Ushauri: Mke wangu kaniambia mtoto wa kwanza sio wangu na baba yake anamuhitaji

dmorigo

JF-Expert Member
Jan 9, 2018
238
136
Kama kichwa cha habari kilivyo,

Wadau nimekwama kutoa maamuzi juu ya hili suala nabaki kuangalia tu siku ya tatu leo. Wakati naripoti halmashauri baada ya ajira mwaka 2015 Kigoma nilikutana na msichana miongoni mwa walimu tuliofika.

Yeye ni mwalimu wa degree kasomea SAUT na mimi ni diploma nimesomea SHYCOM, tulijikuta tunaanzisha mahusiano ya kimapenzi na bahati nzuri tulipangwa kituo kimoja tukaamua kuishi pamoja kama mke na mume na ndivyo jamii inatambua mpaka sasa.

Likizo ya mwezi wa 12 mwaka huo huo 2015 tulitawanyika kila mmoja akaenda nyumbani kwao, mimi Mwanza yeye Tabora na baada ya likizo tulikubaliana kupitiana ili turudi pamoja kituoni, hivyo alitoka Tabora akaja Mwanza tukarudi wote Kigoma na maisha yakaendelea.

Mwezi wa pili mwaka 2016 tuligundua kuwa kapata ujauzito, tulifurahi sana sote na hasa mimi maana nlitamani kuwa na mtoto alijifungua salama mtoto wa kiume.

Tatizo tangu mwanzo wa mahusiano yetu amekuwa akichart na kuwasiliana sana na baadhi ya wanaume, nikimuuliza anadai walisoma naye chuoni miongoni mwao kumekuwa na wanaume wawili common kama wasipopiga simu basi watatuma SMS na baadhi nimekuwa nazikamata na namuonya nasamehe maisha yanaendelea.

Mwezi wa saba mwaka jana nilisafiri nikamuacha nyumbani mwenyewe na mtoto nakumbuka nilimpigia simu hakupatikana tangu asubuhi kufika jioni nikamtuma jirani yetu aniangalizie kama hawajambo hapo kwangu alinijibu kuwa mke wangu aliondoka tangu saa tatu kuelekea mjini na hajarudi mpaka muda huo.

Mpaka usiku hakurudi na alirudi saa sita mchana wa siku iliyofuata na hapo ndio alipatikana hewani. Nilipomuuliza alikuwa wapi na alilala wapi alikataa kuwa hakutoka na simu haikuwa na charge.

Kwa kuwa sikuwa na ushahidi nikapotezea na maisha yakaendelea. Mtoto wa kwanza tayari ni mkubwa na ana mimba kubwa ya miezi saba. Sasa hili la juzi ndio limenifanya niombe ushauri humu.

Alipigiwa simu miongoni mwa namba zile mbili, akasita kuipokea ila baada ya kupiga tena akapokea mazungumzo yaliashiria kuna mipango wanapanga juu ya mtoto fulani, uzalendo ukanishinda baada ya simu kukatwa nikawa mbogo.

Nikaomba kujua kinachoendelea, alijaribu kuficha lakini baada ya makofi mawili akafunguka kuwa mtoto wa kwanza sio wangu na baba yake anamuhitaji ambae ndio huyo wanayewasiliana.

Nilihisi kuishiwa nguvu maana siku zote najua na naamini mtoto ni wangu tangu anazaliwa mpaka sasa ana miaka miwili. Namuuliza ilikuwaje mpaka mtoto akawa sio wangu naambiwa likizo ile ya kwanza alikaa kwao wiki moja na wiki tatu zote alikuwa mwanza SAUT kwa huyo mwanaume.

Mpaka anakuja kunipitia najua anatokea kwao Tabora kumbe alikuwa Mwanza humohumo, hapo ndipo mimba ilipatikana na alimjulisha kuhusu hiyo mimba na amekuwa akifatilia maendeleo ya mtoto mpaka sasa anamtaka mtoto wake.

Siku ile alipolala nje na kurudi saa sita za mchana kutopatikana siku nzima kumbe mwanaume yule alikuja kumsalimia na kumuona mtoto na walikuwa wote mjini.

