Ushauri kwa Serikali 2020-2025

Joseph S

Member
May 3, 2020
13
15
Habariiii
Ndugu wananchi ninaomba kushauri mambo yafuatayo kwa serikali kuanzia 2020-2025.
1.Iajiri maafsa wa kukusanya mapato wengi mpaka ngazi ya kata,kijiji na mtaa.Kazi yao kubwa itakuwa kukusanya mapato kwa ufanisi kulingana na sheria na kanuni zinavyosema.H
Faida zake
  • Ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,kwani mapato mengi yanapotea na mengine hayakusanywi kabsa kwani maafsa wa ukusanyaji mapato kuna baadhi ya maeneo hawayafikii kwasababu ya uchache wao hasa vijijini na hata mijini pia.
  • Itaongeza idadi ya ajira kwani wasomi wengi wataajiriwa kama ma afsa wa TRA
2.Iajiri ma afsa biashara mpaka ngazi ya kijiji au mtaa.Hawa watakuwa wanatoa consultancy kwa wafanyabiashara wote ndani ya eneo husika.Watashiriki kutoa elimu ya biashara kwa wafanya biashara na watu wanaohitaji kufanya biashara.Uwekwe utaratibu kuwa mtu yeyote anayehitaji kufanya biashara ni sharti ni sharti awe anapata guidance ya afsa biashara ili kuleta ufanisi na kuepuka kuanguka kwa biashara.Ili serikali iweze kumudu kuwalipa mishahara hawa maafsa biashara ni sharti ianzishe business consultation fee ambapo mfanyabiashara atalazimika kuilipa pindi afanyapo biashara.
Faida zake
  • Itaongeza wigo wa ajira especially kwa watu waliosomea elimu ya biashara kwani wengi wataajiriwa kama ma afsa biashara.
  • Itaongeza ufanisi katika biashara kwani watu wengi watakuwa na elimu ya biashara hivyo itakuwa ngumu biashara nyingi kuanguka.
  • Itaongeza ubunifu katika biashara.
Kwaleo niishie hapa ila naruhusu kuwachallenged....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom