choza choza
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 2,289
- 4,093
Kumekuwa na mada nyingi za kukejeli walimu kuwa wana maisha magumu mpaka bodaboda kujilinganisha na walimu (kuna kaukweli ndani yake) sasa hizi ni mbinu ambazo walimu wanatakiwa wazifate ili waishi kulingana na kipato chao
1. Zaa watoto wachache, wakizidi sana wawili, hii itamuwezesha walimu kuwahudumia vizuri kuanzia kula, mavazi, kusoma shule nzuri nk.
Sasa wewe fyatua watoto 5+ na mshahara wako wa chini ya laki 6 ndio kina mpwayugu wanakuja kukuwakia.
2. Punguza wategemezi,
Hakuna kada inawategemezi wengi kama walimu, yani walimu ndio wasaidie wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, mtoto wa mtu akifeli huko anasukumiwa kwa mwalimu ili atafutiwe cha kufanya. (Bodaboda hawana wategemezi) Ewe mwalimu, mtegemezi wako awe baba yako na mama yako tu, hao wengine fanya ukipata hela ya sensa, kusimamia mitihani nk.
3. Jenga nyumba ya wastani
Rejea point namba moja, ya kuzaa watoto wachache, jenga nyumba yako tuu ndogo ya wastani ya kukutosha wewe na wanao wawili na kachumba walau akija baba au mama, sio mwalimu unajitutumua kujenga jumba kama kanisa na mshahara wako huo, utachekwa na mpwayugu.
4. Kama ni mwanaume oa mwanamke ambaye atafanya kazi walau aingize 5000 kwa siku ili isaidie matumizi madogo madogo ya nyumbani.
5. Punguza pombe, narudia tena punguza pombe.
Kwa kipato cha mwalimu halafu kila siku unataka unywe bia 5+, utaishi maisha magumu sana, kama ni kunywa walau mara moja moja kwa kiasi.
6. Achana na mikopo kandamizi hovyo hovyo kama hauna plan ya maana kwa muda huo.
Hapa ndio chanzo cha maisha magumu kwa walimu, mikopo kandamizi. Kuna walimu tangu waajiriwe hawana kadi zao za benki wamezikabidhi kwenye microfinances, asee mnatia aibu! Kopeni kwa mipango sio unakopa ili ukalipe mahari, harusi, gambe nk.
7. Tafuta kausafiri ka pikipiki ka cc100 walau kakusaidie kwenye mizunguko ya hapa na pale ili kuepuka kupoteza hela nyingi kwa watu wa kazi ya laana( bodaboda, nikimnukuu lema) pale ambapo maisha yatakaa sawa unaweza tafuta hata ka ist
8. Punguza wanawake, usizae hovyo hovyo na kila mwanamke maana utaongeza familia za kuhudumia.
Kuna mwalimu kazaa na wanawake watatu tofauti na haishi na hata mmoja, mshahara ukitoka atoe laki kwa kila mwanamke kwa ajili ya matunzo, ni laki tatu hiyo, mshahara wake ni laki 5 na hapo amekopa benki hata hiyo laki 5 hapokei tena, unategemea asichekwe na mpwayugu?
Mwenye kusikia na asikie