VeroEretico
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 505
- 388
Mambo ya kudhurumika vipiSio lazima u save,unataka ku save ufanyie nini hiyo Pesa hilo ndio swali la kwanza?
Kama shida yako ni pesa ili ununue kiwanja, nenda kampuni wanazouza viwanja
chukua kiwanja uwe unalipa kila mwisho wa mwezi hela yako yote inaenda huko
ukimaliza deni kiwanja chako unacho! kiwanja kinaweza kua cha thamani hata ya 50m
lakini hujawahi shika 50m ya mara 1, lakini tayari una kiwanja chako.
AU
Unakiwanja unataka kujenga, Ushajua mahtaji ya nyumba yako,nenda hard ware iliyo karibu na site yako
wambie unalipia material then ukshamaliza kila kitu utakuja fata material yako,kila ukilipa unachukua risiti
kila hela unayopata mwisho wa mwezi peleka kwenye ile hardware, material yakitosha chukua gari nenda
kafate material yako yote peleka site Anza ujenzi,material yame cost zaidi ya 20m lakini ki uhalisia wewe bnafsi
hujawahi shka hata 10m ya mara 1,kwa hyo unaweza ukaona namna ya kufanya uka save pesa yako kwa namna hiyo
watu wanaweka hela bank kama hawana chakufanyia wakati huo,watu wana save kama hela haina kazi wakati huo
ila kama unajua una viporo kibao mbele yako,anza kuvipunguza kdg kdg kama nlivyotoa mifano hapo Juu kuja kushtuka
una vitu kibao vya maana na vya gharama lakini haujawahi hata siku 1 kumiliki pesa CASH yenye thamani ya mali unazomiliki.
Njia za ku save zipo nyingi hiyo nliyokupea mfano ndio njia ninayoitumia mimi kufanya maisha yangu,Haijawahi niangusha na wakati wote naonekana na pesa ila lait wangejua ninavyodunduliza,wangeufyata.
Maana unaweza ukawekeza mwenye store/ supplier/Duka akapata losse akafirisika ktk biashara zake inakula kwako