Ushauri: Mke wangu anatembea na mfanyakazi mwenzie hadi kamzalisha

We jamaa kuna sehemu unakopi hivi visa au? Maana kwa siku moja unaomba ushauri kama demu mara mwanaume, mara mjane mara kahaba mara mtawa.
 
Kwa hiyo SMS ina maana huyo Jamaa anasema wewe ni BOYA?Any way.Kwanza Mshukuru sana Mungu kwa kupata hiyo habari ili kwa upande wa ushauri.Nakushauri Utulie kwanza ili ufanye uamuzi wa busara maana kwa kweli hiyo hali ni TATA sana.

ILA TRUST me.Ww sio BOYA.Boya ni huyo Jamaa aliyekuita BOYA.Ukitulia Kabisa bila kufanya Jambo lolote kwa sasa Mpaka mtoto azaliwe utaelewa UBOYA wa Huyo Jamaa.Kwa sasa hivi Tulia kabisa na hiyo line hakikisha inakuwa hewani wakati wote ila usiipigie,usijibu meseji wala usifanye Jambo lolote la kuonesha kwamba umetambua kinachoendelea.

Fanya Utafiti tu wa kujua iwapo wanao ni Damu yako na iwapo Jamaa ana Familia basi tafuta data za msingi za familia yake kimya kimya ila Usifanye maamuzi yoyote ya kuexpose kinachoendelea.
 
Nilianzisha nyuzi si chini ya 3 kuwaonya kuwa musioe wanawake wenye mshahara. Mukaja juu na kusema umalaya ni tabia ya mtu.
Kama umalaya ni tabia ya mtu basi wafanyakazi wote ni Malaya.
 
Mwenye mimba ni wewe ama
Hakuna mwanaume anaeweza kuleta upumbavu huu kwa watu
Kweli boya
 
Kuna muda unajifanya mwanamke,kuna muda unajifanya mwanaume,kuna muda unajifanya shoga kuna muda unajifanya lesbian ..unatuchanganya ujue!!
 
Mpaka nimeamua kukuandika sijui nifanye nini, mimi ni kijana wa miaka 33 nimeoa na nina mtoto mmoja na sasa hivi mke wangu amekwenda nyumbani kwetu kujifungua na hii ndio sababu ya mimi kuja kukuandikia.

Iko hivi, mimi na mke wangu tulikuwa vizuri sana katika ndoa yetu, ni mwanamke ambaye niliona ananiheshimu na kujali kweli kila mtu anampenda. Hatujawahi kugombana lakini wiki mbili zilizopita alikwenda kujifungua nyumbani kwetu, mimi ndiyo nilimpeleka lakini kurudi nyumbani katika kuhangaika kufanya usafi ndiyo nikakuta kuwa kuna laini ya simu ambayo ilikuwa kama imedondoka.

Nilipanga kuitupa ila nikaamua kuiweka kwenye simu kuangalia. Sikukuta kitu cha maana hivyo nikaamua kuitoa ila kabla ya kuitoa kuna SMS Mbili ziliingia ni kama zile zinasubiri uwashe simu ndiyo ziingie.

Ni meseji za mwanaume ambaye alikuwa akilaumu mke wangu kwa kwenda kwetu kujifungua. Kuna SMS moja ndiyo uliniumiza zaidi, uliandikwa “Mtoto wa kwanza nilihudumia mimba unajifungua mtoto kafanana na huyo mwanaume wako! Huyu wa pili nimekuambia anataka niwe karibu na wewe umeenda kujifungulia kwenu?

Nataka ujue kwamba huyo mtoto kama ni wangu ukirudi namchukua sitaki mwanangu kuishi na huyo Boya!”

Niliiangalia ile namba nikaja kugundua kwamba ni namba ya mfanyakazi mwenzake, nikafuatilia mtandaoni nikajua ni mtu ambaye namfahamu hata kwenye harusi yetu alikuja huyo kaka na wafanyakazi wenzake tena kama familia yake hata ile kutafuta hoteli kwa ajili ya wageni nilitafuta mimi na huyo ni mmoja wao wale ambao alitoa list ya watu wake watakaokuja siku ya harusi.

Sikujibu chochote hizi meseji na mpaka sasa hivi hakijatumwa chochote, nahisi labda mke wangu kamwambia kuwa hiyo laini kashapoteza sijui, ila ninachowaza sasa hivi nifanye nini? Nimekaa na hiki kitu wiki mbili mwenyewe nahisi kuchanganyikiwa kweli najiona kabsai nafanya vitu ambavyo sivyo naomba ushauri nifanye nini?
We kweli boya......kuna cha kuuliza hapo wakati majibu unayo?
 
Back
Top Bottom