Ushauri wangu kwa Sam Mahela ni huu hapa;
Kulingana na mambo muhimu ya utoaji wa habari zilizogusa hisia za watu kwa mwaka 2014, tunakuomba ugombee tuzo za mwaka huu, kwa sababu kuna mambo muhimu ya kijamii tisa uliyopambana na habari zikaweza kuifikia jamii na watu wakaguswa na habari zako na ikapelekea hao watu kusaidiwa.
1) Ulifuatilia swala la Bi Salome Mhando, mkazi wa Mabwepande ambaye alitelekzwa na mumewe bwana Ally Nasoro kwa madai ya mkewe kuzaa kupita kiasi, na leo hii yule mama kapata msaada mkubwa mpaka wa kujengewa nyumba na pesa taslimu milioni mbili.
2) Uliweza saidia kufanyika jitihada za kijana wetu, marehemu Sande Mrema, ambaye alikuwa na uzito mkubwa zaidi ya kilo 250 kutaka kusafirishwa, ingawa ilishindikana, lakini kikubwa ulichokifanya ni jitihada zako za kuisaidia ile familia na kupata pesa zao kiasi cha dola 13,802.
3) Alifuatilia sakata la mwanafunzi wa darasa la saba wa kike aliyefungiwa ndani na mwanaume katika eneo la Kinondoni na kumbaka mwanafunzi huyo na kusababisha mwanafunzi huyo kutokufanya mtihani wake wa siku ya pili wa kumaliza darasa la saba mwaka jana, na kubwa zaidi ni mtuhumiwa kupelekwa mahakamani.
4) Swala lingine kubwa ni jitihada zako ulizozifanya kwa kuibua ile habari ya yule kijana aliyekuwa amemfungia kikongwe ndani maeneo ya Manzese zaidi ya miaka 20, ilisemekana kikongwe yule alifariki kumbe alikuwa amewekwa ndani na mtoto wake wa kuzaa, ni habari ambayo iligusa hisia za watu.
5) Ulimsaidia yule mtoto aliyepelekwa India kutibiwa baada ya kunywa kemikali akidhania ni maji na kuharibu mfumo wake wa kuharibu chakula na huyo mtoto saa hizi anaendelea vizuri.
6) Ulimsaidia yule mama aliyekuwa amevimba miguu kwa zaidi ya miaka 15 na yule mama alikuwa na hali mbaya sana, nakumbuka wakati unarusha habari yake inasemekana na harufu alikuwa anatoa mbaya sana, lakini hukujali uliweza mpaka kumshika na kumpa msaada zaidi wa kuhakikisha anakwenda kutibiwa India na jitihada ulizozifanya ni kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu yake mimi mwenyewe nilichanga.
7) Ulifuatilia swala la wanafunzi kuoana wao kwa wao maeneo ya Rorya, Sengerema, Kahama tena ni shule za serikali. Uchafu huo unafanyika kwa sababu ya wanafunzi kukosa mabweni ya kulala matokeo yake watoto huteseka mpaka kufikia hatua hiyo.
8) Pia uliibua habari ya mzee Issa, yule wa Mabibo kufungiwa ndani na watoto wake na mkewe bila msaada, na mzee huyu nakumbuka ile habari alikuwa akijinyea, ulionyesha uvumilivu ukaingia ndani na kujifungia na kumsafisha na kuokoa maisha yake, ni jambo la kupongezwa sana.
WanaJF, ni habari amabazo nimezifuatilia kwa kina na ziko zingine youtube, mnaweza mkaona siyo vitu vya kubuni na ndiyo maana nimeona nimpe ushauri huyu kijana atumie habari hizi kugombea tuzo mwaka huu, kama utabahitika kusoma habari hii ifanyie kazi na usichoke.