Ushauri kwa Serikali yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa Serikali yetu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Msaranga, Jan 20, 2012.

 1. Msaranga

  Msaranga JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mimi nilikua napendekeza serikali yetu kuunda mamlaka ya udhibiti elimu kama ilivyo ewura.sababu ya ushauri huu ni kwamba sasa hivi garama za shule zimepanda sana kila mtu anafungua shule yake na kupanga bei ya ada yeye mwenyewe.tukiwa na mamlaka hii tutaweza kupanga bei ya ada kwa shule za msingi na sekondari na pia kuweza kuhakiki ubora wa shule hizi.kama jinsi ewura ilivyo weza kuwadhibiti wafanya biashara ya mafuta kuweza kuwa na bei moja ka hapa nawapongeza sana ewura.

  Naomba kuwasilisha wadau tujadili kwa mapana kwa sababu watanzania wanaosemesha watoto wanataabika sana na hizi ada za shule.kwa kuwa zile shule zetu za kata sikuhizi hamna elimu tena kule wengi tunakimbilia english media .
   
 2. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja mkuu, kusema kweli ada za shule binafsi zimekuwa kubwa na wakati mwingine haiendani na hadhi ya shule wala hali za maisha za wananchi wa kawaida lakini pia hata kama shule binafsi zinakuwa na ubora halafu na ada zinakuwa kubwa kupita kiasi halafu mwananchi wa kawaida anashindwa kabisa kugharamia hii itakuja kuleta athari kwa taifa letu kwa maana ya kwamba wale watoto wa maskini watasoma kwenye shule ambazo ni cheap zisizo na ubora na wale matajiri watasomesha watoto wao kwenye shule expensive zenye ubora na hatimaye kutazuka matabaka miongoni mwa wananchi na nadhani ishaaanza kujitokeza, hapa kinachotakiwa ni kwa serikali kuweka mamlaka ambayo itasimamia ubora wa shule na kudhibiti gharama za ada kwa shule hizo, nimesikia kuwa serikali inataka kuweka muongozo huo na sijui washafanya utafiti kiasi gani kuhusu kupata ada elekezi na vilevile hata kama wataweka muongozo wa ada elekezi sina uhakika kuhusu usimamizi wake maana serikali yetu ina tabia ya kutoa maagizo ila ufuatiliaji unakuwa hautiliwi mkazo na inaweza kupelekea kuzalisha mgogoro baina ya serikali na wamiliki wa shule kwa sababu ya kutofanya utafiti wa uhakika na wa kutosha!
   
 3. Msaranga

  Msaranga JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  kwa kweli nakuunga mkono mkuu kwa 100%
   
 4. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Shule binafsi ni huduma kwa jamii na ni biashara pia, wamiliki wanahitaji faida ili kuzidumisha,kuziendeleza na kuziboresha shule zao LAKINI gharama za ada zisiwe zenye malengo ya kupata super profit kiasi kwamba kusomesha katika shule hizo inakuwa kama ni anasa, isije ikapelekea watu wakashindwa kupeleka watoto shule kwa kutomudu gharama kubwa, lengo hasa iwe ni kutoa huduma ya elimu kwa jamii na wananchi wachangie ada itakayowezesha shule kujiendesha na sio ada kuuubwa kama vile kukomoana au kutoa ujumbe kwamba "akina fulani msije kusoma huku".
  Hapa inahitajika mamlaka ya kudhibiti ada na ubora wa shule.
   
 5. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ushauri mzuri ila ni serikali ipi unayoishauri, umesahau kuwa imeweka pamba masikioni na tope machoni, hawasikii hawaoni.
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  mambo aliyosema mwanzisha thread yote ni sawa lakini kasahau kuwa ni serikali gani anayoishauri!
  Hiyohiyo serikali ndiyo imesababisha hayo yote yatokee, laiti ingelikuwa (labda) umebadilisha serikali ndio ungeliweza kuiambia hiyo inayoingia. Kwa maana haya makosa yote sio kwamba wameyafanya bila kujua au kushauriwa na wataalamu bali ndivyo walivyo.
  Lakini kingine, unadhani hiyo ewura inawajibika!?
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Ni kuongeza ulaji tu.Haina maana maana hao EWURA wanafanya cha maana?
   
 8. Msaranga

  Msaranga JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  ULAMAKAFU) EWURA WANAJITAHIDI SANA KUDHIBITI BEI YA MAFUTA LEO HAWA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA WASIOKUWA NA HURUMA UNGEKUTA BEI YA MAFUTA NI 3000tSH
   
Loading...