Ushauri kwa CCM: Mwondoeni Lowassa kwa Mdahalo

Ushauri kwa CCM: Mwondoeni Lowassa kwa Mdahalo

CCM wanamuogopa Lowassa

...hakuna ANAYEMWOGOPA. hofu hii mnaileta nyie! Lowasa nje ya marafiki hana hoja. Hana jipya. Kila kitu kinaandaliwa na kina Abuu...Kaa..Liwongo. Lowassa anatafuniwa kama mtoto. Hana meno ya kudadavua hoja.
Fedha zake zinafanya kazi yote hii, ni maigizo tu. Kumbuka ana shahada ya tamthilia na sanaa za maonesho ya UDSM.
1. Alianza na kutengeneza Mashehe, akawaita wa Bagamoyo. Ikaonekana ni FEKI! Walikanusha. Akakaa kimya!
2. Katengeneza wachungaji na wainjilisti.
3. Akatengeneza KUPENDWA na wapanda bodaboda wa Rujewa. Ilionekana kuwa Pikipiki alizinunua mwenyewe. akazisafirisha kwa malori mpaka nje ya Dodoma. Akakodi waendeshaji, kisha kuwaita eti wametoka Mbeya.
4. Hata kilichotokea Arusha, ni mwendelezo wa tamthilia hii ambayo inalenga kuudanganya umma kuwa ANAPENDWA! kila aliyeuwa pale ALILIPWA, alisafirishwa hadi Arusha.
5. Njia pekee ya kupima credibility yake ni kumwacha AJISIMAIE mwenyewe kwa hoja katika midahalo. PERIOD!
 
  • Thanks
Reactions: M2.
uongozi hauhitaji maongezi wala mijadala bali unahitaji mipango na watu(team) ya kufanikisha malengo ya msingi
 
Hakuna haja ya kusubiri vikao, Lowasa ni kumfyekea mbali na genge lake. Hafai, ila hajui kuwa hafai. Ukitaka nchi ikabidhiwe kwa majambazi ndo sasa. We ona wezi wote wanaanza kurudi karibu. Rostam alishapotea, Karamagi, na watuhumiwa wote wa Richmond. Ngoja apewe, tutaona baada ya miaka miwili tutakuwa wapi.
Ogopa mtu asiye na uchungu na Nchi na wananchi wake. Ogopa mtu anayejali maslahi yake tu hata kama yanagharimu maisha ya wengine. Hilo ndo kauli mbiu ya magenge yote ya mafisadi.
 
Bado watu wana fikra zile za kizamani enzi za mafashist.
Mafashist walikua ni mahiri wa kuongea ili waungwe mkono kwenye udikteta wao.
Lowasa ameeleza wazi kuwa anataka kufanya mambo kwa vitendo.

Unasahau kuwa kuna tofauti ya kilafudhi kwa makabila ya Tanzania .Tofauti hiyo inaathiri makabila hayo hata wakati wa kuongea kiswahili. Makabila mengine kama ya watu wa Pwani yanauwezo wa kupangilia maneno ya kiswahili.

Hata hivyo hakuna uhusiano wowote kati ya mbwembwe za majukwaani na utendaji wenye tija ya kuleta
aendeleo .

Ingekua maneno mengi ndio mipango bila shaka Ukanda wa Pwani ungekua na maendeleo makubwa.

Watanzania debate sasa timezichoka sana.
Tumewaachia wanafunzi wa sekondari. Tunataka mtu mwenye uwezo wa kubadili changamoto kuwa fursa. Sio mtu wa kulalamika.

Kuna hatari kubwa sana kuwanyima watanzania mtu wanayempenda. Waongoza debate hawawezi kubuni vimaswali vyao eti ndio kigezo cha kutuchagulia Rais.

Lowasa hajaanza kutajwa kwenye midomo ya watanzania leo au jana. Ndio maana hata wale walotaka kuzima nyota yake kwa kuwadanganya watanzania kwa muda wote wa miaka 8 na kusambaza nyimbo kila kona kuwa Lowasa ndiye anayepita kila idara kuiba na kufuja pesa na mali za umma, wameshindwa kuwatenganisha watanzania na Lowasa.
Hiyo ndio njia pekee ya kumwondoa Lowasa kwenye hard talk
 
...hakuna ANAYEMWOGOPA. hofu hii mnaileta nyie! Lowasa nje ya marafiki hana hoja. Hana jipya. Kila kitu kinaandaliwa na kina Abuu...Kaa..Liwongo. Lowassa anatafuniwa kama mtoto. Hana meno ya kudadavua hoja.
Fedha zake zinafanya kazi yote hii, ni maigizo tu. Kumbuka ana shahada ya tamthilia na sanaa za maonesho ya UDSM.
1. Alianza na kutengeneza Mashehe, akawaita wa Bagamoyo. Ikaonekana ni FEKI! Walikanusha. Akakaa kimya!
2. Katengeneza wachungaji na wainjilisti.
3. Akatengeneza KUPENDWA na wapanda bodaboda wa Rujewa. Ilionekana kuwa Pikipiki alizinunua mwenyewe. akazisafirisha kwa malori mpaka nje ya Dodoma. Akakodi waendeshaji, kisha kuwaita eti wametoka Mbeya.
4. Hata kilichotokea Arusha, ni mwendelezo wa tamthilia hii ambayo inalenga kuudanganya umma kuwa ANAPENDWA! kila aliyeuwa pale ALILIPWA, alisafirishwa hadi Arusha.
5. Njia pekee ya kupima credibility yake ni kumwacha AJISIMAIE mwenyewe kwa hoja katika midahalo. PERIOD!

Huo uwezo wake wa kutengeneza image yake ndo unawatisha
 
Back
Top Bottom