Kwa mazingira ya sasa chini ya utawala wa rais Magufuli, kufanya uchaguzi bila kwanza kuhakikisha kuna Tume Huru ya Uchaguzi ni kukipoteza chama mlichokijenga kwa damu.
Kama hamkujifunza kwenye chaguzi ndogo za marudio na uchaguzi wa Serikali za Mitaa basi mtakuwa ni ma tabulalasa na hamtapata mwalimu mwingine wa kuwafundisha labda aje malaika.
Nimemsikia Tundu Lissu akitangaza kugombea Urais, sawa ni haki yake, lakini bila kuhakikisha uwepo wa tume huru, namsikitikia anaweza kuongeza machungu ya risasi yaliyoanza kupona, kwa vile hakuna Mkurugenzi yeyote wa Halmashauri wala msimamizi wa NEC aliye tayari kupoteza kazi yake kwa kumtangaza mpinzani kashinda.
Pamoja na ukweli kwamba CCM ina hali ngumu kisiasa ndani na nje ya chama, lkn kwao uchaguzi huu ni wa kufa na kupona, wanajua jinsi mgombea wao alivyopita kwa shida uchaguzi uliopita, wanajua fika wananchi walivyo na hali mbaya kimaisha, wanajua katiba inavyosiginwa, jinsi utawala wa sheria unavyopindwa, unyanyasaji, utekaji na jinsi uchumi ulivyoyumba.
Endapo mtaingia bila Tume Huru, nawahakikishia mkipata wabunge 5 na madiwani 50 nchi nzima, basi mkatambike na kujifukiza.
Ni hiyari yenu kusuka au kunyoa, muingie kwenye uchaguzi mbaki chama kisicho na mbunge hata mmoja au mpiganie kwanza Tume Huru.
Sabato njema watu wa Mungu.