Ushauri, Master Degree Programme

von tosy

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
251
155
Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dodoma katika fani ya Mazingira. Nikiwa nimehitimu Bach. Of Arts In Geography and Environmental Studies (Ba,GE's) mwaka 2016

Baada ya kumaliza Degree yangu ya kwanza natamani kujiendeleza zaidi kimasomo ili kuweza kuongeza maarifa pia na ujuzi katika fani niliyosomea. Lengo la Uzi Huu ni kuomba ushauri Kwa watu waliopo katika fani mbalimbali kuhusiana na maswala ya soko la ajira katika degree programme zifuatazo

Master of Disaster Risk Management (M.DRM) kutoka chuo kikuu cha Ardhi

Master Degree in Environmental Planning and Management (MEP) kutoka chuo cha mipango Dodoma

Master of Science In Environmental Management (MSc.EM) kutoka chuo kikuu cha Mzumbe

Master of Arts in Geography and Management (MA GEM) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Nitangulize shukrani Kwa wale wote watakaokua tayari kuchangia Uzi huu Kwa lengo la kuelimisha na kutoa uzoefu walionao katika fani ya tasnia husika (Mazingira).

Naimani Uzi huu utakua msaada mkubwa kwangu na Kwa vijana wengine wenye mlengo unaofanana na wangu.

Nawasilisha.
 
Kama, unazungumzia kuajiriwa umepotea bora tu hiyo hela ya kusomea hizo program ukalime mashamba au fanya biashara ili baadaye usije leta mrejesho baada ya miezi 18 au 24ya masters yako ukaanza kulialia.

Sikukatishi tamaa, ila wazo la kuajiriwa unapoenda kusoma litoe kwanza katika mipango yako.

Zaidi, twambie ni kwa nini unaenda kusoma hiyo masters maana hujamaliza hata academic year moja tangia umehitimu hiyo bachelor yako.

Mwisho, program yoyote inasoko pale tu utakapo jitambua wewe binafsi kuwa unahitaji kuwa wapi na kufanya kazi ipi.

Ila kusema.kuhusu soko la ajira kwa kufatisha program aliyosoma mtu hiyo bado sana.
 
mkuu mm napenda kujua tofauti yenu mliosoma bachelor of arts & enviromental studies na wale waliosoma bachelor of science in enviromental studies. pia kama kuna tofauti ya kiutendaji au mjkm!!
 
Elimu ya kutafutia ajira ni degree huko kwingine mbwembwe tu na unaweza usiajirike.

Sikukatishi tamaa ila huu ndio ukweli, utajijengea expectations ambazo ukienda ajirani hutazikuta au ukakuta watu wana bachelor's unataka wakufundishe Kazi Wewe mwenye Master's.

Masters maana yake ni Coach'Mkufunzi' ajiriwa kwanza update uelewa
 
Back
Top Bottom