Ushauri kwa Sheikh Alhad

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
9,648
Reaction score
14,999
Ushauri kwa sheikh Alhad.

Moja ya jukumu la Sheikh ni kutoa elimu ya dini, kusomesha vijana, watoto na watu wazima.
Kusomesha sira, hadithi, Quran tukufu au vitabu mbali mbali vya dini.

Njia kuu ni kutenga muda kama masaa 2, saa 1 either kukaa msikitini kusomesha, madrasa au hata nyumbani au ktk shule za waislam.

Njia nyengine ni kutumia media kuwapa mawaidha vijana umuhimu wa swala, zaka, swaumu , kuacha zinaa, ulevi na kamari.

Tunahitaji kukuona ukitumia ilmu aliekupa Allah kupitia social media ukisomesha dini
Mfano mzuri ni Sheikh Walid , kabla na baada ya kuchaguliwa kuwa Sheikh wa mkoa amejikita huko, anasomesha vijana, anasihi wazee, anaamrisha mema katika msingi wa uislam. Baada ya kutenguliwa usheikh wa mkoa hakuyumba amerudi katika malengo makuu ya sheikh

Utamuona sheikh msabah, sheikh mselem, Sheikh Rusaganya, Sheikh Nurdin Kishki nk, ambao wanatumia ilmu ktk kuwafikia waislam moja kwa moja, au sheikh mazinge, Sheikh Shafii ktk kuelimisha wasiokuwa waislam.

Namsihi sheikh Alhad ajikite huko, huko ndiko kwenye kheir, lkn kunatakiwa kuwe subra ya hali ya juu maana mawasiliano kati ya wanasiasa na wakubwa yatakatika lkn mawasiliano na Allah yatakuwa karibu zaidi.

Sheikh upo ktk kamati ya Amani, sio mbaya lkn jikitize lengo kuu wakati lengo kuu la sheikh ni kuwakunjisha watu goti kuwapa ilmu. Sheikh Hassan bin Ameir alkifunga safari hadi Kongo kupigisha goti watu.

Pia Malumbano na wanasiasa yanapoteza muda na unaweza ukajikuta sheikh unatumia muda mwingi ktk dunia ktk kazi ambayo ilitakiwa ifanywe na wanasiasa, vyombo vya dola au mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…