Ushauri: Nataka kuondoka nyumbani sababu ya manyanyaso kutoka kwa wazazi

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Habarini wakuu! Ni mimi kijana wenu humu JamiiForums napitia nyakati ngumu kwakweli, nahitaji masaada wenu.

Anyway kama mnavyojuwa week iliyopita kama sikosei hivi nilikuja na uzi humu baada ya kuona home manyanyaso yamekuwa mengi hasa kutoka kwa mama. Kila ninapojitahidi kutimiza majukumu yangu home bado manyanyaso hayaishi, naambiwa sioshi vyombo vizuri, kule uwani sipafanyii usafi vizuri na maneno mengine mengi.

But it's okay, nilikuja na wazo langu la kuondoka home ili niepuke na manyanyaso ya mama na mipango yangu ilienda kama nilivyopanga, maana nimeshapata baadhi ya rooms za kupanga imebaki mimi kuhamia.

Na kama mnavyojuwa pesa ninayotegemea kuanzia kulipia kodi ya ghetto na kununua mazagazaga mengine bado naisubiria, maana pesa hiyo nimeshaipigia bajeti itakuwa ni hela ya boom awamu ya pili ila bado mzigo haujatiki. Ila nishaongea na Katibu wa mkopo chuoni kwangu ameniambia kuanzia wiki hii mzigo unaweza kutiki.

Of course, kuna wadau humu walinishauri niondoke home kwa amani ili nipate baraka za wazazi, nami ushauri wao nimeufanyia kazi lakini mambo yamekuwa tofauti na nilivyotegemea.

Iko hivi, leo mchana nimewaambia wazazi wangu freshi tu suala langu la kuondoka home na kwenda kuanza maisha ya ghetto, wakanihoji sababu zangu ni zipi za kutaka kuondoka nyumbani, kwakuwa nilikuwepo na wazazi sikutaka kuwaelezea manyanyaso yao ndio yananifanya mimi kuondoka home bali niliwaelezea tu kuwa sasa hivi najiweza kujihudumia pia nahitaji kuwapunguzia majukumu yao kwangu.

Lakini jibu nililopata naambiwa naonekana mjeuri, sijui nimeshaanza uhuni au kuna uhuni nataka niende nikaufanye huko ninakotaka kwenda. Mara mama ananiambia ninataka kukwepa kazi za hapa nyumbani, mara naambiwa naenda kufuata wanawake huko, naambiwa nitaenda kupata tabu yaani maneno yalikuwa mengi.

Okay, anyway kumbe kutaka kuondoka kwangu home na kwenda zangu ghetto naonekana mjeuri, naonekana nataka kukwepa kazi za home? But it's okay, leo ndio nimeamini sametimes wazazi michosho (Mizinguo).

Hapa inabidi niondoke tu hata bila ya kupata ruhusa kwa wazazi, hakuna cha kupata baraka za wazazi wala nini. Baraka za Mungu tu pekee zinanitosha mimi kuniongoza huko ninakotaka kwenda.

Natanguliza shukurani wakuu.
 
Wewe nae , tulikuelekezaje hapa?!

Sisi tulikuambia nenda ukatafute Geto lako zuri, weka vitu vyako then unaanza kuhama taratibu. Siku nyingine unawaambia una discussion utalala huko huko, siku nyingine unalala home.

Ukishaanza kupotea taratibu then wazazi watajua tu kuwa huyu mtoto ana makao mapya wakikuuliza wewe wape visingizio. Tena ikibidi unawaambia mazingira ya chuo inabidi usogee karibu na chuo sababu shughuli za chuo zinakulazimu kukaa hostel na wenzako.

Sasa wewe unawaita wazazi unaanza kuwapa risala wazazi wenyewe hawakukubali wanakuona kilaza, mzembe, hauna akili na hauwezi jisimamia unategemea upate matokeo mazuri khaaaaaah we mtoto.
 
Wewe nae , tulikuelekezaje hapa?!

Sisi tulikuambia nenda ukatafute Geto lako zuri, weka vitu vyako then unaanza kuhama taratibu. Siku nyingine unawaambia una discussion utalala huko huko, siku nyingine unalala home...
Basi nitakuwa nimeamua makosa kuambia wazazi kumbe hili suala nilitakiwa nifanye kimya kimya. Asante ndugu ushauri nzuri nishau note ngoja niufanyie kazi.
 
Habarini wakuu! Ni mimi kijana wenu humu JamiiForums napitia nyakati ngumu kwakweli, nahitaji masaada wenu.

Anyway kama mnavyojuwa week iliyopita kama sikosei hivi nilikuja na uzi humu baada ya kuona home manyanyaso yamekuwa mengi hasa kutoka kwa mama. Kila ninapojitahidi kutimiza majukumu yangu home bado manyanyaso hayaishi, naambiwa sioshi vyombo vizuri, kule uwani sipafanyii usafi vizuri na maneno mengine mengi.

But it's okay, nilikuja na wazo langu la kuondoka home ili niepuke na manyanyaso ya mama na mipango yangu ilienda kama nilivyopanga, maana nimeshapata baadhi ya rooms za kupanga imebaki mimi kuhamia.

Na kama mnavyojuwa pesa ninayotegemea kuanzia kulipia kodi ya ghetto na kununua mazagazaga mengine bado naisubiria, maana pesa hiyo nimeshaipigia bajeti itakuwa ni hela ya boom awamu ya pili ila bado mzigo haujatiki. Ila nishaongea na Katibu wa mkopo chuoni kwangu ameniambia kuanzia wiki hii mzigo unaweza kutiki.

Of course, kuna wadau humu walinishauri niondoke home kwa amani ili nipate baraka za wazazi, nami ushauri wao nimeufanyia kazi lakini mambo yamekuwa tofauti na nilivyotegemea.

Iko hivi, leo mchana nimewaambia wazazi wangu freshi tu suala langu la kuondoka home na kwenda kuanza maisha ya ghetto, wakanihoji sababu zangu ni zipi za kutaka kuondoka nyumbani, kwakuwa nilikuwepo na wazazi sikutaka kuwaelezea manyanyaso yao ndio yananifanya mimi kuondoka home bali niliwaelezea tu kuwa sasa hivi najiweza kujihudumia pia nahitaji kuwapunguzia majukumu yao kwangu.

Lakini jibu nililopata naambiwa naonekana mjeuri, sijui nimeshaanza uhuni au kuna uhuni nataka niende nikaufanye huko ninakotaka kwenda. Mara mama ananiambia ninataka kukwepa kazi za hapa nyumbani, mara naambiwa naenda kufuata wanawake huko, naambiwa nitaenda kupata tabu yaani maneno yalikuwa mengi.

Okay, anyway kumbe kutaka kuondoka kwangu home na kwenda zangu ghetto naonekana mjeuri, naonekana nataka kukwepa kazi za home? But it's okay, leo ndio nimeamini sametimes wazazi michosho (Mizinguo).

Hapa inabidi niondoke tu hata bila ya kupata ruhusa kwa wazazi, hakuna cha kupata baraka za wazazi wala nini. Baraka za Mungu tu pekee zinanitosha mimi kuniongoza huko ninakotaka kwenda.

Natanguliza shukurani wakuu.
Inawezekana pengine ulikuwa huwajui wazazi wako kuwa ni watu wenye maneno maneno au ni vipi? Inaonekana kama ni tabia yao hii!
 
Back
Top Bottom