Kwa hali ninayoiona huku Mitaani CCM inabidi mjipange kuanzia sasa. Yale mapenzi waliyokuwa nayo Wananchi wakati awamu ya Tano ikiingia madarakani naona kama yanapungua kwa kasi sana. Nitoe mifano michache tu.
- Sasa hivi wananchi wanasumbuliwa sana na masuala ya kodi kwa sababu ya dhana kuwa lazima kodi ikusanywe.
- Mzunguko wa fedha ni kidogo sana. Mzunguko wa fedha unaonekana pale Serikali inapoleta fedha kwenye ngazi za chini. Hizi fedha zikiletwa kutekeleza miradi hutawanyika na hata muuza nyanya anaipata.
- Huku kwenye Halmashauri wako hoi bin tabaan. Hakuna fedha inayoteremshwa huku chini na hakuna kazi inayofanyika. Mfano kuwatembelea wakulima,kutembelea shule, kutoa ushauri wa kitalaam huko viijini
- Migogoro ya kila mara na vyama vya Upinzani. Ni busara kukaa nao meza moja na kujadiliana nao. Usiwadharau wapinzani nao wana watu wengi nyuma yao. Bila kuficha Rais wetu anafanya kazi nzuri sana. Mfano moja tu. Hivi sasa tatizo la umeme ni kama limekuwa jambo la kihistoria, lakini anatakiwa kukaa na Wapinzani ili awasikilize.
- CCM mjiangalie sana 2020 siyo mbali.