USHAURI KWA DARASSA

baro

JF-Expert Member
May 12, 2014
2,500
2,000
Nawasalim , wana bodi hasa katika hili jukwaa la celebrities,

Ni muda mrefu toka niache kufatilia muziki huu wa kibongo hii ni kutokana na kukosa mashairi yenye kuvuta hisia kwa jamii ,Mara ya mwisho ilikuwa namsikiliza Roma Mkatoliki na Nyimbo zake zikizokuwa na harakati za kimapinduzi hasa katika kuikumbusha serikali ,


Kwa sasa ,nimerudishwa na huyu msanii anayejiita "DARASSA" hakika ni mpuuzi tu ambaye atashindwa kumkubali jamaa katika nyimbo zake hasa huu wimbo wake wa taifa , uitwao *Muziki* hakika anahitaji pongezi kuanzia kwa Maproduza, Muimba Kiitikio ( Ben Pol) na yeye mwenyewe darasa ,bila kumsahau , Muongozaji na Mtengenezaji wa vidio ( Hansacana) kwa produza kufanya kweli na kuthibitisha kuwa wanaokimbilia Africa kusini ni wapuuzi na malimbukeni kwani hata wao wabongo wanaweza


DARASSA , hii kwake ni Neema na nyota kukubalika kwa nyimbo zake ,
Ili aendelee kuwika kimafanikio na kwenda tofauti na wanaolewa mafanikio hasa wasanii wa hip hop , afanye yafuatayo;

1. Aunde Management Team ya Skilled and Professional people , ambao watamsaidia kuandaa strategic plan ya muziki wake na soko lake ndani na nje ya nchi

2. Akodi jengo liwe kama ofisi , ambapo ataratibu shughuli zake zote na kuajili vijana kadhaa watakaohusika katika mitandao ya kijamii kufungua na kuongoza akaunti zake mbalimbali kwa weredi mkubwa na kuwa wanatoa updates za kila jambo analofanya au analotaka kufanya


3. Akubali muziki ni biashara nzuri hvyo asisite kushirikiana na wasanii waliofanikiwa kama diamond katika kusaka fursa nje ya nchi na collabo na wasanii wakubwa wa nje , ni ukweli usiopingika diamond ana network kubwa kwa nje

4. Ajitambue kuwa sasa yeye ndio kioo kwa muziki wa hip hop nchini ,hvyo inabidi atumie fursa hii kufanya watu wa kada mbalimbali waupende na wauheshim kama ilivyo kwa kina Jay Z, Nas scoba, P diddy ,n.k


5. Tabia za kuvuta bangi, madawa ya kulevya , pombe hivi hurudisha nyuma maendeleo na kupoteza katika game , ajifunze kwa Mr nice , 20% , chid Benz, Daz Baba, Feruzi n.k

Mwisho , ila si kwa muhimu , bahati haiji Mara 2, cha msingi chukua ushauri wangu kama umo humu ,ama washabiki wako au wapenzi wako walioko humu , kukuona unafanikiwa zaidi ndio furaha yetu si wapenda hip hop ,

Kumbuka , "Usivute sigara ukaja choma kibanda"

*Acha maneno weka Muziki*
Sasa acha Maneno piga muziki biashara ,ukichelewa utakuja kubebwa mgongoni kama mtoto mdogo

Asante
 

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,403
2,000
Usimuoverrate kihivyo, kuajiri watu wote hao kwa kipato gani? Tatizo mnataka kumfananisha kila msanii anayewika na Diamond, huyo Diamond hadi kufikia hatua ya kuwa na ofisi na kuajiri watu wengi haikuwa rahisi namna hiyo, Darasa na kuhit kote anapiga show ya mil 4, wakati Diamond kaanza kudai show ya mil 10 miaka mi5 iliyopita, kwa dau hilo atawezaje kuyafanya hayo?Halafu usiseme ndio kioo cha Hiphop wakati wimbo wa 'muziki' sio Hiphop
 

baro

JF-Expert Member
May 12, 2014
2,500
2,000
Usimuoverrate kihivyo, kuajiri watu wote hao kwa kipato gani? Tatizo mnataka kumfananisha kila msanii anayewika na Diamond, huyo Diamond hadi kufikia hatua ya kuwa na ofisi na kuajiri watu wengi haikuwa rahisi namna hiyo, Darasa na kuhit kote anapiga show ya mil 4, wakati Diamond kaanza kudai show ya mil 10 miaka mi5 iliyopita, kwa dau hilo atawezaje kuyafanya hayo?Halafu usiseme ndio kioo cha Hiphop wakati wimbo wa 'muziki' sio Hiphop
Nafikiri unashindwa kuelewa , nguvu ya wimbo mmoja inawrza badili kila kitu

Punguza roho ya korosho
 

Papizo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
4,686
2,000
Huyo Diamond mwenyewe amefunikwa sasa hivi fanya mchezo nini.....nani anashika number mojadiamond au Darasa??mzee wa sio mamba wala tembo bra bra sitaki kusikia amewafunika ile mbayaaa mpaka domo....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom