Ushauri kuhusu wazo la huu mfumo

Jobek2

Member
May 16, 2023
72
77
Habari wanabodi,

Shida ya hii forum unaweza kuomba ushauti mijitu inakutazama tu

Twende kwenye Mada
TZ na dunia nzima wafanyabiashara na wanunuzi wanakutana na barrier ya uaminifu.Hasa wanunuzi waliombali na muuzaji lets say mikoa tofauti.

Kwa kuona hiyo.Ndipo zinakuta technology ya Ecommerce.Zipo site nyingi za Ecommerce kama ebay,Amazom,Alibaba,kikuu, na nyingine nyingi.

Kupitia hizi ecommerce maarufu mnunuzi anaweza kununua kitu chochote akiwa sehemu yoyote ile duniani.

TOFAUTI na hizo ecommerce kubwa yani International kuna hizi za local kama Jiji, jumia, Kupatana.com hizi site na App zinatofauti kidogo kwani hutaweza kufanya malipo ya bidhaa moja kwa moja badala yake utawekewa namba ya muuzaji.

SASA WAZO NDIO LINAKUJA HAPO
Nini kinakwamisha ecommerce za bongo kutokuwa na payment gateway?

Na uzuri wake ni kwamba kwa kila bidhaa itayouzwa unakata % kadhaa.Mfano bidhaa inauzwa 10,000 tsh/ wewe unakata 500/ na mteja atakapo fanya malipo unaweka malipo PENDING..mteja atakapothibitisha kapokea malipo ndio nawewe unaruhusu malipo kwa muuzaji ndivyo wengine kina Amazon hufanya hivyo kuepusha wizi!!?

Sasa kwa uelewa wako hapa bongo ugumu utakuja wapi kwenye kutengeneza mfumo kama huu wa kuuza na kununua.Wewe unakuwa kama mtu wa kati tu unaemuunganisha mnunuzi na muuzaji

Sidhani kama nimeeleweka kwakua nimeandika kwa spidi ya jet bila kufanya marejeo ya bandiko ila kama umepata concept karibu tujadili.
 
Amazon wanauza mizigo yao kwa kiasi kikubwa, wana magodown yao kibao hawana huo utaratibu ila Alibaba naskia wana huo utaratibu ulioelezea

Hicho kitu kinaitwa Escrow, Mnunuzi analipia mali kwa mtu wa kati, Muuzaji anamtumia mali mnunuzi, mali ikifika kwa mnunuzi mtu wa kati anampa pesa yake muuzaji.

Shida inakuja kwenye vyombo vya sheria kuwa na msaada kidogo, muuzaji anaweza kutuma mzigo nae mnunuzi analipia kwako mtu wa kati, Picha linaanza hawa makanjanja unakuta mnunuzi kapokea kila kitu ila anabadili mzigo anaweka vilivyoharibika kisha anakuja kulalamika kwako kwamba mzigo umeharibika umrudishie hela yake, nae muuzaji anakuwashia moto anahitaji pesa yake ama arudishiwe mzigo aliotuma.

Ila ndio ujasiriamali huo, Risks hazikwepeki.
 
SASA WAZO NDIO LINAKUJA HAPO
Nini kinakwamisha ecommerce za bongo kutokuwa na payment gateway?
Zipo site unalipia moja kwa moja kabisa jaribu kudadisi vizuri utaziona, Ila sababu kuu ni kutokua na uaminifu wa bidhaa yaan unaweza ukaona bidhaa kwa picha ukaletewa bidhaa kwenye picha na uhalisia ni tofauti kwa hio anaedeliver ndio ataambiwa km mteja atalipia karidhia au halipii hajaridhia
 
Bongo hii nitajie ecommerce ya hapahapa TZ unayoweza kulipa mzigo direct moja kwa moja
 
  • Thanks
Reactions: PAS
Amazon wanauza mizigo yao kwa kiasi kikubwa, wana magodown yao kibao hawana huo utaratibu ila Alibaba naskia wana huo utaratibu ulioelezea

Hicho kitu kinaitwa Escrow, Mnunuzi analipia mali kwa mtu wa kati, Muuzaji anamtumia mali mnunuzi, mali ikifika kwa mnunuzi mtu wa kati anampa pesa yake muuzaji.

Shida inakuja kwenye vyombo vya sheria kuwa na msaada kidogo, muuzaji anaweza kutuma mzigo nae mnunuzi analipia kwako mtu wa kati, Picha linaanza hawa makanjanja unakuta mnunuzi kapokea kila kitu ila anabadili mzigo anaweka vilivyoharibika kisha anakuja kulalamika kwako kwamba mzigo umeharibika umrudishie hela yake, nae muuzaji anakuwashia moto anahitaji pesa yake ama arudishiwe mzigo aliotuma.

