Uchaguzi 2020 Ushauri kwa CHADEMA, kuna vitu tuachane navyo. Tujikite na kuwatumikia Wananchi, Uongo hauwezi kutusaidia

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,190
27,237
Habari wanajf, leo kuna jambo moja ambalo nimeona nilizungumzie ili tuweze kukaa sawa na kuweza kushinda mapambano yetu yanayokuja.

Ninaamini kuwa hadi sasa CHADEMA ila ilani nzuri sana ambayo ikitekelezwa italeta manufaa kwa nchi na wananchi kwa ujumla.

Nguvu kubwa tuiweke hapa kwa maana ndio utakuwepo utofauti kati ya Chama tawala na chadema.

Kama tunavyojua mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na tupo kwenye kampeni kipindi hiki, yes propaganda chafu inaweza kuwa moja ya silaha kubwa kuweza kushinda lakini hizi propaganda chafu ziwe zinakaribiana na ukweli.

Nimejaribu kufikiria mara mbilimbili aina ya maneno/tweets anazotoa mgombea wetu nabaki kukosa majibu na kuhisi pengine chama hakijaweza kukaa naye au kumsaidia kufanya hizi propaganda.

Mgombea uraisi wetu ambae tunahitaji kuwa mbadala wa chama tawala anatakiwa kuwa smart mara mbili kuliko aliyepo madarakani ili uhalali wa yeye kumuondoa uwepo.

Ni lazima kujitofautisha, kama wa chama tawala anafanya mabaya, basi wa kwetu afanye mazuri wananchi wawe na imani nae.

Wapiga kura wapo wa ina nyingi, pia kuna kundi kubwa la wasomi ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuchambua yupi ni sahihi na yupi sio. Hapa nazungumzia wale ambao hawana ushabiki.

Tweets za mgombea wetu zinafikirisha sana, unawezaje kutweet jambo ambalo wewe mwenyewe hauna uhakika nalo?

Hebu fikiria siku kadhaa nyuma wakati anahojiwa juu ya kufungiwa kwake alisema mgombea wa CCM anaenda mapumziko ya siku 8 (jambo ambalo sio kweli) na akasema ataanza kampeni tarehe 12(jambo ambalo sio kweli).

Haya maneno mgombea wetu anatakiea kuachana nayo kwa kuwa yanaondoa credibility yake. Haya maneno ni ya kuokoteza mitandaoni wanatakiwa wabaki nayo mashabiki tu wala yasifike kwa mgombea uraisi na kuyazungumza.

Leo mgombea wetu ametweet kuwa wafanyabiashara kariakoo wanalazimishwa kufunga biashaea kwenda uwanjani kwenye kampeni za ccm. Anasema hivi akijua kabisa kuwa ni uongo, watu wapo kkoo na wanaona anayosema, mwisho wa siku nao wanabaki wanajiuliza ni kariakoo ipi hiyo?

Hakuna mfanyabiashara kariakoo anaelazimishwa kwenda uwanjani na haiwezekani, kinachofanyika ni gari ya matangazo kupita na kuwatangazia watu kuwa kuna mkutano uwanja wa taifa ,sasa kwenda au kutokwenda inabaki kuwa uamuzi wako.

Hizi propaganda ashauriwe zibaki kuwa kwa mashabiki tu na sio kwa level yake.

Chadema tujisahihishe hapa, tumsadie na mgombea wetu nae ajisahihishe.

IMG_20201009_114140.jpg
IMG_20201009_114122.jpg
 
CHADEMA haina Sera mbadala za maendeleo ila kuwaghiribu wapiga kuwa ati "sasa ni saa ya ukombozi".

Sera mbadala ya maendeleo ya watu ielezwe vizuri kwa kutumia mifano ya maendeleo ya vitu yaliyofanywa na Serikali ya CCM kama hayakisi maendeleo ya watu kwa maana ya ustawi wao. Isiwe tu kuyabeza ila pia Lissu aeleza akipewa ridhaa atawafikisha wapi Watanzania kimaendeleo, na kwa jinsi gani. Hili la kuweka rehani maliasili ya nchi ni usaliti na uhaini.

CHADEMA haina mwandaaji wa kampeni kama Polepole

CHADEMA haina viongozi mfano wa Mama Samia au Majaliwa, ambao wanakubalika katika jamii kwa kila jambo na matendo yao.

Kinachoendelea Uwanja wa Mkapa Dsm muda huu ni ushahidi kuwa CCM haina chama mshindani. Kupuuza nguvu ya wasanii ni upumbavu na ulofa uliokubuhu
 
Kama wanalazimisha shule zifungwe na watumishi waache maofisi wazi waende kwenye kampeni zao,hilo la kulazimisha wafanyabiashara ndio litawashinda?
 
Ras Simba anakula kodi zetu bure ni wakati wamuachie aende uraiani siyo Kushinda shinda ikulu
 
Sio kwelo, na pia hili jambo lilipaswa kufanywa na washabiki tu huku mitandaonj.
Kama wanalazimisha shule zifungwe na watumishi waache maofisi wazi waende kwenye kampeni zao,hilo la kulazimisha wafanyabiashara ndio litawashinda?
 
Shida kubwa iliyopo chadema ni washabiki wa huku mitandaoni
Walitaka wawafungie watu uwanja wa Taifa ili hata baada ya burudani ya Fiesta kuisha washindwe kutoka ili huyu jiwe aweze kuwahadaa na hayo makalavati anayoyaita flyover lakini watu wameshtuka wamesema hawaendi
 
Watumishi wote na familia zao kura kwa lissu.Mmeteswa sana miaka 5 bila ongezeko la mshahara,kupanda madaraja,increments,malimbikizo n.k.

Mpigie lissu kura ubarikiwe pia.
 
Waache Wajazane Upepo Hawata pata hata 20%
Watapigwa pigo kubwa
Nabado
 
Back
Top Bottom