Katika bajeti ya mwaka huu fungu (vote) lililotengewa fedha nyingi kuliko yote ni malipo/marejesho ya deni la Taifa.. Takriban shilingi trilioni 9..... zaidi hata ya mishahara na marupurupu ya watumishi ..takriban trilioni 8....
Haya mafungu mawili ambayo hayaepukiki (ring-fenced) yatatumia makusanyo karibu yote ya vyanzo vya ndani hasa kodi..TRA inatarajiwa kukusanya sh trilioni 18..
Kuna haja sasa kwa serikali na wadau wengine kubuni vyanzo vipya vya mapato; na hasa kuwekeza zaidi ktk uchumi wa vijijini (rural economy) na pia kujenga mazingira mazuri kwa wajasiriamali wa kati na wadogo waweze kukua na kuweza kulipa kodi...
Ktk uchumi wa vijijini tuwekeze katika upatikanaji wa maji kwa wananchi na wakulima; barabara zinazopitika mwaka mzima; upatikanaji wa mitaji; upatikanaji wa huduma za ugani (extension services)..
Pia nguvu ya serikali ktk viwanda iwe ni kwa vile ambavyo vina mahusiano ya karibu na mazao ya kilimo na mifugo..