Ila ndio ujasiriamali huo, Risks hazikwepeki.
Aisee asante kwa ufafanuzi...Ni kweli changamoto kama izo apo sasa itabidi uwe na agent wa usafirishake kuna wale transporter wanafanya vizuri

Sasa mkuu swali lingine..Ni kwamba hiyo Escrow unaomba kwa kampuni lets say Crdb,Mpesa n.k au ni mfumo binafsi kama paypal ambao uwezi upata kwenye local payments..??kwasababu kibongo site kama hii inabidi iwe na malipo ya local kama Mpesa sijui Lipa namba ili uendane na waTZ
 
API za makampuni ya simu na bank unazilink mauzo yanaenda direct bila mbambamba,
 
Betting sites, BetPawa, sportpesa, kazijaribu
Sasa izo ni ecommerce mkuu? Na ukumbuke izo zinaenda direct kwa kampuni..So hujaelewa idea yangu ngoja nikufafanulie

Malipo ambayo na B2B yani direct yanaenda kwa Mtu na Mtu direct.Lakini hapohapo kwenye huo muamala unakata automatically asilimia zako kadhaa(% ) Na pia kuna sehemu ya kuhold malipo
 
Okay, Tunzaa from what i know mfano unataka kununua Ubuyu na unauzwa 5000, unaweza kuweka plan labda ya kununua huu ubuyu kwa siku 5 ambapo utakuwa unalipia Tsh: 1000 kila siku ili jumla ifike 5000 upate ubuyu wako. Thats what i know from Tunzaa,

Idea yako ya kudevelop hiyo Platfom ni nzuri by the way ila unatakiwa ucheze smart sana na uweze kutengeneza utofauti na trust. Inawezekana ila committment, kwasababu haitaishia tu kucode bali itahitaji kuuza and thats the most difficult part of business.
 
Tena nimetoka kureview hiyo tunza hapa..Wao ni B2C ile wanaita (Bussiness to Company) yani user(mimi na wewe) hatuwezi kuweka bidhaa zetu pale ni wao tu.Naona ni duka la mtu kaamua kujiendeleza kihivyo.

Mimi idea yangu ni both B2B na B2C yani kampuni au watu.utaweza kuuzia mtu direct..
 
B2C sio Business to Company, B2B ni Business to Business na B2C ni Business to Consumer, alafu Tunzaa sio duka la mtu ni fintech inayomuwezesha mnunuzi kununua vitu kwa kulipia kidogo kidogo, so inaLink any Business ambayo itajiRegister kuprovide service/product kwa Consumers. Soma vizuri.
 
Sasa izo ni ecommerce mkuu?
Unaelewa maana ya Electronic-Commerce? Maana sio unaandika ushubwada wako tu hapo,

Electronic commerce (e-commerce) refers to companies and individuals that buy and sell goods and services over the internet.

Wanaobet ni km wapo kwenye gulio, unajua gulio ni nini na linahusikaje na Electronic-Commerce?
 
Mimi idea yangu ni both B2B na B2C yani kampuni au watu.utaweza kuuzia mtu direct..
Unazitaji hizo alafu unakataa eti betting companies hasihusiani na e-commerce, Mzee shule ulienda kuusomea ujinga? Au neno e-commerce linakupiga chenga usijue kua hata services zinauzwa na kununuliwa sio goods only
 
Malipo ambayo na B2B yani direct yanaenda kwa Mtu na Mtu direct.Lakini hapohapo kwenye huo muamala unakata automatically asilimia zako kadhaa(% ) Na pia kuna sehemu ya kuhold malipo
Wewe hujui hio ipo kwenye betting companies, ukiingiza Pesa inaingia papo hapo uki-win unalipwa papo hapo na unaweza kutoa papo hapo, unanielewa lakini au umesomea kupinga kila unachokiona bila kufanya utafiti?

Yaan kuna watu watatu wewe, Serekali na betting company, wewe ukiingia ukabet ukashinda utapewa Pesa yako na kuna 10% inatumwa kwa Serekali km kodi papo hapo inaingia kwenye wallet ya Serekali, ushanielewa sijui? Ukishashinda unachukua Pesa yako km ilivyo yaan zile Pesa zimewekwa kwenye kitu kinaitwa E-Wallet yaan Electronic-Wallet, unanielewa sijui? Au nakuvuruga zaidi?
 
Free advice, kama umeona gap kwenye market taratibu tu build your digital product weka features unazoona ni suluhisho la tatizo lilikopo, ingiza bidhaa sokoni subiri matokeo, improve taratibu. Punguza focus na watangulizi wako bali jifunze kwa watangulizi wako uone nini wanafanya nawewe utafanya nini cha ziada kwa wanachofanya ili ufanye bora zaidi upate wateja.
 
Back
Top Bottom