Ushauri kwa BAKWATA

Ushauri kwa BAKWATA

dini yetu inatutaka kusoma quran na kuiweka kichwani na kuwalazimisha watoto wetu kufanya hivyo kwani Mwenyezi Mungu alishajua kuwa zama za mwisho vitabu vitavamiwa, watu watabadilisha baadhi ya aya as quran kwa manufaa Yao binafsi, hapo kama quran haipo kichwani utaweza kubabaika lkn kama ulibahatika kuisoma na kuihifadhi kichwani huwezi kubabaika. Na Allah anajua zaidi
wale wenye Faraqi, matalasimu, halubadili na makombe walisoma nini? Kabla ya kufa kuna maisha, vijana wa kiislam wanaadhirika kwa kusosa ajira kutokana na ukosefu wa elimu. Ukienda pale msikitini hata sadaka haitoki na kama ikitoka basi ni sh. 50, 100, 200, 500 tu ambazo hazitoshi kumlipa Imam na matumizi ya msikiti, hawawezi kuchangishana kujenga msikiti ila kwa kuwanategemea wafadhiri wenye rangi zilezile kila siku, hii yote ni kutokana na ukosefu wa kipato. Ninamsifu sana Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa kuwahimiza waislamu wasome zaidi pia elimu ya circular ingawa baadhi yao wanampiga vibao hadharani anapowaambia mambo yanayotokana na kusoma elimu ile ya Uchina aliyoiagiza Bw. Mtume isomwe. Mtume alijua kuwa iko siku jamii itakubwa na maradhi kama UKIMWI ambayo yatahitaji elimu ya Wachina. Hebu ona vijana wa kiislam waliokwenda kuswali lakini bado wanaiba misikitini viatu vizuri vya waumini wenzao wanaoswali wakati wa ibada. Kama ukiangalia viatu vya waumini vilivyovuliwa pale mlangoni msikitini wakati wa kuswali utagundua kuwa hawa waliokondani humo msikitini ni maskini sana, ndala na yeboyebo zilizochoka sana, na wale wenye viatu vizuri inawalazimu kuviingiza msikitini ili visiibiwe. Waumini wamevaa nguo za mitumba zilizokuwa zinavaliwa na wagalatia (wazungu) kutoka ulaya. Hivi vyote ni viashiria vya umaskini ambavyo BAKWATA yetu lazima ijione kuwa ina dhima ya kuwafanyia mageuzi waislamu kuhusu elimu na kazi nyingine za kuinua kipato chao, maana watu wenye kipato hata sadaka na zaka watatoa nyingi kiasi cha kuweza kugharamia kuwatuza masheikh wao, kuwalipa walimu wa madrasa na kuwatunzi mayatima vizuri, hivyo kuupeleka mbele uislamu. Wakristo wao wanatoa sadaka na zaka kubwa makanisani hivyo wanamudu kuwatunza wachungaji wao vizuri, sisi tunategemea nyama ya ngamia na tende ziletwe kutoka kulekule. Waislam tusisubiri tukosolewe na watu wengine ili tuwashikie majambia tuwapige, tujisahihishe sisi wenyewe kwa wenyewe ndani kwa ndani. Aliempiga kibao Mzee Mwingi alikosea sana, kwani Bw. Mtume aliposema itafuteni elimu hata mbali na uarabuni ilimaanisha kuje kuwe na watu wa kuyasema kama yale aliyoyasema Mzee Mwinyi kwa waislamu pale siku ile. Mafundisho gani hayo yanayoruhusu kumzaba mzee kama Ali Hassani Mwinyi kama sio laana na bangi
 
naona Leo mmeamua kututukana ! inabidi uulize kwanza ilikuaje ?? halaf ndio ufanye utafiti sawa bwana Mdogo
 
natafuta sponsor nimechaguliwa bachelor of pharmacy ila nmekosa mkopo nimesoma mada hii imenigusa sana mm ni miongoni mwa wahusika na walengwa wa moja kwa moja wa hii mada wazaz wetu wengi hali duni sana tunajitahid kuvuka lakn vikwazo ni vingi tunatambua jins din yetu ilipofika mungu atutie nguvu inshaallah
kwa ambaye amafaham taasis za kiislam zinazotoa ufadhili hata pia mikopo ya kielim anifahamishe kwan naona giza mbele yang nikishindwa kupata hii digrii bas nitauvaa mtaa bila pa kuanzia kuna muda nalia nikikaa peke yang nikiangalia familia yang daah rabbi mola wetu turuzuku vya halal tupe njia tuish ili kesho tuione pepo yako.nn
 
naona Leo mmeamua kututukana ! inabidi uulize kwanza ilikuaje ?? halaf ndio ufanye utafiti sawa bwana Mdogo
natafuta sponsor nimechaguliwa bachelor of pharmacy ila nmekosa mkopo nimesoma mada hii imenigusa sana mm ni miongoni mwa wahusika na walengwa wa moja kwa moja wa hii mada wazaz wetu wengi hali duni sana tunajitahid kuvuka lakn vikwazo ni vingi tunatambua jins din yetu ilipofika mungu atutie nguvu inshaallah
kwa ambaye amafaham taasis za kiislam zinazotoa ufadhili hata pia mikopo ya kielim anifahamishe kwan naona giza mbele yang nikishindwa kupata hii digrii bas nitauvaa mtaa bila pa kuanzia kuna muda nalia nikikaa peke yang nikiangalia familia yang daah rabbi mola wetu turuzuku vya halal tupe njia tuish ili kesho tuione pepo yako.nn
Dah... machozi yamenilenga kuusoma utenzi wako huu.... Yarabi mfanyie wepesi mja wako huyu ili atimize wosia wa Bw. Mtume kwa waislam wa kuitafuta sana elimu ya wachina. Mimi binafsi niko tayari kukuchangia ili ulifanikishe hili, nina imani nikifanya hivyo nitaipata radhi ya Bw. Mtume S.A.W kwa kukuwezesha kuitafuta elimu ya Wachina.
 
Hawa watu wakishauriwa vizuri ni wabishi halafu huko mbele ys safari wanaanza kulalamika kuwa wanatengwa! Kwani ukifundisha pia Taaluma kama vile hesabu, sayansi nk huko kwenye madrasa ni haramu!
Ninachokiona hapa ni kuwa waalimu wengi wa madrasa hawana kabisa Taaluma nyingine! Wapigeni chini muajiri vijana wasomi watakaofundisha Taaluma nyingine pia! Tunawatakia MEMA ili huko mbeleni watu wa kulia lia kama shehe Khalifa wasiwepo!
 
Mkuu kavulata sikutegemea kama utakuwa empty kiasi hiki ...Nani kakudanganya kuwa mtu akisoma sana Quran bila secular atakuwa mtengeza majini !! daa kumbe uko empty kiasi hiki je vipi kuhusu wachungaji niambie Kazi anayofanya kadinali pengo zaidi uchungaji? mi naona umeamua kutukana waislamu ila unaogopa kuongea moja kwa moja ...hivi unajua kuwa shule za fedha Ni zakiislamu?
SHULE za feza ni za waislam lakini siyo wa bongo ni wa uturuki! Na Uzi umelenga wabongo! Hata hivyo SHULE za feza siyo madrasa wala siyo seminari! Na ni mbili tu miongoni mwa nyingi kwa upande was pili!
 
Back
Top Bottom