Ushauri kwa huyu rafiki yangu

Ushauri kwa huyu rafiki yangu

somalilady

Member
Joined
Mar 8, 2021
Posts
23
Reaction score
27
Habar zenu wanajamiiforum..hope ni wazima mnaendelea vzr na majukum ya kitaifa..

Ndugu zangu ushauri wenu unahitajika kwa huyu rafiki yangu..Ni graduate ambae ni jobless bado ..lakini alibahatika kuolewa na jamaa mmoja ambae pia ni graduate wa muda kidogo...wameishi kwa miaka 3 ya ndoa lakini huyu jamaa kiuchumi hayuko fresh pia ni mvivu sana wa kazi...hapo nyuma bidada ndo alikuwa anaprovide mahitaji ya home lakini nae kwasasa hali yake si shwari hana kazi...

Katika miaka mitatu walioishi juzijuzi huyu dada akahisi ni mjamzito na kupima ikaonesha kweli ni mjamzito kibaya alivomwambia jamaa kuwa ni mjamzito jamaa akakubali ila ilivopita wiki uyu jamaa akasafiri akafunga na simu hapatikani mwezi mzima mpk sasa... Dada wawatu yakamshinda akaamua arudi kwao tu maana hamna matumiz wala chochote kitu

Baada ya kurud kwao kuna mtu alikua anamfukuzia huyu dada kabla hata hajaolewa sasa baada ya kupata taarifa kuwa bidada yupo kwao akaamua kumtafuta na kuongea nae..huyo mtu yupo vizuri kiuchumi ni mhadhiri wa chuo pia ana shule yake pamoja na miradi yake mingine...kamfata bidada na kumwambia yeye yupo tayar kukaa nae hata kama ni mjamzito na pia hata familia yake ataisaidia endapo watakua pamoja

bidada hajajua cha kufanya mpk now je, amkumbali uyo jamaa wakaishi pamoja au aendelee kukaa kwao akimsubir jamaa ambae kampa mimba..pia ana hofu ya kumhisi uyu jamaa kama ana mke na watoto ...lakini pia hali ya familia yake si nzuri kiuchumi kiasi kwamba baadhi ya mahitaji ni ngum kupatikana...Na jamaa anataka kama binti atakubali basi wakaishi pamoja....Je, uyu bidada afanyeje?..tumpe ushauri utaomfaa ...

Asanteni...

N:B usikurupuke kuoa au kuolewa.
 
Changamoto ni huo ujauzito wa mtu mwingine.

Matendo na matukio yanayotukuta wazazi huwa yanajirudia hata kwenye maisha ya watoto wetu.
 
Ukweli utakuweka wazi ndugu usijifanye eti rafiki yako

Ushauri msikilizie jamaa kwa muda utakao hisi jamaa ataweza kuja huwez jua labda kuna tatizo limempata

Pili mchunguze huyo jamaa vizur ambaye n mboga Saba (mhadhiri) na ujue undan wake Kama ana familia au la

Tatu ukiolewa na huyo mboga Saba utakuwa umefuata pesa tu ili usaidiwe wewe na kijusi tumboni hvyo jitafakar vizur pesa sio suluhisho la mambo yote

Mwisho kaa chin tulia usichanganyikiwe maisha n haya haya huwez jua Mungu atafungua riziki kwa nyote yaan huyo choka mbaya ( msela wako) na wewe n suala la muda tu SABABU s unaona jamaa hajakataa ujauzito ila uchumi tu umemkimbiza wasiliana na wazazi wake pia wape taarifa juu ya hili wanaweza kuwa na ushauri mzuri


Sikiliza NEREA YA SAUTI SOULS UKISINDIKIZA SIKU YAKO
 
Aisee nimeamini watz sio waelewa ...huyo ni rafiki yangu..ila anyway ukipewa cheo usikatae..acha nichukue ushauri wenu nijaribu kumshauri
 
Aisee nimeamini watz sio waelewa ...huyo ni rafiki yangu..ila anyway ukipewa cheo usikatae..acha nichukue ushauri wenu nijaribu kumshauri
Kama jamaa kasepa na kazima simu hamna haja kusubiri amekupa nafasi ya kutafuta uelekeo mpya wa maisha. huenda katoroka majukumu jumla..
 
Kwa kua ana njaa na aliempata anafedha afanye hivi;
1-asitake kumfahamu sana huyo baba status yake kimahusiano labda kiafya wakapime.
2- amwambie yuko tayari kuishi nae lakini kwakua anamimba amtafutie eneo amjengee nyumba ambayo atakua anaishi nae pamoja pamoja na kabiashara kadogo ambacho kitamfanya aweze kujikimu.
3- akubaliane na khali halisi kua yule keshamuacha hivyi asipoteze muda wake kumtafuta, mwishoe hii bahati itayeyuka
4- kama hataki kumwacha mwanaume wake basi aendelee kusubiri lakini umri haukusubiri wala majukumu......

Hapo ni kucheza kama pele.
 
Ukwr upo ivi uyo mwenye ela emeambiw iyo mimba ni yake na jamaa analea njaa mbaya sana..mimba nyingi uwa tunabambikiwa hapa
 
1. Upendo halisi na wa dhati hauna conditions, mtu unayempenda kweli na shati huwezi muona kwenye taabu ukasema ukinikubali ndio ntakupa hiki na kile, ila utafanya tu maana ukipenda mtu huwezi vumilia kuona anapata shida.

2. Upendo wa dhati hautazami material things kama priority, wote KE na ME wameweka Materials mbele kuliko upendo. Huyo rafikiyo amechanganywa na alivyonavyo jamaa na jamaa nae kajua rafikiyo ananjaa so anamuonesha ambavyo anakosa.

Awe makini sana. Asizidi haribu mambo. Marriage is more of love kuliko materials. Ampende mtu alivyo si vitu vyake. Afadhali abaki kuwa mchepuko wake apate atakacho ila abaki na ndoa yake kuliko kuharibu ndoa kwa asiyempenda maana na kwa huyo atatoka tu.
 
Back
Top Bottom