Ushauri kwa mwanandoa huyu

Kichochoro

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,135
1,163
Wakuu ni rafiki yangu wa karibu sana mwaka wa tatu anaishi na mke wake ambaye yeye anadai alimuoa tu kutokana na kwamba akiwa single aliwahi kutoka na huyo binti na hatimaye akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito wazazi wa binti walileta hoja kwamba ni mwanafunzi na yeye ili kuua soo akaona akubali kumuoa ili kuepusha mambo mengi kama kupelekwa mahakama na polisi.

Lakini hakuna ndoa yoyote iliyofungwa walivutana tu kienyeji! Sasa rafiki yangu huyu amekuwa akiniita mara kwa mara nimshauri maana anasema huyo mwanamke hampendi kabisa toka moyoni Ila anaishi naye tu.

Sasa anataka kuachana na huyu dada lakini tangu aishi naye hakuna ugomvi wowote ulishawahi kutokea kati yake na yeye Ila kinachomuuma anaishi na mwanamke asiyempenda yaan kiufupi Hana furaha!

Nimeileta hoja hii humu ili niweze kupata mawazo mengine ambayo pengine ninaweza kumwelezea nayakamsaidia.
 
Me nakushauri ya wanandoa waachie wanandoa.

Utamshauri amuache, kesho watakunana huko chumbani jamaa atakuja.

Unashangaa unaenda kw amshikaji shemeji vituko haviishi, leo juice ya pilipili, kesho chai na kabeji, siku nyingine nyama yenye mende.

Walipendana wenyewe, wacha waamue wenyewe.
 
90% ya ndoa nyingi zenye mafanikio,

chanzo chake,
Mwanamke alimpenda zaidi mwanamke kuliko mwanaume alivyompenda uyo mwanamke.

Kibongo bongo tunaita,
  • Alipewa MKE na wazazi au
  • Demu aling'ania kutoka ghetto baaada ya show au
  • Jamaa alimtia mwanafunzi mimba akaona Haina jinsi Bora aoe au
  • Mwanamke alihamishia vitu kwa jamaa mdogo mdogo

Ushauri wangu:

jamaa aendelee kukaa na uyo mwanamke, Kama sofa zote za wife material amekidhi.

Asije akaangukia kwa slay queen akafa kwa kiharusi
 
Mwambie rafiki yako ndoa nyingi zipo hivyo hivyo, (watu wengi wameoa/kuolewa na watu ambao hawakuwapenda/sio machaguo yao)
Amshukuru Mungu kwa kumpa asichokiomba.

Halafu sijui kwa nini inakuaga hivyo.
 
Linapofikia suala la kuoa, mihemko na mahaba ya KIFILIPINO unaweka pembeni.

Mwanaume unatakiwa kuoa mwanamke anayekupenda zaidi ya unavyompenda wewe.

Hii itakusaidia kuwa na familia imara itayofuata amri zako, atakua chini yako na utamsimamia utavyoona wewe inafaa.

Wanaharakati watalalamika huo ni mfumo dume,

Nasema ndio,

Ni mfumo dume unaofaa kabisa kuongoza familia tangu dunia hii imeumbwa.

Wallahi nakwambia ndugu,

Ukifuata hisia zako za mahaba niue.

Ukijichanganya Ukavuta ndani mwanamke uliempenda zaidi ya alivyokupenda wewe, na yeye akalijua Hilo.

Huli hulali na hufurukuti juu yake,

Aisee kwa nnavowajua wanawake wa style hiyo Hakuna rangi utaacha kuona dunia hii

Atakupelekesha mpaka maji utaita "mmma"
 
Mwambie rafiki yako akae na huyo mwanamke asimuache , mara nyingine ndoa upendo huja pole pole
 
Mwambie rafiki yako ndoa nyingi zipo hivyo hivyo,(watu wengi wameoa/kuolewa na watu ambao hawakuwapenda/sio machaguo yao)
Amshukuru Mungu kwa kumpa asichokiomba.

Halafu sijui kwa nini inakuaga hivyo.

kapata asichokiomba
 
Mwambie hana akili, kama moyo wake haumpendi dudu lake linampenda. Huwa nawashauri kila siku kama unaona binti humpendi tafadhari usimwingizie dudu wala usimpe mimba. Sasa hapo utavuna ulichokipanda.
 
Mabaharia wenzangu ..ukimpata demu anakupenda kuliko unavompenda...na kichwani Yuko smart...oa huyohuyo....

Nawewe mama ushauri we mwambie aendelee nae...ukisema waachane afu wakarudiana utakua umejiaibisha
 
Mwambie rafiki yako ndoa nyingi zipo hivyo hivyo,(watu wengi wameoa/kuolewa na watu ambao hawakuwapenda/sio machaguo yao)
Amshukuru Mungu kwa kumpa asichokiomba.

Halafu sijui kwa nini inakuaga hivyo.
Unapewa unachostahili siyo unachokitaka. Hahaa
 
Tamaa ya pisi kali wanywa Castle, wavaa visuruali vilivyochanika mapajani, wanaotembea na simu zinazozidi kipato chao, wanaojipamba kwa vitu artificial ndio inamsumbua.

Mwambie anachokitafuta atakipata. Huyo ndiye mke wake, ukishakabidhiwa na wazazi hiyo ndio ndoa, ndoa sio ule ubwabwa wa ukumbini wala si vile vigelegele vya kanisani.
 
Tamaa ya pisi kali wanywa Castle, wavaa visuruali vilivyochanika mapajani, wanaotembea na simu zinazozidi kipato chao, wanaojipamba kwa vitu artificial ndio inamsumbua.
Mwambie anachokitafuta atakipata.
Huyo ndiye mke wake, ukishakabidhiwa na wazazi hiyo ndio ndoa, ndoa sio ule ubwabwa wa ukumbini wala si vile vigelegele vya kanisani.
 
Back
Top Bottom