Ushauri juu ya mahusiano yangu

Eizyek

JF-Expert Member
Aug 12, 2019
297
1,000
Wakuu habari gani?

Mimi nilikuwa na mahusiano na binti mmoja since 2014, nilirusha ndoano na mahusiano yetu yakaanzia hapo. Kutokana na harakati za maisha na nini, mimi nilitoka mkoa ule na kwenda mkoa mwengine kiutaftaji kwahiyo mawasiliano yakawa mtiahani kutoka mwaka 2016 adi 2020 tukawa hatujawahi onana wala kuambiana lolote lile.

Mwezi wa 3 mwaka huu kama zali tu akapata number yangu akanichek mahusiano yakarudi upya kwa speed ya 4G, kiukweli ndoto zikaanza kupangwa na upya na mipango mingine ila hapo maana alikuwa na boy mwengine akasema ametamana naye.

Tatizo lilipoanza, nikichelewa kujibu text tu ni msala. Hajui nakuwa na shughuli ama nini anasema “sijui tuachane, sijui kimeenda kimerudi”. Najishusha tunaendelea ikafika time ikabidi nimweke wazi kwamba muda mwengine unavyotuma text nakuwa busy akaelewa.

Sasa jana kuna mtu kanipigia na kunieleza tabia za huyo binti. Kwamba huyo binti ni malaya sana na hajieshimu, mimi nikamuuliza ni kweli kuhusu wewe nilivyoambiwa, akaanza kupaniki kwamba basi tuachane sijui nini mimi nikabaki kimya

Imefika kipindi nimefikiria nimeona ni bora ni break up na huyu mtu kwanza anamarafiki wengi sana wa kiume na kila time anawapost

Ushauri wadau kwamba, je huyo mtu anaweza kuwa mtu sahihi kweli?


Sorry kwa uandishi mbovu
 

recycle Bin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,563
2,000
Fimbo ya mbali haiui nyoka mkuu, ni miaka imepita na hujui alikua anafanya nini na mawasiliano yalishakatika japo sio vibaya sana kwa sababu huwa inatokea ila usikilize moyo wako na ushirikishe akili yako ipasavyo kufanya maamuzi.
Binafsi ningemuacha.
 

manonawire

JF-Expert Member
Dec 31, 2017
871
1,000
bloo unawesa tuma ile elfu hamsini yule babu wa kijijni ameludi tufanye ule mchakato.

🚶‍♂️ 👣
 

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
7,021
2,000
Mbn kama tayari umeshajua ni nini unatakiwa kufanya mkuu..

Siku nyingine jitahidi usikosee herufi yoyote kwenye lugha ya kiingereza.andika kama inavyopaswa kuandikwa.

Mbwembwe za “L” na “R” uziache hukuhuku kwenye kiswahili chetu tutakuelewa🥂
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom