sonaderm
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 618
- 1,816
Kwanza nianze kwa kukupongeza kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa television ya wanyonge!
Na hii naweza kusema ni kutokana na uzoefu ulionao kwenye sekta hii ya habari na weledi mkubwa ulionyesha katika kipindi chote..
Wakati unajiandaa kutimiza majukumu yako mapya, ningependa kuangazia maeneo machache ili kuiboresha TBC ambayo naiona kama ishapoteza muelekeo.. Kama kuna mengine wana JF watayasema hapa.
1. Boresha ubora wa picha wa TV. Picha za TBC hazina ubora na hata wakati mwingine studio kunaonekana giza hasa wakati wa taarifa ya habari! Ninaweza kusema watangazaji wa TBC wote wanaonekana weusi wanapotangaza au wanapokuwa studio!
2. Boresha vipindi ili viendane na wakati. Mfano mzuri ni ubunifu hasa kwenye vipindi vya vijana. Jaribu kuwakilisha mambo ya msingi kwa njia rahisi na hasa ukiwalenga vijana ambao ndio wengi na watazamaji wakubwa wa TV! Unaweza ukajifunza clouds TV au EATV.
3. Boresha maslahi ya wafanyakazi wako. Kwa jinsi ninavyoelewa, inawezekana kabisa kituo cha TBC kina watangazaji wengi ila maslahi na delivery ni poor! Ni bora ukawa na watangazaji wenye tija na wachache wenye ubunifu ili waendane na ushindani wa media hapa nchini!
4. Kuonyesha Bunge Live. Jitahidi kadri unavyoweza kutowanyima watanzania kile wanachokitaka. Fanya live coverage ya matukio yote ya kitaifa na muhimu hasa bungeni. Ni wazi watanzania wanapenda kuona mijadala hii moja kwa moja!
5. La tano nitakwambia siku nyingine, ila anza na hayo machache kwanza ili tuone kasi yako!