johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 96,225
- 168,790
Najua zipo kanuni zinazoongoza mawasiliano ndani ya bunge na wala sizipingi.Ninachoshauri ni matumizi ya lugha ya kiuongozi ndani ya bunge na si wabunge kujiongelea tu kama wapo vijiweni.Mathalani mbunge anapoizungumzia taasisi nyeti kama TISS umakini ktk lugha ni muhimu ili asivuke mipaka.Au namna ya kulizungumzia jambo ambalo bado liko katika upelelezi wa polisi kunahitaji umakini mkubwa, kinga pekee ya kibunge siyo sababu ya kuingilia upelelezi.Nilisikia michango ya Zitto, Bashe na Aeshi bungeni, walikuwa na hoja nzuri lakini zinazoonyesha wazi kuna tatizo la mawasiliano ama ktk mhimili wenyewe wa bunge au kati ya bunge na serikali.Lakini hii ya Kessy na wimbo wa Roma ndio imeleta kitendawili cha tumuamini nani kati ya Kessy na Waziri mwenye dhamana aliyedai aliviagiza vyombo vyote iwapo kuna tatizo kwenye wimbo wowote basi apewe taarifa yeye kwanza lakini hana taarifa zozote ziwe za Roma au msanii mwingine yeyote.Lakini baya zaidi ni kutolea mifano nchi kama Rwanda, Arabs na Kongo ambazo tuna mahusiano nazo kiushirikiano.Ahsante nawasilisha.