Ushauri kwa huyu ex-wangu

Ushauri kwa huyu ex-wangu

HABARI za mda huu usiku tulivu
Naomba niende direct kwenye mada
Mimi ni kijana mwanzoni kipindi nipo
O level niliwahi kuwa na uhusiano na msichana mmoja ila yeye alikua anasoma shule ya jirani lakini baada ya kumaliza masomo ya o level Mimi nilifanikiwa kwenda advanced yeye hakufanikiwa hivyoo alibaki mtaani na wazazi wake walimwambia ngoja wajipange ili waje wamsomeshe mwaka mmoja baadae kipindi nipo likizo baada ya muhula wa kwanza wa advance nilimwambia
Mpenzi wangu kuwa naomba MUNGU akijalia tuwe wanandoa mbeleni akakubali na alifurahi sana na hapo mahusiano yalikolea sana na hadi ikafikia hatua ya kunitambulisha
KWA wadogo zake kuwa huyu shemeji yenu
Nilipokuwa form six mwishoni nilipata taarifa kwa mmoja kwa marafiki zangu kuwa mpenzi wangu kuna jamaa mmoja dereva wa TRA anafukuzia mpenzi wako nilipopata taarifa hizo nilikua kimyaaa nafanya utafiti na kimya kimya bila ya kumuuliza mpenzi wangu mana
Nilitaka kuthibitisha jambo hiloo

Baada ya kumaliza paper ya form six narudi tuu home mpenzi wangu mapokezi yake hayakuwa na furaha sana alinipokea kawaidaaa tuu kama nimetoka sokoni ila nilipiga moyo konde kusema labda kwa kuwa tumezoeana

Si unajua siku hizi mifumo ya serikali lazima kupitia jkt kwa form six nami jina langu lilikuwepo basi nilimpa taarifa mpenzi wangu kuwa baada ya week moja na nusu ntaondoka
Kwenda jkt akasema sawa

Kumbe yeye wakati huo mapenzi yapo motomoto na dereva wake wa TRA na alimuahidi kuja kumtolea mahali mwezi wa saba wakati Mimi mwezi wa Sita ndio naenda jkt

Zimebakia siku tatu jioni napata sms kuwa" boyfriend wangu niilikupenda sana ila nimepata mwanaume natolewa mahali mwezi ujao ila mimi siwezi kukuacha mana nimekuozea ila kuvumilia mpaka uje kumaliza masomo ndio kumenishindaa"niliumia sana nikaja kujua ukweli juu ya taarifa ambayo rafiki yangu alinipa lakini nilipitia wakati mgumu sana ila kwa kuwa nilikua nipo depo hisia zilikata na nikawa nipo kimyaaa


Baadae nipo chuo sasa naendelea na masomo yangu siku nilipata sms habari yako

Wakati huo nilipata taarifa kuwa ex wako tayari mjamzito jamaa kaishamjaza na life Lao NI la kawaidaa na mwanaume kabadilishwa kituo cha kazi kutoa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine
Basi nilienda kipindi cha DINI na nilitoka nikapiga namba Ile kumbe alikuwa ex wangu akapokea simu kwa kuanza kuomba misamaha mkubwa sana Mimi nilishakusamehe ila naomba utambue KUWA wewe ni mkewa mtu akanijibu kuwa ndio ila nimekwama sana hivyoo naomba unisaidie kama utaweza hela kama laki moja kwa kuwa nipo nasoma na Nina shughuli zangu zingine za kibiashara hapa mjini nikaona sio mbaya nilimpa akanishukuru sana

Kuanzia pale nilibadili line ila alinitafuta tena akiwa na mimba ya miezi saba kuwa anaomba hela ya mana ameambiwa aende hospital kubwa mana ndio mimba ya kwanza kwa check up zaidi mana anaumwa mara kwa mara nilimsaidia ila sikupendakuwasiliana naye mana mkewa mtu

Kuanzia mwezi uliopita kaachana na bean yake na karudi kwao sasa hapo simu kila siku kwangu na kaisha tuma watu wamsaidie kuomba msamaha kwangu anataka kurudiana na Mimi naomba ushauri wenu wadau wa jf kwa kijana mwenzenu
Chuo gani kinafundisha watu kuandika bila vituo?Labda umechanganyikiwa mkuu kwa kuombwa msamaha.Nauliza tu,je mimba itakuwaje?au anataka umlelee mwanaume mwenzio mtoto?msamehe mkuu,mrudie kama anavyokuomba lakini akijifungua tu mtoto ampeleke alipomtoa abaki peke yake umuoe!
 
Chuo gani kinafundisha watu kuandika bila vituo?Labda umechanganyikiwa mkuu kwa kuombwa msamaha.Nauliza tu,je mimba itakuwaje?au anataka umlelee mwanaume mwenzio mtoto?msamehe mkuu,mrudie kama anavyokuomba lakini akijifungua tu mtoto ampeleke alipomtoa abaki peke yake umuoe!

Tayari kaishajifungua Mkuu
 
Umefika form six na jeshini umeenda halafu unashindwa kufanya maamuzi? Bado unampenda wewe
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Umefika form six na jeshini umeenda halafu unashindwa kufanya maamuzi? Bado unampenda wewe

Kwani Mkuu hujawahi kuona professor au PhD holder kwenye suala la love napo wanahitaji ushauri
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mapenzi balaa hili jambo unaliombea ushauuri plz nadhan basi kuna kitu naww una hatia nacho umetuficha coz kwa hali ya kawaida hili si la kujadili ni kuachana nae
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mapenzi balaa hili jambo unaliombea ushauuri plz nadhan basi kuna kitu naww una hatia nacho umetuficha coz kwa hali ya kawaida hili si la kujadili ni kuachana nae

Naficha nn Mkuu SI nimeweka wazi kwambaa
Sina hisia kwa sasa ila yeye ndio kanigandaa
Kwaio nipo hapa kuchukua ushauri
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuanzia pale nilibadili
line ila alinitafuta tena
akiwa na mimba ya
miezi saba kuwa
anaomba....

pumbavu sisi sio rika lako ulibadil laini afu akakupataje?? acha kutubebea akili
 
Duuu bob unazingua kinoma kwaiyo unaomba ushauri gani sasa jombaa wanawake hapa Dar wako kibao nawe unaumiza kichwa kwaajili ua mtu aliekutia Dore wee vipi chalii angu Mwache aende....
 
Yaani unaomba ushauri kwene kitu ambacho hata mtoto mdogo anatatua mwenyewe hivi hata shule uliyosomea inaitwaje ambayo hawezi kutengezea wanafunzi wake akili yakujiongeza
 
Hisia kwake sina kabisa ila yeye kanigandaa
Kama mwanaume kamili kuwa na msimamo brother. Na huyo dem inaonekana hana msimamo na pia aliolewa na ana mtoto juu, mashaka yangu anachotafuta kwako ni kumtunza mtoto... na mtoto akishakua lazima akuteme tena. Nakwambia hivyo maana mm yalishanikuta kama yako.
 
Kama mwanaume kamili kuwa na msimamo brother. Na huyo dem inaonekana hana msimamo na pia aliolewa na ana mtoto juu, mashaka yangu anachotafuta kwako ni kumtunza mtoto... na mtoto akishakua lazima akuteme tena. Nakwambia hivyo maana mm yalishanikuta kama yako.
Yalikukuta kivipi Mkuu hebu fungukaaa nielewe Mkuu au njoo PM

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom