Just talker
Member
- Jan 6, 2021
- 50
- 63
Siasa ni mchezo mchafu, siasa ni uadui na vita, siasa sio nzuri. Hayo ni baadhi ya maneno nimeanza kuyasikia kitambo sana hadi leo. Mwanzoni nilikuwa naamini hivo pia, sikuwahi kufatiria kwanza kabla ya kuyakubali ila kwasababu niliyasikia hata kwa watu wazima hiyo ikatosha kuniaminisha.
Nikiwa nimekuwa angalau mtu mzima (am 26 now) navutiwa sana na uhitaji wa maendeleo kwa ujumla (social, economic, political and technology) lakini najikuta ili kuwa miongoni mwa wafuasi wa maendeleo kuna uhitaji wa siasa, sasa kwanini nimeaminishwa kuwa siasa sio nzuri Wakati bila siasa sitapata maendeleo au siwezi kuwapatia kila maendeleo watu.
Nakumbuka nikamuuliza mtu mmoja akaniambia walioko kwenye siasa tayari wametosha hatakiwi mwingine kuongezeka.
Hakuniambia kuwa ni uharisia haitakiwi mtu kuongezeka ila kumekuwa na matukio mengi yasiyo mazuri ya kutishia amani baadhi ya wengi walioko kwenye siasa. Hii ikasababisha kukata kwa kiu ya wengi walio hitaji kuingia kwenye harakati za siasa.
Matukio kama ya kushambuliwa, watu kutekwa, watu kupotea na wengine kesi kibao zisizo isha mahakamani na polisi.
Matukio ya kuvunja mioyo ya wenye uhitaji wa kweli na tija ya kuyaleta maendelo kwa wananchi kwa kufanyiwa fitina kwenye kura na kuwafanya baadhi kuamini kuwa ili ushinde utakiwe kuwa chama flani ambacho labda huenda kisiwe kimekuvutia kwa namna moja ua nyingine ila itakuwa uhakika kuwatumikia wanachi baada ya kupita kwenye kura za maoni maana lazima ushinde hata kwa njia tofauti.
Maneno mengi na leo nimeamua niilete hapa JF kwasababu hapa kuna wanasiasa wengi mno, wenye experience na wasomi pia nikihitaji ushauri wa mambo ya fuatayo hapa chini.

- Mambo gani nizingatie, na mambo gani natakiwa kuyafahamu kabla na baada ya kuwa mwanasiasa?
- Upi ni ukomo/mipaka ya mwanasiasa (wapi anatakiwa na wapi hatakiwi)
- Natakiwa niwe na sifa zipi itoshe kuitwa mwanasiasa.
- Je, ni kweli sitatakiwa tena kuwa mtu flani au mwajiriwa kwenye sekta yoyote baada ya kuwa mwanasiasa.