Naumia nimeshindwa nifanye nini mpaka imefikia hatua najisikia hasira juu ya mtoto kila akiniita na akinisogelea karibu.

Mke wangu ndio sitaki kabisa kumtazama najiskia kummeza nina hofu pia na hii mimba ya mtoto wa pili pengine naye siyo wangu nimeshindwa niamue nini.

Naombeni ushauri
 
Ehhh Mungu nakuomba kwa huruma yako umfanye mwanadamu huy awe na maamuzi ya busara na siyo kesho tukute habar ingine magazetini

Omba uhamisho wa kituo cha kazi ,,

Achana nae maana kama ameweza danganya miaka 2 na anamimba ingine si rahis kuamini hata hyo,,

Na Mungu anakupenda sana mana kakuonyesha mapema kabisa kuliko ungefunga nae ndoa
 
Aisee pole sana mkuu ...daah wanawake kuna mda mwingine hatujui hata nini tunataka yaan kaolewa n bado hajarizika had kuzaa nje mmmh... Kuwa na subira katika kufanya maamuzi usje jikuta unagawana nae majengo ya serikali,mmja mochwari mwingine jela... Mungu akutangulie kwenye maamuzi utakayochukua yawe yenye busara zaidi...pole aisee
 
Ehhh Mungu nakuomba kwa huruma yako umfanye mwanadamu huy awe na maamuzi ya busara na siyo kesho tukute habar ingine magazetini

Omba uhamisho wa kituo cha kazi ,,

Achana nae maana kama ameweza danganya miaka 2 na anamimba ingine si rahis kuamini hata hyo,,

Na Mungu anakupenda sana mana kakuonyesha mapema kabisa kuliko ungefunga nae ndoa
Yaan vikombe vingine ni vigumu kuvinywea kwakweli...Mungu atuepushe na balaa kama hizi
 
Ehhh Mungu nakuomba kwa huruma yako umfanye mwanadamu huy awe na maamuzi ya busara na siyo kesho tukute habar ingine magazetini

Omba uhamisho wa kituo cha kazi ,,

Achana nae maana kama ameweza danganya miaka 2 na anamimba ingine si rahis kuamini hata hyo,,

Na Mungu anakupenda sana mana kakuonyesha mapema kabisa kuliko ungefunga nae ndoa
Asante kwa ushauri wako
 
Ebu tulia kwanza ...usikulupuke hapo unabid ucheze kama Pele ... maana yake usije ukakuta.... uyo mtoto ni wakwako ila yeye mke wako ndo ajafahamu ...sasa unabid umchunguze vizur mtoto ...kama ni wako au la unaweza ...kuangalia vidole ...au kichwa au pua au miguu au maskio au macho ...yaani kama ni mtoto wako unaweza kumgundua Vizuri...then kitu kingine... usijiue maana nyie walimu mlivyokuwaga wajinga unaweza ukabwiga sumu hivi hivi....tulia tu ...hii dunia sote tunapita ...maana wewe sio wakwanza kufikwa natatizo kama hilo ...wapo wengi ...waliokulipata na wengine wakafa wakaenda....so tuliza akil .. hiyo mindset... yako unabid uichezeshe vizur .
 
Aiseee
Mwache aendee.
Utakufa kwa pressure wakati sio wako.
Muda bado unao wa kulitafuta penzi LA dhati...
Swala LA msingi hama kituo mapema iwezekanavyo...
Mwachie kila kitu usije ukapata chochote cha kukufanya umkumbuke...

Kaa ukielewa kua yupo mwaminifu alie wekwa na mungu kwa ajili yako na siku zote
Kisicho ridhiki hakiliki
Kila LA kheriii
 
Sheria yangu siku zote kuwa mpenzi anayekudanganya mwezi mzima apo akuna mapenzi.... Kwa Mwanamke anayekupenda kwa dhati kabisa akunaga siri anakuwa Na ofu ya kukupoteza siku ukijua....Usilazimishe mwambie tu kutokana Na sababu pendwa uaminifu aupo so kila Mmoja ajue njia Yake kwa amani kabisa bila kuadisia watu Na yoyote Mwenye kuuliza unamwambia tumetengana for good
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom