USHAURI: Jimbo la SEGEREA apewe J. Mtatiro

USHAURI: Jimbo la SEGEREA apewe J. Mtatiro

KIBARAone

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
642
Reaction score
243
Kwa heshima na taadhima nakiomba chama changu cha CHADEMA kikubali kumpa huyu Mwana harakati jimbo hilo na kwa jinsi alivyojipanga hilo jimbo litaenda UKAWA.

Nimeamua kutoa ushauri wa aina hii kutokana na uwezo mkubwa aliona katika kujenga HOJA katika kuchambua mambo ya kisiasa na kielimu. Hivyo nasi ingependeza zaidi kwenye bunge lijalo awe miongoni mwa wabunge machachari katika bunge la jamhuri ya Tanzania.
 
NA JIMBO LA ILALA APATIWE !
**MUKADAMU WA CUF ANAKUBALIKA SANA**

NB/ HAKUNA MUDA WA KUTEST AU KUBIP!

PEOPLE CHOICE MATTERS
ii
 
Ileje hakuna NCCR , CDM ndiyo yenye nguvu lakini amepewa NCCR...

Ni suala la maridhiano tu...

Tafakari...

mkuu nimeishi segerea kwa muaka 18; naijuwa vema! watu wasegerea wanachaguwa chama badala ya mtu. pia kulitokea kutokuelewana kwa viongozi wa CUF na wa chadema; ikasababisha Kila chama kum simamiusha mgombea wake kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa
 
kbosho...

Ndiyo maana nikatumia neno MARIDHIANO...

Ikitokea pakawepo maridhiano ya viongozi ni rahisi kuwaelimisha wafuasi wakaelewa...

Tafakari...
 
Kwa heshima na taadhima nakiomba chama changu cha CHADEMA kikubali kumpa huyu Mwana harakati jimbo hilo na kwa jinsi alivyojipanga hilo jimbo litaenda UKAWA.

Nimeamua kutoa ushauri wa aina hii kutokana na uwezo mkubwa aliona katika kujenga HOJA katika kuchambua mambo ya kisiasa na kielimu. Hivyo nasi ingependeza zaidi kwenye bunge lijalo awe miongoni mwa wabunge machachari katika bunge la jamhuri ya Tanzania.

Mimi ni mkazi wa Segerea, na kwa kiasi kikubwa sana huku watu wana chagua chama zaidi kuliko hata mtu, na kwakuwa ninamkubali sana Mtatiro kwa uwezo wake wa kujenga hoja, ningewashauri UKAWA ili wawe na uhakika wa kulipata hili jimbo, MTATIRO angejiunga na CHADEMA kwa kipindi hiki halafu wampe fursa ya kugombea ubunge, kwa utaratibu uleule walioutumia kumpa BABU DUNI ugombea wenza kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Jimbo hilo keshaandaliwa mwanasiasa nguli Makongoro Mahanga. Sisi tunachagua chama, si mgombea kwa hiyo atapita tu. Tumwache Edo na watu wake nao wapate majimbo ili mafuriko yaendelee.
 
Ileje hakuna NCCR , CDM ndiyo yenye nguvu lakini amepewa NCCR...

Ni suala la maridhiano tu...

Tafakari...

Mkuu pia mipango imefanywa mfano Bagamoyo wameoewa cuf kulingana na ckuwa inakubalika lakini mgombea anayekubalika ni wa CDM hivyo leo atachukuwa kadi ya CUF na kugombea
 
Naunga mkono Mtatiro yafaa awe kwenye bunge la JMT
 
Jimbo hilo keshaandaliwa mwanasiasa nguli Makongoro Mahanga. Sisi tunachagua chama, si mgombea kwa hiyo atapita tu. Tumwache Edo na watu wake nao wapate majimbo ili mafuriko yaendelee.

Kama ni makongoro bora liende kwa wenzetu cuf, nakumbula machungu ya 2010 na hapa amekuja kwa uchu wa madaraka tu
 
Back
Top Bottom