Ushauri kwa BAKWATA

Ushauri kwa BAKWATA

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Dunia imegeuka geukieni elimu dunia kwa watoto wenu wa Kiislam kwa vitendo. Geuzeni madrasa zenu kuwa vituo vya elimu ambako watoto wanafunzwa masomo ya dini, hesabu, english, sayansi, historia, na ufundi badala ya kulazimisha watoto wenu wakariri (wahifadhi) Quran pekee wakiwa wadogo sana umri uleule ambao watoto wengine wako bize na kujifunza A B C D na 1, 2, 3,.... Umri mdogo ni muhimu sana kwa watoto kuhamasika kujifunza kitu chochote.

Nimefanya utafiti wangu mdogo kwa watoto wa kiislamu nikagundua kuwa wale wanaoimba taarab, muziki, wakata mkaa, wamachinga, na walinzi wa usiku wengi wao wamepitia madrasa hizi lakini wamekosa elimu, ajira rasmi na mitaji ya kufanya biashara kama wale wenzao waliopitia madrasa pia lakini wana asili ya Asia kama vile waarabu, wahindi, wapemba, nk.

Hii ina maana kuwa elimu ya madrasa haitoi ajira, ujuzi wala mitaji ya biashara kwa watoto wanapokuwa watu wazima hasa kwa watoto ambao hawana asili ya Asia. Yaani waislamu weusi wengi wao wanakosa elimu, ujuzi na mitaji ya biashara wanapofikia umri wa kujitegemea na matokeo yake watanyakazi yoyote bila kujali elimu ya dini waliyoipigania na kuihifadhi vifuani walipokuwa watoto kwenye madrasa hizi.

Hii ni tofauti kabisa na watoto wa kiislamu wenye asili ya Asia ambao watakuwa na elimu ya dini na ujuzi na mitaji ya kufanya biashara. Wengi wao weusi wenye elimu kubwa ya kidini wanaishia kugombania uimamu misikitini na kutupiana majini, kuwa waganga wa kienyeji na wapiga ramli na makafara ili kujipatia riziki.

Wazazi wa Watoto wa kiislamu weusi (Waafrika) lazima wawe makini sana kwenye elimu za watoto wao wakiwa wadogo, maana samaki anakunjwa akiwa mdogo, wapeni watoto elimu zote za dini na dunia kwa wakati mmoja utotoni ili kuwapunguzia adha ya kuwa wazindikizaji wa wenzao kwenye maisha watakapokuwa wakubwa, maana elimu ya dini haitoi ajira ya kutosha kwa vijana wengi.
 
So, tatizo sio madrassa, ni mitaji?

Haya, wito kwenu wazazi mnaowapeleka watoto madrasa, tafuteni na mitaji ili muwawezeshe watoto wenu wawe kama watoto wa Asia huko!

UDINI!
 
hawaajiriki kwa kukosa elimu na ujuzi na wala hawana mitaji na ujuzi wa biashara, shiida, wale wenzao wanapeta tu kwenye mayadi ya magari, shida iko kwa wamatumbi
 
Enzi za nyuma waislamu wengi walikuwa discouraged kusoma, kutokana na walipoenda kujiandikisha huko walilazimishwa kutumia majina ya kikatoliki (athari za baada ya ukoloni wa muzungu).. Mifano ipo mingi, muathirika mmojawapo akiwemo W/Mkuu wetu mstaafu wa JMT mzee Cleopa Msuya.

Hata hivyo, kusema hayo kwa sasa ni weak arguments. Zama hizi haya mambo ya watoto kusoma ni kwa wote.. Hakuna mzazi asiyempeleka mwanae shule na kumhimiza kwenda madrassa.. Sio kweli, nimekataa!
 
Una laana sio bure,utafiti ucjifanyie wewe mwenye kichaa utawafanyia waislam Nyumbu kwelikweli
sijui alahu yaalam, lakini nahisi wewe ni muislam mwenye light skin na nywele za maboya sio za kipilipili. Wale wenye nywele zinazouma zikichanwa kama mimi wameshanielewa nilichosema na kumaanisha. Baada ya kumalizika swala wale wamatumbi huwa wanatawanyika na nyie wenzetu wenye ngozi zenye nuru kidogo mnabaki nyuma kupeana khabari za namna ya kupiga madili, kugawana pesa za kufungulia biashara na khabari nyingine kuhusu maisha hapa mjini. Wengine ndugu zao wako Oman, Abudhabi Wale wenzangu kama mimi ninawahusia na kujihusia nafsi yangu tuwasomeshe watoto wetu ilmu hata ikibidi Uchina ili tupate kipato kitakachotuwezesha nasisi tupate wepesi kwenye utafuti wa riski na kutimiza ile nguzo ya tano ya Uislamu ya kwenda Mecca kuhiji, Vinginevyo tutakuwa wazindikizaji wa wenzetu ndani ya misikiti.
 
Enzi za nyuma waislamu wengi walikuwa discouraged kusoma, kutokana na walipoenda kujiandikisha huko walilazimishwa kutumia majina ya kikatoliki (athari za baada ya ukoloni wa muzungu).. Mifano ipo mingi, muathirika mmojawapo akiwemo W/Mkuu wetu mstaafu wa JMT mzee Cleopa Msuya.

Hata hivyo, kusema hayo kwa sasa ni weak arguments. Zama hizi haya mambo ya watoto kusoma ni kwa wote.. Hakuna mzazi asiyempeleka mwanae shule na kumhimiza kwenda madrassa.. Sio kweli, nimekataa!
"vicious circle" aliyepata elimu huko nyuma anajua utamu wa elimu, nirahisi kuhakikisha kuwa na mwanawe anakwenda shule. Vilevile mtu mwenye elimu atapata ajira na mshahara wa kumudu kumlipia mtoto wake ada na michango mingine ya shule, lakini mtoto wa mpika vitumbua ataomba mtoto wake afeli mtihani ili ada isije kuwa kero kwake, mtoto wa mfanyabiashara atamrithisha mtoto wake ujuzi na mtaji wa kufanya biashara, je mtoto wa maskini atakuwaje? Sasa pitapita huko maofisini na makazini ili ujionee ni akina nani wana ajira za nguvu za kupata mishahara, pitapita huko kariakoo, shaurimoyo na kwenye mayadi ya magari ili uone ni akina nani wana mabiashara makubwa kisha rudi nyumbani kwako ukatafakari. Mtoto wa maskini atakuwa Rais, engineer, daktari, nesi, mkuu wa mkoa, waziri au meneja kama tu utampatia elimu dunia. Bila elimu hii mtoto wa masikini mweusi Tanzania atakuwa taabuni nakuishia kuwa mganga wa kienyeji hata kama amehifadhi juzu 30 kifuani mwake. Lengu langu hapa sio uchochezi au kuchonganisha wala kubeza kundi la watu, bali kukuonyesha kuwa elimu ya dunia ni muhimu pia itolewe sambamba na elimu ahera, na muda wa kuyafanya haya yoote ni umri uleule wa utotoni, badala ya kuwalaza macho usiku kucha watoto wetu kwenye maulid wakipiga madufu tuwaache wakalale mapema na kujiandaa kwenda shule kesho na badala ya kuhifadhi quran kifuani tu wahifadhi pia sayansi na hesabu kichwani.
 
Sijui unaongelea zama zipi? Hivi hao wachoma vitumbua wote ni waislamu? Na kuhusu sherehe za kidini, kuna mikesha mingapi kwa upande wa pili au unaiona kwa waislamu tu?

Ukizungumzia maskini nchi hii, hutaji kundi fulani la dini tu, zaidi ya 70% ya Watz bila kujali itikadi zao na maeneo watokayo ni masikini, hivyo kama kigezo cha 'umasikini' ni sababu ya watoto kutokupelekwa shule basi usibague wala kuchagua, kapu ni moja.

Wewe unaona 'ubaya' tu kwenye hizo mambo za waislamu na huamini kama kuna jema lolote, ndio maana unahitimisha unavyohitimisha. Sasa kama ndivyo, hapo sina cha kukusaidia.

Kwa ufupi, unachokisema hakiakisi uhalisia.. Au labda unajadili kwa muktadha wa Dar na Pwani tu? Hebu nenda Shinyanga, Musoma, Kagera, Mara na vijiji vinginevyo visivyo ukanda wa Pwani halafu useme watoto wote wa maskini wanaenda 'madrassa' ndio maana wanakosa elimu dunia..

Nachelea hili likiishiwa hoja, mtahamia kwenye misikiti. Mtataka watu wasifanye ibada zao.
 
Mimi nilikuwa specific kwa Uislam tu sio kwa sababu nyingine za umaskini. Huko Shinyanga unakosema hakuna waislamu wengi hivyo mfano wako hauswihi kwenye hili. Nenda vyuo vikuu ukaone walimu na wanafunzi walioko huko utajua namna waislam wasivyofanya juhudi kwenye elimu ingawa wako wengi pia nchini. Sasa fanya utafiti ni kwanini wako wachache huko chuo kikuu wakati walikuwa wengi zaidi kwenye shule za msingi.
 
Sijui unaongelea zama zipi? Hivi hao wachoma vitumbua wote ni waislamu? Na kuhusu sherehe za kidini, kuna mikesha mingapi kwa upande wa pili au unaiona kwa waislamu tu?

Ukizungumzia maskini nchi hii, hutaji kundi fulani la dini tu, zaidi ya 70% ya Watz bila kujali itikadi zao na maeneo watokayo ni masikini, hivyo kama kigezo cha 'umasikini' ni sababu ya watoto kutokupelekwa shule basi usibague wala kuchagua, kapu ni moja.

Wewe unaona 'ubaya' tu kwenye hizo mambo za waislamu na huamini kama kuna jema lolote, ndio maana unahitimisha unavyohitimisha. Sasa kama ndivyo, hapo sina cha kukusaidia.

Kwa ufupi, unachokisema hakiakisi uhalisia.. Au labda unajadili kwa muktadha wa Dar na Pwani tu? Hebu nenda Shinyanga, Musoma, Kagera, Mara na vijiji vinginevyo visivyo ukanda wa Pwani halafu useme watoto wote wa maskini wanaenda 'madrassa' ndio maana wanakosa elimu dunia..

Nachelea hili likiishiwa hoja, mtahamia kwenye misikiti. Mtataka watu wasifanye ibada zao.
..... pamoja na maendeleo ya sayansi na technogia ambayo inawawezesha watu kwenda na kurudi Mecca kwa siku moja jamaa bado palepale pa .....fungeni kwa kuuona mwezi kwa macho yenu wenyewe!!!
 
Unahamisha magoli..!
 
Unahamisha magoli..!
Sheikh sayansi wala geography hamna, maandiko : msafiri asifunge, technolojia: ila msafiri aliyepanda bus au ndege afunge tu haina neno. maandiko yanagongana na technolojia
 
Unahamisha magoli..!
Kaka magoli hayahamishi, ila hali yetu waislamu sio shwari kielimu hivyo kiajira, hivyo kiuchumi, hivyo keki kubwa ya taifa inaliwa na wengine.
 
Dunia imegeuka geukieni elimu dunia kwa watoto wenu wa Kiislam kwa vitendo. Geuzeni madrasa zenu kuwa vituo vya elimu ambako watoto wanafunzwa masomo ya dini, hesabu, english, sayansi, historia, na ufundi badala ya kulazimisha watoto wenu wakariri (wahifadhi) Quran pekee wakiwa wadogo sana umri uleule ambao watoto wengine wako bize na kujifunza A B C D na 1, 2, 3,.... Umri mdogo ni muhimu sana kwa watoto kuhamasika kujifunza kitu chochote.

Nimefanya utafiti wangu mdogo kwa watoto wa kiislamu nikagundua kuwa wale wanaoimba taarab, muziki, wakata mkaa, wamachinga, na walinzi wa usiku wengi wao wamepitia madrasa hizi lakini wamekosa elimu, ajira rasmi na mitaji ya kufanya biashara kama wale wenzao waliopitia madrasa pia lakini wana asili ya Asia kama vile waarabu, wahindi, wapemba, nk.

Hii ina maana kuwa elimu ya madrasa haitoi ajira, ujuzi wala mitaji ya biashara kwa watoto wanapokuwa watu wazima hasa kwa watoto ambao hawana asili ya Asia. Yaani waislamu weusi wengi wao wanakosa elimu, ujuzi na mitaji ya biashara wanapofikia umri wa kujitegemea na matokeo yake watanyakazi yoyote bila kujali elimu ya dini waliyoipigania na kuihifadhi vifuani walipokuwa watoto kwenye madrasa hizi.

Hii ni tofauti kabisa na watoto wa kiislamu wenye asili ya Asia ambao watakuwa na elimu ya dini na ujuzi na mitaji ya kufanya biashara. Wengi wao weusi wenye elimu kubwa ya kidini wanaishia kugombania uimamu misikitini na kutupiana majini, kuwa waganga wa kienyeji na wapiga ramli na makafara ili kujipatia riziki.

Wazazi wa Watoto wa kiislamu weusi (Waafrika) lazima wawe makini sana kwenye elimu za watoto wao wakiwa wadogo, maana samaki anakunjwa akiwa mdogo, wapeni watoto elimu zote za dini na dunia kwa wakati mmoja utotoni ili kuwapunguzia adha ya kuwa wazindikizaji wa wenzao kwenye maisha watakapokuwa wakubwa, maana elimu ya dini haitoi ajira ya kutosha kwa vijana wengi.

Wewe ni zaidi ya mbulula kiwango cha lami. huu uzi umeandikiwa au umecopy somewhere? toa ushuhuda maana hapa nlipo nkiwa na miaka kumi nilishahifadhi zaidi ya juzuu tatu, shule nilikua natusua kama kawaida.hata hao unaodhani tangu wakiwa wadogo walikua wakifundishwa A, B, C ..... kwangu sikuwapa nafasi ya kunisogelea kitaaluma. achaga undondocha wewe simbilisi.kwa kukusaidia fuatilia shule za hao watu uone ufaulu wao ijapo wamebase pia kwene madrassa.

ELIMU DUNIA KAMA USEMAVYO NI MINOR FACTOR KAMA KIGEZO CHA UCHUMI WA MTU.
 
tunajenga nyumba moja tusigombee fito: Sijasema waislamu hawana akili lahsha na wala sijasema watu wasiihifadhi dini yao, waislamu wana akili nyingi sana ndio maana wana uwezo wakuhifadhi juzuu kadhaa kifuani tena kwa ufasaha, ila shida hapa ni wazazi wa kiislamu, wengi wao hawahimizi wala kutoa mazingira mazuri kwa watoto wao kusoma elimu dunia ambayo hata Mtume aliitilia muhimu, hata mimi nilisoma shule baada ya kutoroka madrasa (kwa sheikh) nilikopelekwa na baba kusoma dini tu kwa miaka 3 mfululizo nikiwa mdogo sana. Baada siku moja sheikh wangu kuniambia aya ambayo Mtumbe alihimisa watu waitafute elimu hata Uchina ambako hakukuwa na waislamu ndiyo nikaanza kumhoji masuala mengi sana yaliyopelekea mimi kutoroka na kwenda shule hadi nikapata PhD na sasa nauchangia uislamu wangu vizuri kwakuwa ninapata rizki zangu kwa wepesi kabisa. Mtume SAW alikuwa anafahamu kuwa dini yake haitakamilika kama watu hawataitafuta pia elimu ya Wachina, maana alijua kuwa Sayansi itakuja kubadilisha maisha na mambo ya wanadamu siku za mbeleni, alijua uvumbuzi mkubwa utakuja kutokea huko siku za mbeleni ambao msingi wake ni elimu ya Uchina, alijua huko mbeleni kutavumbuliwa vitu kama saa, magari, ndege, satellites, radio, television, simu, vipaza sauti, speakers, n.k ambavyo vitakuja kubadilisha baadhi ya mambo kwenye uislamu lakini bila kuathiri misingi ya Uislam. Sasa Sheikh ambaye hajatii amri ya Bw. Mtume ya kuifafuta elimu ya Wachina ana la kujibu mbele ya Mtume SAW, na haswihi kuwa Iman mbele ya umma huu wa sasa ambayo elimu ya Wachina imetamalaki katika kila sekta ya maisha ya muislam. Ni vizuri kusikia kuwa unafanya vizuri darasani, sasa sijui idadi yenu mko wangapi darasani waislamu wa sampuli yako? Wahimize wenzako waige alichokihusia Mtume kwenye elimu ya Uchina, hasa wale ambao familia haijui chochote kuhusu biashara wala sehemu ya kupata mtaji wa kufanya biashara kama ilivyo kwa wengine.
 
tatizo lako wewe kavulata unafikiria zaidi dunia lkn sisi waislamu tunafikiri zaidi akhera that's why watoto wetu huwafunza qurani kwanza then mengine yafuate!! Leo hii taasisi kama the Islamic foundation wana shule nyingi sana za awali,primary, na secondary pia Al Akhii nurdin kishki (Allah amuhifadhi) kupitia taasisi yake ya Al hikma ana shule zinazotoa elimu bora na vyuo vimejengwa na vinaendelea kujengwa imma kuhusu bakwata hao wanajulikana waziwazi kuwa Ni taasisi ya serikali kiasi kwamba hata mh magufuri amewaambia pia wabane matumizi na wakapangiwa idadi ya wawakirishi!!
ndugu zangu waislamu tusiache kuwapa watoto wetu ilmu ya akhera kwani ndio muongozo kamili wa maisha yetu just imagine mtu hajasoma sekula lkn amesoma dini na akafanya mema je akifa ataingizwa jahannam kwa kosa la kutokusoma sekula? na je mtu akasoma tu sekula na kuiacha dini wewe unategemea huyu mtu ataishi vipi hali ya kuwa qurani ndo muongozo wetu
baraka llahu feykum
 
Aliyesoma sana quran halafu akakosa kipato atafuga majini yanayodhuru watu na kuandika matalasimu na makombe, si ndiyo? Bw. Mtume hakuwa mjinga aliposema tafuteni elimu hata ikibidi Mashariki ya mbali. Shule za kiisilamu watoto huwa wanakumbwa na majini kila wakati, watoto wanavuta bhangi na walimu wao, na ufaulu uko chini sana nidhamu hakuna. Ninaweza kukuorodheshea baadhi ya shule hizo halafu uniambie ipi iliwahi kuwa kwenye 10 bora kwa ufaulu kitaifa kwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Pitia vyuo vikuu vyote nchini ukiacha vya Zanzibar halafu orodhesha idadi ya walimu na wanafunzi waliosoma quran kisha ilinganishe na wale walimu na wanafunzi ambao hawajui hata alifu bee tee ndo utajua ninachokisema mimi na unachokosea wewe. Pamoja na uchache wao lakini tunahitaji wataalamu wa mahesabu, marobani na ndege za kutupeleka kuhiji, madaktari, waendesha mitambo, wahandisi, watengezeza vipaza sauti na speaker, n.k. Kwasasa watu hao wengi na vitu hivyo vingi vinatoka na kutengenezwa na wagalatia.
 
Back
Top Bottom