USHAURI: Mchumba wangu anataka mwanamke wa kusimamia mali zake ananiambia haoni sababu ya mimi kupoteza muda wangu chuoni

huyo mwanamme hakupendi(angekupenda angekuwa anasisitiza usome zaidi ili uwe na maarifa zaidi ya kuangalia hizo so called mali zake)elewa educations its a key kwa kila kitu hapa duniani.and you still very young miaka 23 only unataka kuolewa why?weka nondo kichwani mpaka PHD the rest will follow.
 
Mimi ni binti wa miaka 23, sijaolewa lakini nina mchumba wangu kashajitambulisha kwetu na kila kitu kimekamilika, niko chuo mwaka wa pili naingia mwaka watatu. Sababu za kuja huku nikuomba ushauri, mchumba wangu ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha tena sana, kwa sababu hiyo anawasaidia wazai wangu na wanamsikiliza kwa kila kitu mwezi uliopita aliniambia kua nikifungua chuo hataki niendelee kusoma.

Anasema anataka kuoa mwanamke wa kusimamia mali zake si wa kwenda kuajiriwa ananiambia haoni sababu ya mimi kupoteza muda wangu chuoni wakati hata nikimaliza sitafanya kazi aliponiambia nilikataa na kumuambia mimi ni mpaka nimalize chuo, lakini alienda nyumbani kwa wazazi wangu na kuwaambia mimi simsikilizi na kama nataka ndoa basi niache chuo kwani hakina maana kila kitu atanipa.

Huwezi amini wazazi wangu na ndugu zangu wote wako upande wake, wananiambia niache chuo kwani hakina maana nisijekukosa mume sababu ya elimu ambayo haina hata ajira. Pamoja na kunishawishi nilikataa lakini mimi sijapata mkopo hivyo wazazi wangu ndiyo wananilipia ada, wamegoma kunipa pesa ya ada na wananiambia kama ninataka kusoma sana nijisomeshe, wao wanataka niolewe kwakua tu mwanaume anapesa. Nimechanganyikiwa niiko njia panda sijui chakufanya ni nini?
Iwapo wewe binafsi unaona mumeo mtarajiwa anania njema nawe kwa siku za mbeleni , na wakati huohuo wewe unataka ukamilishe ndoto yako ya masomo, na wazazi wako wameishajitoa kuhusu malipo yako ya ada, nakushauri UAHIRISHE masomo yako , ufunge ndoa, baada ya hapo iwapo bado utaona kuna unahitaji kusoma, unaweza malizia kozi yako online , ama kwa njia nyingine yeyote inayofanana na hiyo. Ni muhimu sana utambue kuwa hadi amefikia uamuzi wa kukutaka usimamie mali zake, basi tambua ana nia njema kwako na iwapo ataona hueleweki anaweza tafuta mchumba mwingine.
 
Postpon masomo yako usiachenl na kwakuwa huna mkopo utakubaliwa ombi lako kirahisi then akishakuoa baada ya miaka miwili angalia upepo kama bado msimamo wako upo vilevile au umebadilika mana mtakuwa mshazoeana.
Utaamua aidha usome evening class baada ya kusimamia hiyo azi
Au kosoma mchana mana unaweza kumshawishi umuhimu wa unachokisoma but lazma kifananane na usimamiz wa fedha, raslimali watu au biashara ndio anaweza kukuelewa but sio usome local government au education utegemee utamshawishi.
 
Jiongeze mpige hela shemeji kahonge chuo!.. Mwaka mmoja unadhani ukitoa 3Mil HOD wako ataikataa !!.. Kwako maji ya shingo tayari huna haja ya elimu nunua cheti!..
The trouble is if you don't, risk you risk more!
Eenh
 
Kukuoa hajakuoa akuachishe chuo kwani ukiwa unasoma huku unasimamia biashara zake tatizo liko wapi eti

Na ww umeshafanya moyoni maamuzi ya kumsikiliza mchumba wako na wazazi wako ebu fanya vile moyo wako unapenda mwana kuyataka mwana kuyapata
 
Postpone then utajiendeleza, maana uking'ang'ania kusoma alafu huna wa kukusomesha nako ni kazi bure. Maana hata wazazi wako hawako upande wako....labada kama unaweza kujisomesha

FANYA OPORTUNITY COST..!
 
Haka katoto hakana adabu, tajiri mkubwa anatafuta mtu wa kusimamia mali, si aajiri watu.. na kabla yako hadi amekuwa tajiri mkubwa nani alikuwa anasimamia hizo mali??
Mkuu! Hii ni chai kama chai zingine za hapa jf, yaani mnaamini kweli huu ni ukweli?
 
Busara ndogo sana maishani inaweza kukuweka mbali na mabalaa makubwa sana maishani!!!.....

Mwenye makosa ni wewe mtoa mada kwa Kuweka mbele mahusiano hata kumfanya huyo jamaa akuone kama mke wake na kujiona ana haki kama Mume....nadhani ni kwa sababu ya fedha!!!....

Mimi kwa utu uzima wangu nahisi kuna jambo nyuma ya pazia....kuhusu jambo hilo kwa mume wako ambalo hujaamua kuliweka hapa hadharani!!!.....

Inawezekana maisha na mambo yako ya chuo unayaweka mbele hata kwenye mahusiano yako!!!....

Hata hivyo inaonekana huyo jamaa hajakomaa kiakili na ana masimango sana!!!....

Fanya maamuzi sahihi kwa kuijenga kesho yako sahihi.....
 
Kubali mawazo ya wazazi wameshaona mbali
Waweza ukaendelea na ukajikuta maisha yako mabaya na mimba juu
Na mbaya zaidi mimba ya boda boda
Utajuta zaidi
Kila kitu pesa mama nawe zishakusogelea ni kuzitunza tu
Akiolewa na kuachika muda mfupi itakuwaje na chuo aliacha?

Kwanini asimalize chuo na hiyo elimu itamsaidia zaidi kuendesha biashara zao na mumewe?

Huyo ajue anaolewa na mwanaume mjinga na mwenye wivu sana.
 
Ulienda chuo ili upate nini? Ukijua sababu ya wewe kutafuta elimu itakua rahisi sana lufahamu kama kuna sababunya kuwa mwanachuo au la!
 
Kubali mawazo ya wazazi wameshaona mbali
Waweza ukaendelea na ukajikuta maisha yako mabaya na mimba juu
Na mbaya zaidi mimba ya boda boda
Utajuta zaidi
Kila kitu pesa mama nawe zishakusogelea ni kuzitunza tu
Kuna very thin demarcation kati ya ushauri wako na ule wa kikalumanzira
 
Back
Top Bottom