Ushauri: Jirani amekuwa akifungulia sauti kubwa ya redio

Dawa ya moto ni moto au kwa mwenyekiti utaonekana kiherehere si unajua mtaani noma sana we acha maneno weka Mziki sauti mpaka mwisho alafu wewe unaenda kukaa nyumba ya 10 kusikiliza
 
visa vya wajawazito huwa ni vingi ila akishajifunguwa unaweza mkuta saut ya mtoto jumlisha ya redio anachagua moja redio anairudisha kwenye box analea

mbenee mimba tu :) kwa liavatar tu si haba my dear
 
Shukran mkuu nimekuelewa
 
Nafuatilia thread nipate mrejesho nami yupo ananisumbua sana na misauti ya redio yake mpaka huwa muda mwingine natoka nakaa nje

Unajua pa kupata yale maspika ya matangazo??????? Ila lazima uingie gharama.....

Unamfungia segere la usiku kucha mwenyewe unaenda kulala hoteli ya jirani.....

Siku 1 tu harudii tena
 
Unajua oa kupata yale maspika ya matangazo??????? Ila lazima uingie gharama.....

Unamfubgia like na segere la usiku kucha nwenyewe unaenda kulala hoteli ya jirani.....

Siku 1 tu harudii tena
Looh! hilo si nitafanya mtaa mzima ukeshe kwa disco maana siku hizi mziki tu sherehe watu wanajipangia
 
haina haja ya kuomba ushauri mkuu.. hapo ni BAMBA tu BAMBA akizima.. we kakodishe hata zile za sherehe.. fungulia had mwisho halaf weka ile nyimbo ya K ni K romaaaaa!!!!!
 
Nimeshindwa hii inshu niiweke kwenye jukwaa gani, nikaona hata hapa si mbaya sana, nina Jirani yangu tunaishi nyumba tofauti lakini ziko karibu, yeye kila ikifika saa moja asubuhi ni mama wa nyumbani huamka na kufungulia sauti ya juu sana kiasi kwamba kama ulikuwa umelala lazima utaamka, imekuwa ni tabia yake ya siku nyingi, nikaamua nimfuate kwa ustaarabu nimwambie naomba awe anaweka sauti ya chini, akanielewa baada ya wiki akarudia tena.

Nikamfuata kwa Mara ya pili nikamuomba tena na anapoweka sauti ya juu, ni kuanzia SAA moja asubuhi hazimi redio hadi SAA moja jioni ndio hupunguza sauti na kuweka ya kawaida hata akienda Dukani au mbali kwa masaa kadhaa, ataacha ikiwa hivo kitendo hiki kimenichosha hadi nimeamua yafuatayo:

Nimeamua ikifika usiku wakati yeye ndio amepunguza sauti na mimi ndio niwashe sasa yangu coz anawahi sana kulala ili nimsumbue na yeye apate kero kama tunayopata sisi, je nitakuwa nimefanya makosa?

Naomba mnipe ushauri njia ya kufanya tafadhali, ukizingatia mama mwenyewe ni mjamzito muda wowote anajifungua, nishawaza tena nimsubiri ajifungue ili akiwa na mtoto mdogo hatataka kelele na mimi ndio niwashe sabufa yangu sasa, nitakuwa nimekosea?
Polee
Wajawazito bana ndo walivyo kwo mvimilie yuu
Huna haja ya kufungulia saut kubwa kwamba unamkomesha laahasha
 
Kanunue Mashine ya kusaga then iweke btn you houses, ikifika saa 4 usiku unawasha.....ukimpelekea huo moto akiendelea hama.
 
Transparency will set free your soul, tell her so that you can be free rather than being quite
 
Nimeshindwa hii inshu niiweke kwenye jukwaa gani, nikaona hata hapa si mbaya sana, nina Jirani yangu tunaishi nyumba tofauti lakini ziko karibu, yeye kila ikifika saa moja asubuhi ni mama wa nyumbani huamka na kufungulia sauti ya juu sana kiasi kwamba kama ulikuwa umelala lazima utaamka, imekuwa ni tabia yake ya siku nyingi, nikaamua nimfuate kwa ustaarabu nimwambie naomba awe anaweka sauti ya chini, akanielewa baada ya wiki akarudia tena.

Nikamfuata kwa Mara ya pili nikamuomba tena na anapoweka sauti ya juu, ni kuanzia SAA moja asubuhi hazimi redio hadi SAA moja jioni ndio hupunguza sauti na kuweka ya kawaida hata akienda Dukani au mbali kwa masaa kadhaa, ataacha ikiwa hivo kitendo hiki kimenichosha hadi nimeamua yafuatayo:

Nimeamua ikifika usiku wakati yeye ndio amepunguza sauti na mimi ndio niwashe sasa yangu coz anawahi sana kulala ili nimsumbue na yeye apate kero kama tunayopata sisi, je nitakuwa nimefanya makosa?

Naomba mnipe ushauri njia ya kufanya tafadhali, ukizingatia mama mwenyewe ni mjamzito muda wowote anajifungua, nishawaza tena nimsubiri ajifungue ili akiwa na mtoto mdogo hatataka kelele na mimi ndio niwashe sabufa yangu sasa, nitakuwa nimekosea?

Umenikumbusha nyumba za kupanga na vimbwanga vyake! nilikuwa na mpangaji mwenzangu yeye mziki mpaka mnachanganyikiwa, enzi hizo akina madilu, franco, papa wemba, Kofee, awillo, yaani ilikuwa bandika bandua mpaka nikajua kilingala. solo la byeee

Nilimripoti kwa mwenye nyumba wapi hasikii, nilichofanya nikapanda darini nikaunganisha swich ya umeme wa kwenda kwake ikaja chumbani kwangu.. akifungua mziki sauti ya juu namzimia umeme yeye tu tokea chumbani kwangu, mwishowe akasalimu amrii! alikuwa akiwasha radio kwa sauti ya chini inaongea akiongeza sauti ya juu umeme unakatika kwake tu..
Mafundi njaa wakamwambia radio inataka umeme mkubwa ndio maana ukiongeza inakata umeme..
Ikawa ndio mwisho wa ujinga wake

Nakushauri Kama mmepanga kamripo kwa mwenye nyumba, na asipo sikia tafuta mzee mwenye busara ambaye yeye anamheshimu peleka malalamiko yako kwake ili aongee nae na wewe ukiwepo..
Asipokusika tena jaribu kupita sheria za air polutions zinasemaje kuhusu kelele..ila kama ni uswazi pole sana" acha maneno weka muziki"
 
Back
Top Bottom