kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,178
- 16,864
Kufungwa jela sio jambo zuri kwa vyovyote vile kwakuwa ukishafungwa gerezani kuna wanaofurahia kufungwa kwako na kuna wanahuzunishwa na kufungwa kwako vilevile. Kifungo kikishakuwa cha muda mrefu gerezani au kuhukumiwa kunyongwa kabisa wale waliokuwa wakikutegemea mwisho wake watakata tamaa na kutafuta njia mbadala ya kuyafanya maisha yao yaendelee bila wewe. Na wale uliokuwa umewakosea hadi ukahukumiwa kifungo na wao watasamehe na kutafuta njia mbadala za kuyafanya maisha yao yaendelee.
Sasa ukipata msamaha wa kutoka gerezani kama huu mliopata kutoka kwa Mh. Rais wa nchi na kurudi uraiani tena hiyo itakuwa bonge la surprise kwa uliowaacha uraiani kwa muda mrefu na kuanza kutafuta njia mbadala za kuendesha maisha yao bila wewe. Na hapa ndipo ninapotaka kukuonya wewe ndugu yetu uliopata msamaha ili usije ukarudi tena gerezani muda sio mrefu.
Fanya yafuatayo ukifika nyumbani kwako/kwenu:
1. Tulia kimya kwa miezi 3 bila kusema na watu au vyombo vya habari. Muda huu ni muda wa kusikiliza tu na kujifunza mazingira. Angalia TV, Sikiliza Radio, soma magezeti zaidi na kufanya ibada. Usiende mbali na nyumbani. Epuka kabisa kuongelea lile lililokupeleka kifungoni kwa kukiri au kujitetea.
2. Kama unaweza hama nyumba, mtaa, kijiji kwenda kuishi mazingira mapya kabisa.
3. Familia yako: Utakuta, ataona na kusikia mengi sana kuhusu familia yako wakati haupo, usirushe ngumi au kupandwa na jaziba. Anzia pale ulipopakuta kwenda mbele sio kurudi nyuma. Acha kama ulivyovikuta au unavyoviona na kuambiwa. Usihamaki. Ikibidi fuatilia kwa kutumia sheria zaidi kuliko hisia zao ili kujiepusha na kufanya kosa lingine.
4. Changanya ujuzi na uzoefu uliokuwa nao kabla na baada ya kufungwa kuboresha maisha yako zaidi kuliko ulivyokuwa kabla ya kufungwa.
5. Polepole rudia hali yako ya kawaida kwenye jamii- maana maisha yanaendelea.
6. Simulia kwa jamaa, ndugu, watu na wanajamii ubaya wa kufungwa jela ili iwe kanyo kwao wapende kutenda mazuri tu. Usisimulie raha ulizozipata gerezani (kama zipo) ambazo labda zilitokana na udhaifu wa baadhi ya wafanyakazi wa magereza.
7. Epuka vyanzo vya uhalifu kwa kutii sheria bila shuruti.
8. Dai haki zako kwa kutumia vyombo vya sheria na mamlaka halali za kijamii.
Poleni sana ndugu zetu.
1.