Ushauri kwenda honeymoon wakati nimekuwa nae kwamuda hivi sasa

Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
882
1,029
Habar za humu nategemea kufunga ndoa hivi karibuni...hili swala la honeymoon bado instigators kulingana nA bajeti yangu ya harusi


Mchumba nimeishi nae kwa muda miaka mitatu hivyo siioni haja kwenda sababu tayari nimemzoea

Naombeni ushauri maana cjui hii honeymoon sijui ilingia vip kwenye jamii yetu ya watanzania na hata umuhimu wake kwenye jamii
 
Mkuu nenda tu, yani kwa miaka mitatu hapo hapo kwenye kitanda kile kile, shuka maybe zilezile. Change mazingira mkaongee na mipango mingine baada ya harusi. Safari kama hizo ni muhimu, mzee utasimamia kucha kama fisi maji, ila usisahau kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.
 
Habar za humu nategemea kufunga ndoa hivi karibuni...hili swala la honeymoon bado instigators kulingana nA bajeti yangu ya harusi


Mchumba nimeishi nae kwa muda miaka mitatu hivyo siioni haja kwenda sababu tayari nimemzoea

Naombeni ushauri maana cjui hii honeymoon sijui ilingia vip kwenye jamii yetu ya watanzania na hata umuhimu wake kwenye jamii
Hivi, mwanamke umeishi nae kinyumba zaidi ya miaka miwili,unaweza kuendelea kumuita ni mchumba wako?
 
Hili swali nilishawahi kujiuliza bila majibu. Sioni umuhimu wake kabisa zaidi kupoteza pesa tuu bila sababu
 
Weka pesa kwa ajili ya familia.
Honeymoon mliisha enda zaidi ya moja,ila sema tu hamkuirasimisha kwamba ndio Honeymoon yenu.
Kwa muda mliokaa hata muende wapi hakuna jipya.
Asikudanganye Mtu,wenye raha hasa ya Honeymoon ni wale ambao waliooana bila kuanza kufanya zinaa.Hawa ndio wanaijua raha ya Honemoon,ila hawa watu ambao wanaziniiiiii eeeeeee eti kisha wanaowana hapo inakuwa wanajidanganya tu wao na nafsi zao ila hata waende London basi inakuwa hakuna jipya wala hakuna ile hamasa na mzuka wa Honeymoon.Itabakia tu kuulizana Baby ume enjoya Honeymoon yeti,eee nime enjoy kweli baby,huku nafsi zinajisuta.

Weka pesa utumie kwa Mustakabla wa maisha na muendelee kufanya day outing zeni za kawaida tu huku maisha yanaendelea.
Angalizo:-Soma Maandiko,Honeymoon haijaletwa na hao Wazungu
Hembu soma Maandiko na Matendo ya enzi izo.Utaona kwamba wapo Walioowa na kupewa sehem maalum baada ya ndoa zao.The only logic ya Honeymoon ni kuwa na Mkeo baada ya ndoa sehem ambayo ni ngeni kwenu nyote,inaweza kuwa ni Mji,Mtaa,au Hata Nyumba.Lengo ni Faraja
 
Kwenye hiyo miaka mitatu hakuna siku mmeenda ata zanzibar,mbugani au kwingineko kuliko tulia mkatulia ata kamwezi kamoja? Kama unahiyo calture hunymoon sio muhimu sana,shida ni kwa wale msio nayo mjajifungia hapo hapo miaka hamsini yote hamna holiday
 
Kak nenda tuu hawa viumbe ni kama watoto , angalia m c anze na bifu
 
Aseeeeh. Ngoja na mim nifanye mpango mkuu rika langu wote mnaniacha tu nawaangalia mnavyoa
 
Watu mnacomplicate mambo mpaka wavivu wa kufikiri wanaogopa kuoa,kila siku mnazusha vitu vya ajabu ajabu ambavyo havina maana yeyote na ni uzushi uliotukuka.

NB;Natabiri kwenye Biblia agano lijalo HONEYMOON itaandikwa so kaeni tayari kulipokea neno la BWANA
 
mmmmh hii kitu kiukweli mi bado sijaona umuhim wake hasa kwa vijana wa siku izi. Maana unakuta demu kashajiongeza kahamia geto kwa mhuni halafu baada ya harusi eti ooh sijui nini na nini...
ngoja ntajaribu na mimi nione kama kuna issue
 
Honey moon haina maana ni kutumia pesa vibaya mtu unafahamu korido zote kwa huyo mchumba wako fungen ndoa mrudi nyumbani hiyo pesa fanyien mambo mengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom