Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Kwa utamaduni tulivyozoea neno "mkopo"humaanisha deni lililowekewa utaratibu wa kulilipa. Vilevile,ili mkopo uweze kutolewa,lazima mkopeshaji ajiridhishe kuwa mkopaji anao uwezo wa kurudisha kwa kuangalia mazingira,uwezo na aina ya udhamini. Taasisi za kifedha kama benki zinao uwezo mkubwa wa kufanya kazi hii,na zimefanya hivyo kwa maelfu kama sio malaki ya wananchi kama wajasiriamali wadogo,wa kati na hata wakubwa. Muhitaji huchukua mkopo pale anapoona ni lazima kama mtaji wa msingi au kuongezea alionao.
Kwa upande wa Mikopo ya Elimu ya juu,taasisi za kifedha chini ya mikataba maalumu, nashauri kutoa mikopo hii kwa wanafunzi wetu huku bodi ya mikopo ikiwa kama mratibu na serikali pamoja na wazazi au itakavyoonekana inafaa wakawa wadhamini. Nashauri hivi kwa vile sio rahisi bodi ya mikopo ikajua mazingira ya kiuchumi ya wanafunzi na wazazi wao kwa nchi nzima kwa kuangalia taarifa walizopelekewa bila kutokea dosari au udanganyifu. Nia ya serikali ni njema kuwa na bodi ya mikopo lakini haina wawakilishi maeneo yote nchini kuhakiki taarifa hizo kwa usahihi. Ni ukweli kuwa taasisi za kifedha kama benki ya NMB iko kila kona ya nchi hii na kama taasisi ya kifedha yenye uzoefu na utoaji mikopo, ikitumika kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo au itakavyoonekana inafaa,kazi hii inaweza kuwa rahisi zaidi. Mfano, continuing students watakaokosa mikopo,na wanatoka familia masikini,wangeweza kudhaminiwa na serikali katika mpango maalumu kupitia taasisi hizi wakamalizia masomo yao.
Haya ni maoni yangu kwa lengo la kuboresha zoezi hili .