USHAURI: Kuanzisha Jukwaa la Psychology na Philosophy

fokonola bokoyoka

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
966
638
Habari kwa mpigo!

Kwanza kabisa naomba nitoe salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki naTaifa kwa ujumla kwa ajali iliyotokea Rhotia-Karatu na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu kwa wote waliohusika. Mungu awape moyo wa uvumilivu na utulivu katika kipindi hiki kigumu kwa wanafamilia na mtu yeyote aliyeguswa!

"Raha ya milele uwape ee bwana na mwanga wa milele uwaangazi, wapunzike kwa amani. Amina."

Dhumuni la bandiko hili ni kushauri uongozi wa JF kuanzisha jukwaa linalohusu mambo ya Psychology na Philosophy. Ni mara nyingi napitia mabandiko muhimu na mazuri yanayoweza kusaidia members kujifunza mengi, naamini itakuwa kati ya majukwaa yenye mvuto zaidi ndani ya JF.

Naamini kuna wataalam wengi humu waliobobea kwenye huu uwanja na wangependa sana kutumia jukwaa linaloombwa kutupatia elimu hii na vilevile wapo wenye matatizo au ndugu, jamaa na marafiki wenye matatizo hayo ya kukosa wataalam watapata msaada.

Naomba kuwasilisha.

Asante.
 
Back
Top Bottom