Ukweli ni kwamba miji mingi Tanzania inajegwa bila kuwa na ubunifu wa kuvutia hasa kwenye kudizaini bustani nzuri, minara, miti na maua pembeni mwa barabara nje na ndani ya miji.
Mara ingine mipango miji hupima vizuri na kutenga maeneo kama bustani lakini tatizo linakuja kwenye uendelezaji wa hizo bustani. Utakuta eneo limebaki wazi tu bila ya decorations za maana. Au unakuta barabara zinazotoka na kuingia ndani ya miji ziko tupu bila miti au bustani za maua pembeni mwa barabara.
Hivyo kama idara hii maalumu itaanzishwa jukumu lao kubwa litakua kuwashauri mipango miji, kufuatili maeneo ya wazi na kubuni mapambo ya miji huska, kutengeneza bustani nzuri, pembezo mwa barabara na hata kutengeneza minara ya miji.
Ni vema ukuaji wa majiji yetu ukaendana na uzuri wa madhari na sio kuzagaa kwa nyumba tu!
Hili nalo linahitaji USAIDS?
Haipendezi.
Sent using
Jamii Forums mobile app