Ushauri kuhusiana na hii ndoa

compute

New Member
Jun 4, 2012
4
0
Una mke wako wa ndoa ya Serikali/Kanisani/Kimila na huenda Mungu amewajalia mukapata mtoto/watoto. Lakini katika ndoa yenu mkeo anataka arudiane na mpenzi wake wa zamani. Unamwambia nikupe Talaka anakataa lakini usiku wewe ukiwa umelala yeye analala sebuleni na anaongea mambo ya kimapenzi na huyo mpenzi wake wa zamani. Mke huyu utamwelewaje? Wazazi wake wamewakalisha kikao pia wakamshauri kama anataka kurudiana na mpenzi wake wa zamani hiyo biashara haipo. Wazazi wanamtambua mume wake wa ndoa na siyo mpenzi wake wa zaman.i Naomba ushauri wana JF.
 
Hivi kwani ukitaka kutoa talaka lazima umuombe mke?...we endelea kushika pembe
 
Du, aisee unaweza kuona kwako kuna tatizo lkn ukiyasikia ya wengine unamshukuru Mungu!
 
Duh, hii kali yaani mke anafanya dharau halafu dume linabembeleza tu, kweli dunia inaelekea kubaya yaani wanaime tunakosa wivu, sasa ndoa ya nini na ilipatikanaje?
 
Pole sana kaka. Mpe Talaka kaka uanze maisha yako mpya , la sivyo utakua "Mume *****" .


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Aisee pole sana mkubwa, ila kweli najaribu kufikiria ushauri upi unataka nashindwa kuelewa. Chukua hatua hakuna ndoa hapo unapoteza Muda wako.
 
Duh, hii kali yaani mke anafanya dharau halafu dume linabembeleza tu, kweli dunia inaelekea kubaya yaani wanaime tunakosa wivu, sasa ndoa ya nini na ilipatikanaje?

Huko ndio kulazimisha ndoa kama ulikua hujui, hajaoa huyo ila analazimisha ndoa apewe heshima nje kumbe
ndani anataabika
 
Kuna watu wanapenda kuwafanya wenzao kama wajinga, anakufanya Mume ***** huyo, au wewe ndio kama kaATM chake ndio maana hataki kukuacha, ok, tuache hayo, huyo mpenzi wake wa zamani ana mke, au mchumba anayetambulika, kama hana, mpe talaka Mkeo mapema, aende kwa huyo bwana, na kama huyo bwana ameoa au ana mchumba anayetambulika kwao, kaeni kikao nyie wote wanne na baadhi ya watu wa kutosha kutoka kwenye familia zenu ili kieleweke kipi ni kipi, yaani na huyo mtu wa mpenzi wake wa zamani na familia yake wajue kinachoendelea chini ya kapeti mapema, msije leteana fujo later
 
Kama kwenye kikao watasema kuwa bado wanapendana na wanataka kurudiana, nyie ndio mtajua mfanye nini hasa, ili mkae kwa amani na furaha angalau
 
Kaka toka saa 13:56 ulipoweka hii topic mpaka sasa 19:10 Kama ingekua mimi tayari ningeshambandika Talaka kama 2 hvi. Na akileta ubishi kesho asubuhi mpige na ya 3 kabisa. Kazi kwako sasa.


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
duh kuna mkaka alipatwa na mkasa kama huo, ila yeye aliambiwa asimuoe huyo mwanamke mana alikuwa muhuni jama akabisha oohh kuchaguliwa mke na wazazi mambo ya kizamani.. mwanamke alikuwa anzungumza usiku na bwana wake kwa simu kitandani inabidi mumewe ndo atoke chumbani akalale ukumbini mbu wamle weeee.. mwisho alimuacha tu
 
Kaka kuna vitu vya kutaka ushauri, lakini vingine ni maamuzi ya hata bila kufikiria.

Lakini kwanini akaanza hiyo tabia? Hilo nalo ni la kulifikiria kwa undani wake. Lakini iwepo sababu au la, Huyo ni wa Kupiga Chini Fast hata kama anakulisha na mna watoto mia.

Bazazi ni Bazazi!
 
Back
Top Bottom