Ushauri kwa ustawi wa nchi

Ushauri kwa ustawi wa nchi

callixtus

Member
Joined
May 7, 2015
Posts
86
Reaction score
31
Nimekaa na kujiuliza kuwa serikali inakazania sana wanafunzi wasome masomo ya sayansi hata mimi naunga mkono jitihada hizo na niipongeze serikali kwa kuajiri walimu wa sayansi kwani tunaupungufu mkubwa wa wataalam wa sayansi na nimeguswa sana na mh Dk. Kikwete leo kwamba tuna wataalam 3 wa upasuaji wa mishipa ya faham nchi nzima sasa najiuliza hawa wanafunzi wanaosoma sayansi watafundishwa na nani?

Simaanishi walimu hawapo hapana wapo lakini walimu wa sayansi ndo hatuna nikajiuliza kwann hawapo nikajijibu mwenyewe hawautaki ualimu kwa kuwa hakuna maslahi kama udaktari mfano mzuri kuna kijana ana D 3 kwenye sayansi ana div 4 point 29 kaenda kuchukua clinical na akipata ajira atamzidi mshahara mwl mwenye div 3 kwa sasa na huyu mwenye 3 ujue ni wa art maana angekuwa sayansi angeenda kusomea uuguzi sasa najiuliza nani mwenye div 3 atakaye taka kwenda ualimu ili hali anasifa ya kwenda kusomea uuguzi ambao hivi sasa wanamshahara mkubwa kuliko mwalimu?

Cha ajabu askari ana mshahara mzuri lakini hata kama ana div 4 point 29 anaenda depo? ninani miaka hii anajivunia kwenda ualimu?

Mfano huko vijijini muuguzi ana div 4 point29 anaitwa dokta tena wanajua ndo msomi lakini mwenye div 3 anaona-enekana maskini wa kutupwa hivi miaka ya 2050 hii nchi itakuwa na wataalam hao ili hali watu hawatokimbilia ualimu kwa kuwa hakuna maslahi tusipowapata walimu hao wataalam tutawatoa wapiiiiiii mmh sijui lakini huu ni mtazamo wangu tu.
 
Hebu nyoosha maelezo zaidi tupate ujumbe wako.
 
Back
Top Bottom