Ushauri kuhusu ujenzi

M Priska

Member
May 10, 2020
17
11
Habari zenu ndungu zangu,

Ninauwezo wa kuweka akiba ya Laki 4 kila mwezi.

Nina kiwanja changu cha m 27 kwa 20 pale Mbezi ya Kimara.

Maswali yangu ni yafuatayo :
1) Je, naweza kujenga nyumba ya vyumba 4 hapo?
2) Nianzie wapi katika project ya ujenzi wangu? Ninunue kwanza matofali?

Shukran kwa maoni yenu wakuu!
 
Usisahau pia kufanya haya kabla ya ujenzi...
-Ramani ya mpango miji.
-Kusaka hati ya kumiliki kiwanja.
-Kibali cha ujenzi.

Ni mambo fulani (siyo ya lazima sanaaa!) yamekaa kipuuzi fulani, yanachosha kuyafikiria, lakini katika zama hizi za kuja kubomolewa bila kulipwa fidia wala kuhurumiwa, yana msingi mkubwa.
 
Unaweza kujenga lakini itakuchukua miaka kumaliza.

Unaonaje ukitafuta mkopo wenye riba nafuu ili uwe unakatwa kila mwezi walau laki mbili?
Mfano ukiweza kukopa 8-10 M utaweza utaweza kujenga vyumba 2 na sebule ukahamia kisha baadae ukaendelea na ujenzi wa nyumba kubwa au ukaacha matoleo.

Mkopo utaweza kurejesha kwa miaka 2 n.k


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu, na tayari kimesha pimwa na hati ninayo. Ila bado sina kibali cha ujenzi.
 
Mi sikuwa na kibali cha ujenzi,yani nilianza kichwa kichwa tu, wakati nimefika katikati wakaibuka hao jamaa wa kibali cha ujenzi...walinizingua sana wakasimamisha ujenzi badae wakanilipisha mpaka na penalty,sina hamu nao kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si mbaya, ila mikopo naiogopa hatari !! Hii laki 4 ni kwasababu ya hali ya Dunia kwa sasa ya Covid19. Mambo ya kikaa sawa, nitaweka zaidi ya hizo.
 
Aisee pole sana.. hicho kibali lazma nikitafute kabla ya yote.
 
Sawa mkuu, na tayari kimesha pimwa na hati ninayo. Ila bado sina kibali cha ujenzi.
Ili uweze kupata kibali cha ujenzi ni lazima uwe na mchoro wa ramani ya nyumba unaotaka kujenga.Lazima uwe umegongwa muhuri na registered Architect then utaipeleka kwenye ofisi ya halmashauri ya eneo kiwanja kilipo.

Kama hauna ramani Mimi ni Arcitect karibu tufanye kazi ntakuchorea na kukugongea muhuri pia ntakusaidia kufuatilia kibali cha ujenzi.tuchekiane kwenye 0756928360
 
Shukran sana, na save namba yako, nitakutafuta.
 
Ni kweli ila kwa mazingira yaliyopo hakika hata nyumba za kupanga zingekuwa hakuna kwa kuogopa hayo!
 
Mmuu servant kota nayo inahitaji kibali?
Na gharama za kibali cha ujenzi zikoje?
 
Kila kitu kinawezekana, kwa ushauri mwepesi sema na jirani yako aliyekwisha Jenga na muulize kuhusu fundi aliyemjengea na gharama zake ukishazipata ongea na fundi kirefu na asiwe huyo tu tafuta na mafundi wengine hata wanne utakayoyapata kwao utajua pa kuanzia na ikiwa kiwanja ni tambarale basi utatumia gharama nafuu zaidi, ila hiyo mitaa ni vizuri sana fundi kukuwekea kitako chini kabla ya kujenga tofali na kufunga mkanda ikiwezekana hata nguzo fup za msingi kwa kila kona!

kwa kuanzia weka msingi kwanza theni awamu ya pili unakimbiza mpaka kwa madirisha ukija ya tatu unaenda mpaka lenta theni unavuta pumzi ya kupaua!
 
Mmuu servant kota nayo inahitaji kibali?
Na gharama za kibali cha ujenzi zikoje?
Kwa kawaida kila ujenzi mpya unaotaka kujenga kama haupo kwenye kibali cha mwanzo unahitaji uwe na kibali cha ujenzi.Japo kuna watu wanajenga bila kufuata utaratibu.

Kuhusu gharama za kibali za ujenzi huwa zinatofautiana kutokana na halmashauri.Kuna baadhi ya halmashauri wanafanya sh 50000 kwa nyumba za chini.na kuna baadhi ya halmashauri wanachaji kwa square meter haizidi sh 500 kwa square meter moja
 
Asante kwa elimu. Vipi sasa kuna kampuni zozote ambazo unaweza ukawalipa wakutafhte kibali hicho?
 
Asante kwa elimu. Vipi sasa kuna kampuni zozote ambazo unaweza ukawalipa wakutafhte kibali hicho?
Ukiwa na Architect aliyehusika kukuchorea ramani yako atakuongoza kuanzia hatua ya kwana hadi mwisho jinsi ya kupata kibali chako cha ujenzi.Ushauri tu penda kutumia wataaramu husika kwenye kitu husika.inasaidia sana kupata matokeo chanya kwenye kitu unachokifanya.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…