stabilityman
JF-Expert Member
- Jul 9, 2024
- 852
- 1,805
Wanakwambia watoto wanafeli kwa sababu ya njaa ni fact ndio lakini sio hiyo peke yake hata ufundishaji walimu weupe sana kichwani wanatafsiri notes tu, japo wapo wachache wao hasa hao wapo shule kubwa kubwa lakini hawa wengine ni wapo shallow sana! hata wakikasirikaInasikitisha sana nasio dar es salaam tu hata huku mkoani Kuna baadhi ya shule wanatoza fedha kwaajili ya chakula.
Hapo Walimu Wanashikilia Kama Ruba VilePesa za mitihani na tuishieni za lazima ambazo pia ukifuatilia hawafundishi
Kila Mkoa Kazi Kukusanya Michango Wazazi Tupo Hoi HatupumuiInasikitisha sana nasio dar es salaam tu hata huku mkoani Kuna baadhi ya shule wanatoza fedha kwaajili ya chakula.
Wanakomaa kweli kweli 500 ya mtihani lakini tukija kwenye ufaulu wa mitihani ya taifa hola, visingizio vinakuwa vingi ooh watoto hawasikii mara oooh mara ooohHapo Walimu Wanashikilia Kama Ruba Vile
Tumia akili vizuri kumuelewa mleta uzi ..hoja yake 👉ni kipigo kwa mtoto kwa kukosa hela ambayo siyo jukumu la mtoto bali mzazi au mlezi wakeInasemekana kwa mikoa ya kaskazini moja ya sababu inayochangia wanafunzi kufanya vizuri ni uwepo wa chakula shuleni, wewe mtaalamu unatuambia wazazi wanabebeshwa mzigo mzito wanapotakiwa kuwapa watoto wao buku buku za maosi shuleni, kwa hiyo unamaanisha hakuna haja ya mwanao kupata chakula awapo masomoni?
Una hoja usikilizwePamoja na malalamiko yote hayo kiini cha tatizo ni wazazi.
Hapo wengi mko tayari kuwa na watoto lakini malezi ya watoto hamko tayari.
Wanaume wengi wa kibongo matuzimizi yao binafsi kwa siku ni zaidi ya tsh 10000,, tena hao ni wa kipato cha chini wengine matumizi Yao binafsi kwa siku ni zaidi ya 100000 tena hapo anakwambia kajibana sana.
Mtoto juu ya miaka mitano anahitaji malezi kupitia pesa yako zaidi maana hapo mtoto kaanza shule, muda na akili.
Wazazi wapeni malezi stahili watoto ikiwepo haki ya kufurahia mazingira ya shule bila kuwa na njaa na bila kutamani vya wengine.
Baadae mtoto akiwaka tamaa akaanza wizi au uhuni utamlaumu Nani!?
Pia muwe mnahudhuria vikao vya shule na kushiriki mijadala kuepusha malalamiko kama haya.
Wazazi kutaneni na uongozi wa shule mpange utaratibu mzuri, we unywe supu na chapati mbili halafu mwanao anywe uji, hujui uji unaleta usingizi??Ametoa hoja ya maana kabisa.
Bahati mbaya hio huduma ya chakula shuleni si huduma tena ni biashara.
Mfano shule anasoma mtoto wangu kuna mzabuni anatoa inayo itwa huduma ya chakula, sasa waalimu ndio wamepewa kandarasi ya kukusanya fefha , tena kwetu si 1000 bali ni 1500.
Sasa ole mwanafunzi asie lipa!
Si kilamzazi ana aweza kulipa hio 1500, wengini wana watoto 3, mzazi ana lipa 4,500 kila siku ya masimo.
Tufanye siku za masomo ni 200 kwa mwaka, hapo mzazi awe na zaidi ya milion 2, hapo bado usafiri , bado hela za mitihani kila mwezi 6,000 kwa kila mwanafunzi, michango mingine nk.
Na hio ni shule ya serikali inayo simamiwa na halmashauri!
Lakini tuna ambiwa elimu ni bure!
Hivi wangewapa uji ambao labda iwe 300 hadi 500 ingeshindikana kwa mzazi kweli?
Wasikilize na wafanyie kaziUna hoja usikilizwe
Wazazi wengi hawaendi kwenye vikao wanaishia kulalama nje, mawazo yao wanapaswa kuyawasilisha kwenye vikaoWazazi kutaneni na uongozi wa shule mpange utaratibu mzuri, we unywe supu na chapati mbili halafu mwanao anywe uji, hujui uji unaleta usingizi??