ndo uanamke wako kwa mwenzi wako unapotakuwa kuonekana.
Kua nae bega kwabega kumtia moyo kwa kumhakikishia mapito hayo lazima yatokee ili kuvuka hapo mlipo na kwenda hatua nyingine ya kimafanikio zaidi...

Usitoe nafasi mumeo mtarajiwa asononeke kipindi hiki cha mpito. Muombe,mshauri na kumtia moyo apate nguvu mpya kufurahia maisha no matter what....
 
Habari zenu,

Mpenzi wangu yuko hati hati kupunguzwa kazi kwenye hotel kubwa jina kapuni toka jana sina raha toka aliponiambia na tuko kwenye maandalizi ya kufunga ndoa hapa tulipo tumeshauliana hiyo ela atakayopewa aende akosomee udereva ili aweze kubadilisha kazi... yani sina raha kabisa nawaza na je nawaza kuhusu vikao vya harusi mana mpaka sasa tushakwama

nimeleta hii mada ili muweze kunifariji na kunipa ushauri
hapa kwetu wamepunguzwa watu 24 jana dah inaniuma sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Usije tu ukamwacha mwenzio kisa kua kuachishwa kazi...

Hapa ndo uanamke wako kwa mwenzi wako unapotakuwa kuonekana.
Kua nae bega kwabega kumtia moyo kwa kumhakikishia mapito hayo lazima yatokee ili kuvuka hapo mlipo na kwenda hatua nyingine ya kimafanikio zaidi...

Usitoe nafasi mumeo mtarajiwa asononeke kipindi hiki cha mpito. Muombe,mshauri na kumtia moyo apate nguvu mpya kufurahia maisha no matter what....
Asante Dada kwa ushauri, na kwa kunifariji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom