Ushauri: Kuwa msiri katika mambo yako yahusuyo fedha!

Ushauri: Kuwa msiri katika mambo yako yahusuyo fedha!

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
6,475
Reaction score
11,674
miaka ya zamani ni nadra sana kukuta mtu anatoka bank anavamiwa na majambazi wenye silaha za moto..
lakini kwa sasa haya matukio yameshika hatamu hadi inatisha..ilianza taratibu sasa imekuwa kawaida mtu kuvamiwa mchana kweupee.

njia mojawapo itayokusaidia kuepuka kwa asilimia kubwa ni USIRI.japo sio kwa asilimia zote
USIRI katika mipango yako utakuepusha na watu wasio waaminifu.

unaingia Bank unatoa million 20 uende kununua samani..or unaenda kununua shamba or kuwanja.au nyumba
huduma ndani ya bank inachukua kama nusu saa..
unatoka nje paap!! bastola umenyooshewa "achia bag hilo!!
ukileta ubishi wanakutwanga!

sasa baada ya hapo shutuma kwa bank teller..ooh anashirikiana na majambazi yuleee..
possibility ya hili ni 20%
huko nyumbani ulivoondoka ulimwambia nani na nani unaenda labda mlimani city kutoa mamilioni?mke wako?shemeji ako?
rafiki ako? unaefanya nae biashara?
why bank teller tu?
bank teller unafahamiana nae?
wakati unajaza withdrawal form alikua anaona kutoka kule alipo?
umekaa foleni labda dakila kumi..ulipofika dirishan ilichukua labda dakika kumi hadi unapewa pesa zako..alitumia muda gani kuwapigia majambazi? linganisha hili na muda ulotumika kukuhudumia had unasepa
majambazi yalichukua dakika ngapi hadi kufika hapo ulipo?pikipiki zilipaa?
au labda wako around maeneo hayo mda wote wanajuzwa

lakini nataka ujue..inawezwkana hata jirani yako anawasiliana na majambazi wakufuatilie
inawezekana hata ndugu yako akawasiliana na majambaz
hata mke au mume wako pia.
rafiki ndo kabisaa.

jifunze kuwa msiri kwenye mambo yako..usimwamini binadamu mwenzako
mbele ya pesa utu huyeyuka ghafla.hasa kipindi hiki cha magu hali ngumu..wanapora hadi laki
ni ushauri tu

visanga nlivoshuhudia:
-kuna mdada alikua na mume..mume akamjuza mkewe nimenunua nyumba kwa million 40 maeneo ya buguruni..kesho yake mume namba haupatikani..ndugu na wafanyabiashara wenzie wanamtafuta..mke yuko nyumbani anadai mumewe alisafiri
mara kesho anadai mume alienda ukweni kwa wakwe yupo nae
baada ya wiki anadai mume anaumwa yupo huku ukweni
baada ya siku chache polisi wakaenda ukweni katika pekuapekua wakakuta mwili wa mume unaelea ndani ya kisima..una jeraha. mke kajipeleka ukweni kwa mume analia anataka awekwe eda.[emoji19] [emoji19]

ndugu walipatana kuuza shamba la urithi kwa mill 15.siku ya makabidhiano ya pesa wakapewa.mmoja akamvuzia mwenzie akampiga na shoka kichwani akamfukia na kulimbia na zile pesa

unamkumbuka yule mama wa mabwepande aloshirikiana na houseboys kumuua mme wake na kumfukia kisha akjipeleka polis kuripot mume kapotea?kisa mill 40?

mmekaa tu hivi ndani..hakuna anaejua kama kuna pesa ndani zaidi ya nyinyi lakini ghfla mnavamiwa toeni hela..walijuaje?
yuda iskariote is amongst you!
PESA MWANAKHARAM!

BE CAREFUL .TRUST NOBODY MBELE YA PESA..

ITS JUST AN ADVICE..
 
haya mambo ni magumu, ukioa unaambiwa mmekuwa mwili mmoja na unapata pesa unaziweka mezani mshirikiane mipango.

ila roho ya ubinafsi imetujaa, unamwambia mtu kumbe nae anapanga kukupereka kibra
acha kabisa..utu hakuna siku hizi
akiambiwa kat ya million mia na wewe..achague kimoja.
unadhan atachagua nini?

ila wapo walio na hofu ya MUNGU.
 
wacha hela zibakie kuwa benki tu.....
tembea na hela kidogo maana wakikukuta watakukata kata kama hauna hela ya kuwapa
 
Binafsi siamini hata kivuli changu,binadamu ni kiumbe dhaifu..lolote laweza tokea muda wowote mbele ya pesa.
 
Kwenye Karne hii ya teknohama bado mtu unabeba million 20 kwenda kununua kitu? Andika check au hamisha kwenda akaunti yake.

Watu siku hizi hawatembei na mahela mfukoni. Ndio maana utekaji wa Mabasi umepungua pia.
 
Back
Top Bottom