Ushauri juu ya Upatikanaji wa Fedha za Mirathi

Ushauri juu ya Upatikanaji wa Fedha za Mirathi

impelle

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
832
Reaction score
1,110
Habari ya sabasaba wadau
Nimekuwa mlezi wa wadogo zangu watatu(tunashare mama lakini baba tofauti) miaka miwili sasa, baada ya wazazi wetu kufariki yaan marehemu baba yao na marehemu mama yangu.Hawa watoto walizaliwa baada ya baba angu(yeye yupo hai) na mama yangu kutalakiana ,kila mmoja aliamua kuoa na kuolewa na hatimaye kuzaa watoto( nina wadogo zangu pande mbili,kwa kushare baba na kwa kushare mama).

Kama kichwa cha uzi hapo juu, toka mzazi wa hawa madogo afariki (baba yao alikuwa mtumishi) miaka 2 iliyopita ndugu zake walikaa kikao na kumchagua bibi yao tumbo moja na marehemu bibi yao kusimamia ufuatiliaji na upatikanaji wa fedha za mirathi kwa ajili ya watoto wa marehemu.

Mpaka feb 2017, huyu bibi alinipigia simu kunieleza kumpeleka dogo mwingine ambaye ametimiza miaka 18 ili tumfungulishe akaunti mpya, akanambia kwamba anadai fedha ya nauli na hela ya photocopies kwa yale anayoyafanya kufanikisha upatikanaji wa hizo fedha, nilimweleza mimi sina mandate na hizo pesa ila nikamshauri kama ataweza akomae tu,asubiri zikitoka basi atajilipa.,alihaidi kwamba mpaka mwezi aprili fedha zitakuwa zimetoka.

Tumeendelea kusubiri lakini tabia za huyu msimamizi zinanitia wasiwasi hasa anavyoonyesha kuniogopa na kunishawishi tushirikiane hasa mambo ya passwords za account za hawa watoto, mimi kinachonigharimu kwamba naishi na kati ya hawa wadogo zangu 2, mmoja namsomesha chuo cha ufundi,mwingine ndo anamaliza la saba mwaka huu,yeye ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa sana darasani.
Nimeandika kuomba ushauri wa kuchukua hasa kwa kuhisi nitazidi kulemewa na majukumu hasa huyu dogo mwingine nikimpeleka kidato cha kwanza shule za private na huyu mwingine nataka nikomae mpaka amalize diploma ndo atafute kazi au aolewe akitaka.
Huyu bibi na ndugu zake mimi siwajui zaid ya kuongea na bibi kwa njia ya simu.
Naombeni mnishauri tunapoelekea kufunga mwaka huu, kama madogo watakuwa hawajaletewa fedha zao ili ziwasapoti na mimi kunipunguzia majukumu kuendelea na mambo yangu mengine, nini nifanye, au nifanye nini kwa ajili ya wadogo zangu.

Tafadhali wenye uzoefu wa mambo haya ya mirathi hasa kutoka mfuko wa pensheni wa PSPF.
 
Back
Top Bottom